Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

StarTimes Tanzania,
Mlianza kuiondoa TV ONE mlipopigiwa simu mkasema kuna marekebisho mnafanya, mkaja mkaiondoa CLOUDS na chaneli zingine mlivyopigiwa jibu likawa lile kuna marekebisho mnafanya zitarudi lakini mpaka leo hazijarudi nini tatizo?

Rudisheni chaneli hizo pia ingizeni chanel E.
 
Napenda documentaries ila naona mmeondoa NatGeo na Viasat. Whats wrong, halafu mi mtanzania mnanijaziaje channel za naijeria badala ya kuniwekea atleast channel za Tz na East Africa! Mna mpango gani pia kuongeza news channels kama RT na France 24
 
Mmenijazia channel ambazo wala sijui hata lugha zao, hiyo tisa kumo mbona mnapenda kurudia tamthilia hivi? Hiyo so much love mmeirudia tena, double Kara na nyingine ndo kusema hakuna nyingine ama? Mnaudhi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napenda documentaries ila naona mmeondoa NatGeo na Viasat. Whats wrong, halafu mi mtanzania mnanijaziaje channel za naijeria badala ya kuniwekea atleast channel za Tz na East Africa! Mna mpango gani pia kuongeza news channels kama RT na France 24
Star times wameweka channel za Nigeria tu...wameondoa channel nzuri kama mimi napenda musiv..ila wametoa BET, The kiss, ST.Music

Marketing yao ni zero...MTV base eti hata ukilipia kifurushi cha 21k huruhusiwi kuona...kuna shida wanayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Peleka shauri lako TCRA


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
StarTimes Arusha mnapatikana channels mbili tu,TBC na Channelten.Huu ni mkakati maalum wa kuhujumu vyombo vingine Vya habari nini?
 
Mimi Nina tatizo kuhusiana na huduma zenu natumia king'amuzi Cha star times lakin Kuna baadhi ya channel zimefutika kabisa hazionekani mfn: St swahili

Sent using Jamii Forums mobile app

hello habari yako, je zimefutika kabisa haziko kwenye orodha ya chanel au zipo lakini hazionyeshi? je unaishi wapi na unatumia king'amuzi cha dishi au antena?h
 
StarTimes Tanzania,
Habari Startimes,
Mimi ninatumia dish na ninaishi Kahama vijijini,
Tatizo langu,
1- Ni kwanini wakati wa mvua channel zote huwa hazioneshi ?

2- Tabia yenu ya kuweka matangazo yenu ya biashara ya biashara wakati ninapopiga simu huduma kwenye namba yenu ya kwa wateja huwa inanikera sana ukizingatia kwamba muda huo ninaulipia, kwanini muweke matangazo yenu wakati mtu anapiga simu ili kupata msaada?

Na kwanini huduma hiyo ilipiwe ?, kwa nini isiwe Toll free ?, makampuni mengine kama ya simu huduma kwa wateja huwa hailipiwi, kwa nini nyie ?
 
StarTimes Tanzania, Habar Mm natumia king'amuz cha star times cha dish mbona nyny hudum zenu hamuja zi baranc kwa maana mm mwenye kinga'amuz cha dish Tv1 mmezitoa, clouds na Tv E ila m2 mweny king'amuz cha antena anazpat 2ambien kati ya dish na antena kipi kina thaman kweny ma2miz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
StarTimes Tanzania,
Asanteni kwa kuanzisha uzi huu, ninaomba ufafanuzi wa vifurushi na ikibidi menu ya idadi ya channels anazopata mteja baada ya kufanya malipo.

Mfano mimi nimelipia sh 16000 nimepewa chanel zisizozidi 20 hapo tukitoa zile za bure kama 8 au 9 zinabakia chanel kati ya 10 au 11, hapo sijajua kama ni halali au numepunjwa. Naomba ufafanuzi
 
Nina mwezi tu sasa toka ninunue king'amuzi cha Startimes cha dishi.

Nilichoona kifurushi cha NYOTA+ kwa maana ya kulipa shs 11,000/=hakina channel ya kidini ya Kikatoliki, wana ST Gospel, Deen TV, Iqraa na Dome TV.

Channel ya Katoliki kwa maana ya EWTN ipo kwenye vifurushi vinene vya "Smart" shs 21,000/= na "Super" shs 36,000/=.
Nimewapigia kuwaomba watufikirie wanyonge Wakatoliki kwani si wote 'wanene'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…