Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Naomba kuuliza maswali mawili 1) ni lini mtaingiza station za radio za Tanzania maana watumiji cc ni watanzania 2) kwanini ving 'amuzi vingine vina lugha ya kiswahili na vingine vina kifaransa na kiingeraza tu??? 0629088763

habari yako mkananguja kuingizwa kwa radio za Tanzania kunategemea pia na utayari wa watoa huduma, startimes tunapenda wateja wetu wapate huduma hipi. Pia unaweza kubadilisha lugha katika king'amuzi chako kwa kwenya SETTING kisha chagua LANGUAGE unayotaka
 
Habari mnaona hiki changu nilinunua 82900/= TZS mwaka 2011 sasa je na hiki kinahusiana vipi nakuzimwa na kunibakishia TBC 1 tu pekee kama free channel ina maana nyie data hamna za ku track hizi vitu au mnafanya kazi kwa mazoea?
20171230_104944_rmedited.jpg
 
Habari yako kwabwina pole sana kwa usumbufu unaoupata

Startimes tuna ving'amuzi vya aina mbili cha kwanza ni "FTA decoder" bei ya king'amuzi hiki ni Shilingi 89,000, ukiwa na king'amuzi hiki utafurahia chaneli zote za ndani bure kwa muda wote, hii ni kwa mujibu wa sheria na muongozo toka kwa mamlaka husika ikiwemo TCRA.

Kutokana na gharama ya 89,000 kuonekana kubwa na watu wengi kushindwa kuimudu, na ili kuhakikisha kila mtanzania anafurahia huduma ya Television bila kujali uwezo wake startimes kwa kuzingatia maombi na pia maoni toka wa wateja iliamua kupunguza bei ya ving'amuzi na kuwa na kingamuzi chenye bei maalumu, startimes ikaweka ving'amuzi vyenye bei maalumu 'STARTIMES SUBSDIZED DECODER', bei yake ni bei ya chini kulinganisha na bei ya soko (unalipia shilingi 34,000 kupata king'amuzi hiki, hii 34,000 ni hela ya huduma tu) , lengo kubwa ni kuhakikisha mteja anapata na king'amuzi kwanza. kupitia king'amuzi hiki mteja analipia gharama ya huduma tu ambayo anaweza kulipia kwa siku, wiki au mwezi ili kupata chanel za ndani na chaneli za nje.

Lakini baadae mteja mwenye king'amuzi hiki 'SUBSDIZED DECODER' akipata fedha anaweza kukibadilisha kuwa king'amuzi cha FTA, mteja anaweza kukibadilisha kwa kufika katika duka letu la startimes lililo karibu yake na kulipia 'PRICE DIFFERERENCE' (Tofauti ya bei kati ya SUBSDIZED Decoder na FTA Decoder) yaani 89,000-34,000 ambayo ni 55,000. ukifanya hivyo utakuwa sawa na aliyenunua king'amuzi cha FTA utafurahia chanel zote za ndani bure muda wote.

Startimes tumekuwa tukijitahidi kuwaeleza wateja wetu kabla hawajanunua ving'amuzi vyetu, tofauti ya ving'amuzi hivyi ili kumpa nafasi mteja kufanya chaguo sahihi, lakini tumekuwa tunapata changamoto nyingi sokoni kwani mawakala na maagenti wetu wengi hawatoi taarifa hizi kwa wateja ipasavyo. Tafadhahari tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ulioupata kama hukupata maelezo haya, Pia tunakukaribusha katika duka la startimes kwa ajili ya kubadilisha king'amuzi chako kuwa cha FTA. Startimes tutaendelea kufuata sheria na mwongozo toka kwa mamlaka husika

Ahsante!
Hamjaamua kuwaunganisha wateja wenu wote kwenye huduma ya FTA. Kama mmeona wateja hawana hela na mmeamua kuwalipisha hiyo hela kila mwisho wa mwezi kwa channneli za bure ni zaidi ya wizi. Je, TCRA wanataarifa juu ya mpango wenu au ndo njia yenu ya kuwapiga wananchi kwa kisingizio cha kusema "wantanzia wengi hawana hela".

Ushauri wangu kama mmeona umasikini ni kikwazo cha kuuza kwa bei halali fanyeni mpango wa kila mwisho wa mwezi mteja anapolipa mnakata asilimia kadhaa ili kufidia bei ya king'amuzi alichonunua, pindi pesa halali imetimia mnamuachia chanel zake za local lakini siyo hivi mnavyofanya ni zaidi ya uhuni.
 
Kile king'amuzi kilichokua nasikia ni tsh 135000/ kimeshuka mpaka tsh 89000/ naomba ufafanuzi tafadhari
 
Ila startimes bwana yaani mpaka najuta kununua king'amuzi chenu make tangu nikichukue yaani siwasomi kabisa kila nikinunua kifurushi chenu naambiwa nimenunua cha wiki tu,hivi inakuaje mnakuwa na milolongo mirefu hivi?

Kiukweli mnatupa usumbufu sana sisi hasa Wateja wapya yaani hata hizo channel za ndani salio likikata kila channel unaambiwa haijalipiwa.

Jaribuni kujirekebisha mtatufukuza kwenye Huduma zenu hizi.
Wenu mteja.
 
Habari zenu star times
Mm ni mkazi wa mbagala nzasa Dsm
Mmiliki wa kisimbuzi namba
018 1939 5671

Mimi ni mteja wenu tangia enzi na enzi Kabla hamjaleta TV zenye visimbuzi mm nilikiwa na nyie mpaka sasa mmeshazileta nipo na nyie nahisi record zangu mnazo huko.

Shida yangu au lalamiko langu la kwanza ni jinsi mnavyokuwa nyumba ktk kujibu malalamiko yetu kupitia huduma kwa wateja namaanisha tunavyopiga cm na mnavyokawia kupokea kingine ktk page zenu nikianzia na facebook pamoja na hapa mnakawia sana kutoa majibu kwa wateja wenu.

Tuachane na hayo shida yangu kuwa ipo ktk kunitolea channel za dini ya kiislam. TvIman siioni na Africa TV siooni tatzo nini.

Kingine naitaji kulipia jTv naomben mwongozo
 
Imma swala lingine naomben kama inawezekana msimu ujao mtuwekee EPL
Na ktk kuonesha kwenu baadhi ya ligi kwann msitumie lugha adhim ya kiswahili
 
Hamjaamua kuwaunganisha wateja wenu wote kwenye huduma ya FTA. Kama mmeona wateja hawana hela na mmeamua kuwalipisha hiyo hela kila mwisho wa mwezi kwa channneli za bure ni zaidi ya wizi. Je, TCRA wanataarifa juu ya mpango wenu au ndo njia yenu ya kuwapiga wananchi kwa kisingizio cha kusema "wantanzia wengi hawana hela".

Ushauri wangu kama mmeona umasikini ni kikwazo cha kuuza kwa bei halali fanyeni mpango wa kila mwisho wa mwezi mteja anapolipa mnakata asilimia kadhaa ili kufidia bei ya king'amuzi alichonunua, pindi pesa halali imetimia mnamuachia chanel zake za local lakini siyo hivi mnavyofanya ni zaidi ya uhuni.

habari yako MimiTena kama tulivyoeleza juu, startimes tulizingatia vipato vya watu tofauti ndio maana yule anayeweza kununua cha kuonyesha za nyumbani ananunua moja kwa moja, lakini yule ambaye hana fedha kwa wakati huo tunampa bei maalumu ambayo baadae akipata pesa anakuja kumalizia baadae wakati anaendela kupata service!
 
Imma swala lingine naomben kama inawezekana msimu ujao mtuwekee EPL
Na ktk kuonesha kwenu baadhi ya ligi kwann msitumie lugha adhim ya kiswahili

habari yako farujeuri tunashukuru kwa maoni yako, hakika yatafikishwa idara husika, Kuhusu EPL bado tunatambua hili na uongozi mzima wa startimes unafanyia kazi. startimes tunajitahidi sana kuwaletea SPORTS mbalimbali, tegemea hivi karibuni kupata WORLD CUP kupitia startimes pekee!
 
Habari zenu star times
Mm ni mkazi wa mbagala nzasa Dsm
Mmiliki wa kisimbuzi namba
018 1939 5671
Mimi ni mteja wenu tangia enzi na enzi Kabla hamjaleta TV zenye visimbuzi mm nilikiwa na nyie mpaka sasa mmeshazileta nipo na nyie nahisi record zangu mnazo huko...
Shida yangu au lalamiko langu la kwanza ni jinsi mnavyokuwa nyumba ktk kujibu malalamiko yetu kupitia huduma kwa wateja namaanisha tunavyopiga cm na mnavyokawia kupokea kingine ktk page zenu nikianzia na facebook pamoja na hapa mnakawia sana kutoa majibu kwa wateja wenu.

Tuachane na hayo shida yangu kuwa ipo ktk kunitolea channel za dini ya kiislam.... TvIman siioni na Africa TV siooni tatzo nini.....
Kingine naitaji kulipia jTv naomben mwongozo

habari yako farujeuri tunashukuru kwa maoni yako hapa! kwa sasa tumeboresha huduma na matatizo yote yatapatiwa majibu kwa muda muafaka idara zote ikiwemo Callcenter, facebook, instagram na hapa JF.

Pia kuhusu TV imani mkataba wetu na TV iman uliisha, na sisi kama startimes haturuhusiwi kurusha chanel bila kuwa na ridhaa ya wamiliki, hivyo tunajitahidi kwa sasa kuongea na wahusika ili tuirudishe!
 
Habari mnaona hiki changu nilinunua 82900/= TZS mwaka 2011 sasa je na hiki kinahusiana vipi nakuzimwa na kunibakishia TBC 1 tu pekee kama free channel ina maana nyie data hamna za ku track hizi vitu au mnafanya kazi kwa mazoea?
View attachment 663506

habari yako Mediocrist, pole kwa usumbufu ulioupata, ni kweli inaonyesha kingamuzi chako ni kile kinachotakiwa kuonyesha chanel za bure, tafadhari fika katika ofisi ya startimes iliyokaribu new ili waweze kukusaidia.

STARTIMES mara nyingi hatupendi kumwambia mteja alipie kabla hatujajua tatizo ni nini!
 
Mbona hizi channels ambazo TCRA wamesema ni lazima zioneshwe hata kama mtumiaji hajalipia hazioneshwi. Je ni kwa nini?
 
habari yako mkananguja kuingizwa kwa radio za Tanzania kunategemea pia na utayari wa watoa huduma, startimes tunapenda wateja wetu wapate huduma hipi. Pia unaweza kubadilisha lugha katika king'amuzi chako kwa kwenya SETTING kisha chagua LANGUAGE unayotaka
Habari star times,

Nimekuwa mteja wa kisimbuzi X (jina nalihifadhi) kwa muda sasa, lkn sifurahii matangazo yao, sasa nimeamua kuwa moja ya familia yenu!

Napenda kujua yafuatayo;

Mosi, bei yenu ya ving'amuzi ( mm Niko Nyegezi mwanza)

Pili, ubora wa vipindi vyenu (program zenu zikoje)

Tatu, bei ya malipo kwa mwezi (yaani vifurushi vyenu vinaanzia tsh ngapi)

Asanten sana naomba majibu pia!
 
habari yako chambimagaka, karibu sana startimes

Bei za vingamuzi vyetu!
upload_2018-2-5_10-23-13.png

na bei ya vifurushi vyetu ni kama ifuatavyo
upload_2018-2-5_10-26-6.png

angalia mchanganuo huu kwani unaweza kulipia malipo ya siku wiki na mwezi pia, gharama za kifurushi kwa mwezi ni hizo zilizo kwa rangi nyekundu
 
Back
Top Bottom