Status WhatsApp yazua balaa kwa mume mwenye wake wawili

Status WhatsApp yazua balaa kwa mume mwenye wake wawili

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
14,705
Reaction score
30,041
Ukiwa mume mwenye mke zaidi ya mmoja basi kila hatua unayochukua inakubidi uitafakari mara mbili. Hayo yametokea jana baada ya baba mwenye mji wake kumpost mke mdogo kwenye Status WhatsApp

Baada ya mara kwa mara mume kumpost bimkubwa status akaona leo ngoja nimrushe bimdogo nae hewani auze sura,lauhaula! Hilo jambo lilikuwa kosa kubwa sana kwa bimkubwa,kama unavyojua bimkubwa kwa mtazamo wao ndio kama wamiliki halali wa mume huyo,na bimdogo wanamchukulia kama mtu tu aliyeingilia kati penzi au ndoa yao.

Jioni hiyo baada ya bimkubwa kuona mwenzake kawekwa status,kwanza kabisa alimpigia mumewe na kumwambia leo hapiki chakula na kama ikiwezekana mume huyo asirudi nyumbani jana hiyo kama vipi akalale popote anapokujua yeye

Kwa jamaa yangu huyu jana ilikuwa siku nzito sana kwakwe,na sijui kama jana jamaa aliichapa kweli? Hayo ndio mambo ya uke wenza bwana, ukiwa na wake zaidi ya mmoja basi unatakiwa uchukue tahadhari kubwa sana kwa kila hatua unayochukua hasa hasa ikihusisha wake zako.

Ni hayo tu!
 

Attachments

  • 8CAD7FFC-EA8A-4620-A6A6-DC6E05CC79F5.jpeg
    8CAD7FFC-EA8A-4620-A6A6-DC6E05CC79F5.jpeg
    315.6 KB · Views: 20
Huyu Mwanamume na hao wake zake wote wanasumbuliwa na akili za kitoto,

Kifupi wamekutana Pipa na Mifuniko.
Mume anasema alimuuliza mkewe mbona wewe nakupost mara nyingi,kwani unafikiri mwenzio haoni? Na sio kwamba aliyepostiwa ni mchepuko, ni mke mwenzake,lakini ndio raha ya uke wenza ,lazima kuwe na Kashi kashi
 
Mume anasema alimuuliza mkewe mbona wewe nakupost mara nyingi,kwani unafikiri mwenzio haoni? Na sio kwamba aliyepostiwa ni mchepuko, ni mke mwenzake,lakini ndio raha ya uke wenza ,lazima kuwe na Kashi kashi
Ndio maana nikasema wamekutana Pipa na mifuniko,

Mwanaume anayejielewa hawezi kupost picha za wake zake sijui huko status,hayo ni mambo ya wavulana,

Anapost picha za wake zake ili nani aone? Kama sio ujinga ni nini zaidi? Akitombewa aanze kulalamika.
 
Back
Top Bottom