Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

kwa bahati mbaya mteja akikosea NO. za king'amuzi chake wakat wa kurecharge kunautaratibu gani ili kurudishiwa iyo pesa aliyotuma kwenu ?

Habari yako, tunamifumo mizuri ya kuhakikisha mteja akikosea malipo anapata msaada, tafadhari endapo utakosea wasiliana na watoa huduma wetu 0764700800/0677700800 ukiwa na namba sahihi na namba uliyokosea, tafadhari kumbuka pia kuwa na namba ya muamala
 
Kifurushi cha Kuniwezesha kuangalia Mechi zote za WC ni kama Shilingi ngapi?

habari yako endesha, kama unatumia decoder ya antena kuanzia kifurushi cha mambo "13,000" au kama unatumia king'amuzi cha dish kifurushi cha smart "18,000" utafurahia mechi zote 64 za world cup
 
Decoder yangu imezima ghafula na fundi kasema imeunguza IC Je nikinunua Nyingine natumia card yangu Ile iletu? Maana kunakifurushi changu naomba majibu.

habari yako, je unaishi wapi? tupatie namba yako ya smart card tafadhari!
 
Ikiwa mteja kaibiwa king'amuzi chake na mwizi anaendelea kukitumia na kulipia kwenu mnamsaidiaje aliyeibiwa kupata king'amuzi chake? Je aliyeibiwa akija na RB mnaweza kumpa namba za simu za mwizi wake?

habari yako, tafadhari fika katika duka la startimes ukiwa na Lost Report, Kitambulisho chako, namba yako ya smart card pia
 
habari,nataka nibadili kingamuzi changu kutoka kwenye antena kwenda kwenye dishi, garama ni tsh ngapi.
 
habari,nataka nibadili kingamuzi changu kutoka kwenye antena kwenda kwenye dishi, garama ni tsh ngapi.

Habari yako Ocran mifumo ya ving'amuzi hivi ni tofauti, ingawa chanel nyingi zinafanana isipokuwa katika dish zipo zaid, kwa sasa unaweza kununua king'amuzi cha Dishi sh 38000 tu bila dishi, dish ni shilingi 40,000!
 
habari yako mpatto, tafadhari tutumie namba yako ya mawasiliano, tukupatie fundi
@StarTimes Tanzania , nashukuru kwa kuonyesha kunisaidi!! Ninafuraha kusema kuwa tatizo lile nilipata ufumbuzi nalo!!

Kumbe king'amuzi kilikuwa kimefungwa, hivyo niliwapigia startimes nao wakakifungua!!

Ahsanteni sana!![emoji120][emoji120]
 
habari bei ya kingamuzi na dish ni shilingi 78000 tu,

Startimes ndio waonyeshaji rasmi wa kombe la dunia Tanzania

ukilipia kuanzia package ya 18,000 utapata mechi zote katika mfumo wa HD kwa lugha ya kiswahili

tafadhari kama uko tayari tupatie namba yako
0713220660
 
Nita tv flat aina ya ZEC ina king'amuzu ndani niki search napata channel zenu za startimes je naweza kujiunga bila ya kutumia king'amuzi na kama inawezekana utaratibu upoje?
 
Startimes mbona channel za world sports, world premium mmeondoa kweny kifurush cha Mambo?

Je zinapatikan kweny kifurush gani?
 
nina kisimbusi cha startimes kile cha enzi za mwalimu nilikiweka ndani bila ya kukitumia muda mrefu sana maana nilinunua kipindi kile ndio vinaanza sasa nikakikumbuka miezi miwili iliyopita nikaja hapo ofisini kwenu bamaga mkaniambia kuwa card inatakiwa kubadilishwa ila kwa bahati mbaya ziliwaishia siku hiyo hivyo nikashindwa kupata hiyo kadi mpya,ila mkaniambia kuwa nikiweka kifurushi nitaziona channel kupitia kadi hiyohiyo mpaka zikiwa tayari zimefika ntakuja kulipia hivyo nikanunua kifurushi nikarudi zangu nyumbani,kama mnavyojua nyie startimes hamuishi mauzi niliporudi nyumbani nikaunganisha kisimbusi ktk tv daaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhh niliambulia kuona local channel tu ila kile kifurushi mpaka kinaisha sijaona channel nyingine zozote nikaamua kukiweka tena lockup ila leo nimefikiria kuwapa last chance nataka nikitumie sasa niambieni hiyo kadi bei gani ili kama namudu gharama nije kuchukua muda huu maana nataka nione worldcup mwezi huu maana nyie kwa kubadili bei ghafla mnaongoza


namba ya smart card ni 020 3593 9630


kisimbusi changu ni cha antena
 
Back
Top Bottom