Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Mie natumiwa meseji ,kuwa nisipolipia kuanzia tarehe 15/10/2015 nafungiwa,kwa nikilipia baada ya tareh hiyo narudishiwa huduma?
 
Nipo mufindi Iringa,channels kadhaa zikiwemo ITV,TBC1,IROKO,CHANNEL10,etc zimepotea,hata kwenye channel list hazionekani.Wahudumu wenu wananipa majibu ambayo hata hayanisaidii.02139222989.
 
Habari, nimeshawatumia malalamiko mengi kwenu kwenye wallpage hii but sijapata majibu toka kwenu, Naishi majohe kwa ngozoma. King'amuzi kuanzia asubuhi kinaandika no Signal ikifika saa moja kinafanya kazi vizuri tuu, natumia atena ya ndani ile yenye sumaku. Ila nilikinunua zamani sana hata kabla ya kuhamia kwenye mfumo wa ving'amuzi jee? inaweza kuwa sababu ya kuwa ni OLD VERSSION. Nipeni jibu nijipange kutokana na jibu toka kwenu wataalam.

Weka antenna ya nje
 
Naomba Ufafanuzi Kuhusu King'amuzi Changu Tokea Juzi Ni Mwendo Wa Smart Card Error Tu!! Nazima Na Kuwasha Mara Kwa Mara!! Inatulia Na Kurejea Vile Vile Tu, Je Tatizo Ni Nini!!! Maana Ni Cha Muda Mrefu Saaana!! Vile Vya MWANZONI Kabisaa!!
 
King'amuzi cha startimes cha dishi kimeanza kuganda picha hakikua hivyo mwanzo tatizo nini?
 
Mi nataka kutumia USB DVB TV TUNER kwenye laptop/tablet nafanyaje??, kama ni kulipia nalipiaje maana channels zote ziko locked except ST Guide ndo inanyesha?.
Msaada tafadhali.
 
Kwanini hakuna clouds tv kwenye king'amuzi cha antena kwa mkoa wa Mwanza wakati Dar es salaam inapatikana acheni ubaguzi wa namna hiyo!?
 
mi nmelipia kama mara mbili hv na kila nikilipia naangalia wiki moja tu tayari mnanikatia channel kwa nini? sasa hivi nimeshakata tamaa kabisa ya kulipia
 
mi nmelipia kama mara mbili hv na kila nikilipia naangalia wiki moja tu tayari mnanikatia channel kwa nini? sasa hivi nimeshakata tamaa kabisa ya kulipia

Hii hata mimi imeshanikuta sana,nalipa kifurushi cha mwezi baada ya wiki mbili wanakata hata mwezi hautimii,ebu tuambieni ni nini hiki?
 
Mbona hamjibu maswali??, huku mnasema mnatafuta wateja mko serious kweli!!!!.
 
Hii hata mimi imeshanikuta sana,nalipa kifurushi cha mwezi baada ya wiki mbili wanakata hata mwezi hautimii,ebu tuambieni ni nini hiki?

Am not working with Startimes but i think i can ans this, kama upo subscribed kwenye package ya letsay 20,000 per month na umekuwa ukitumia hvyo ikitokea siku unalipia 10,000 nia ikawa kulipia package ya 10,000 bila kuwaambia wabadili package u will remain in package ya 20,000 per month so ur money will be enough for two weeks so the main problem hapa ni kubadili package according to price, kitu ambacho they must explain to customer ila hawafanyi
 
Nashukuru kwa kujaribu kuwajibia ingawa wenyewe wamekaa kmya!ni hivi mimi cjawahi kulipa kifurushi cha mwezi zaidi ya kile cha elfu10 na cjawahi kubadilisha toka tuhamie digitali na huwa nalipa kwa ajili ya mtoto kuangalia katuni tu,vinginevyo huwa napenda kuangalia local chanelz tu.
 
Nimenunua king'amuzi juzi tuuu na kwenye package ya local chenel TBC, channel ten na clouds tv ziliorozeshwa kwamba zitakuwepo. Cha ajabu ni kuwa hazipo kabisa. Je hili linakuwaaje
 
KWANINI STARTIMES CHANNEL YA STARTV INAKATAKATA SAUTI SANA BAADA YA TAARIFA YA HABARI.ri zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

Ahsanteni sana na karibuni nyote[/FONT][/SIZE][/B][/COLOR][/QUOTE]
 
Natumia satelite dish, Startv na TV1 zinascratch sana hasa nyakat za usiku, nimewapigia weee wananikalisha hewan km dakika tano pasipo kupokea halafu wananikatia simu. Kiukweli Startimes huduma zenu ni HOVYO kabisa!
 
Back
Top Bottom