Kitu kinachotupa bei, katika uchumi, ni makutano ya curves za demand na supply, ceteris paribus (all factors being equal).
Katika curves za supply/ demand zinazotupa price kwenye uchumi, kuna abnormal curves.
Kawaida, katika free market, kwa ceteris paribus, price ikiwa chini watu wengi wanakuwa na uwezo wa kununua kitu, demand inakuwa kubwa kuliko supply, bei inapanda mpaka demand, supply na price vinapo stabilize.
Kwa mfano wa Mlimani City, bei za chini zinaweza kujaza watu hapo mpaka ikawa vurugu, pakawa hapakaliki. Na wenye biashara wakiona kwamba kuna wateja wapo hata tukipandisha bei, watapandisha, mpaka pale watakapoona hapa sasa tukipandisha zaidi tutakosa wateja.
Kawaida kitu kinavyozidi kuongezeka price, demand inazidi kupungua.
Lakini, kuna abnormal curves zipo katika vitu kama "luxury goods", kuna vitu vingine vikiwa na bei ya juu ndipo watu wanavitaka, vikiwa na bei ya chini inaonekana kama feki.
Yani inawezekana kitu kisiwe na chochote cha ajabu, ila ile branding tu inafanya bei iwe juu, na watu wanaotaka kujionesha wana hela za kununua vitu vya bei ya juu watanunua.
Ndiyo maana unasikia Kanye West katoa raba inauzwa kwa dola za Marekani 350! Na watu wanaunua, wanataka waonekane wamevaa kitu cha bei mbaya.
Kwenye sehemu za starehe, kuna watu wamejijengea mawazo kwamba sehemu zenye vitu vya bei rahisi zitajaa watu wasio na hela wenye matatizo mengi na wasio na ustaarabu, na kwamba ukienda sehemu za vitu vya bei mbaya utaepuka kukutana na matatizo ya ku socialize na watu wa ngazi za chini za jamii.
Inawezekana hapo Mlimani City/Samaki Samaki panafuata abnormal curve ya "luxury goods/services".
Ila Mlimani City kwa mfano Samaki Samaki kusema unatanua kiota cha maraha naona bado sana.
Nilipelekwa na wadogo zangu nilivyorudi likizo, kufika tu, mwenyewe najua hapa hakuna mtu anayenijua, mchizi mmoja akaanza kupiga kelele kama kaona jini ananiita jina langu, anawaambia watu "mnamjua huyu nani? Mnamjua huyu nani?" kama vile Prince Akim kwenye "Coming To America", nikamwambia cool down, you are putting me on the spot.Jamaa hakutegemea kabisa kuniona pale kwa sababu nilikuwa nimejichimbia nje miaka 10 kabla ya hapo.
Kwa hiyo labda kama sehemu inayoweza kuwakutanisha watu waliotengana siku nyingi, watu wakajua kwamba pale ndipo wanyamwezi wote tunaoshuka Dar tutafika, panaweza kuwa na maana.
Na tukirudi na hivyo vidala vyetu, hizo juisi za sh 5,000 hata USD 2 hazijafika bado, kwa hiyo hatuoni cha ajabu kulipa kama hilo litamaanisha tunakutana na long lost friends.
But the place could be better.