Habari yako
kwabwina pole sana kwa usumbufu unaoupata
Startimes tuna ving'amuzi vya aina mbili cha kwanza ni "FTA decoder" bei ya king'amuzi hiki ni Shilingi 89,000, ukiwa na king'amuzi hiki utafurahia chaneli zote za ndani bure kwa muda wote, hii ni kwa mujibu wa sheria na muongozo toka kwa mamlaka husika ikiwemo TCRA.
Kutokana na gharama ya 89,000 kuonekana kubwa na watu wengi kushindwa kuimudu, na ili kuhakikisha kila mtanzania anafurahia huduma ya Television bila kujali uwezo wake startimes kwa kuzingatia maombi na pia maoni toka wa wateja iliamua kupunguza bei ya ving'amuzi na kuwa na kingamuzi chenye bei maalumu, startimes ikaweka ving'amuzi vyenye bei maalumu 'STARTIMES SUBSDIZED DECODER', bei yake ni bei ya chini kulinganisha na bei ya soko (unalipia shilingi 34,000 kupata king'amuzi hiki, hii 34,000 ni hela ya huduma tu) , lengo kubwa ni kuhakikisha mteja anapata na king'amuzi kwanza. kupitia king'amuzi hiki mteja analipia gharama ya huduma tu ambayo anaweza kulipia kwa siku, wiki au mwezi ili kupata chanel za ndani na chaneli za nje.
Lakini baadae mteja mwenye king'amuzi hiki 'SUBSDIZED DECODER' akipata fedha anaweza kukibadilisha kuwa king'amuzi cha FTA, mteja anaweza kukibadilisha kwa kufika katika duka letu la startimes lililo karibu yake na kulipia 'PRICE DIFFERERENCE' (Tofauti ya bei kati ya SUBSDIZED Decoder na FTA Decoder) yaani 89,000-34,000 ambayo ni 55,000. ukifanya hivyo utakuwa sawa na aliyenunua king'amuzi cha FTA utafurahia chanel zote za ndani bure muda wote.
Startimes tumekuwa tukijitahidi kuwaeleza wateja wetu kabla hawajanunua ving'amuzi vyetu, tofauti ya ving'amuzi hivyi ili kumpa nafasi mteja kufanya chaguo sahihi, lakini tumekuwa tunapata changamoto nyingi sokoni kwani mawakala na maagenti wetu wengi hawatoi taarifa hizi kwa wateja ipasavyo. Tafadhahari tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ulioupata kama hukupata maelezo haya, Pia tunakukaribusha katika duka la startimes kwa ajili ya kubadilisha king'amuzi chako kuwa cha FTA. Startimes tutaendelea kufuata sheria na mwongozo toka kwa mamlaka husika
Ahsante!