Status za RIP Pele

Status za RIP Pele

MwakiIV

Member
Joined
Aug 31, 2018
Posts
79
Reaction score
138
Ulimwengu wa Soka umefikwa na msiba mkubwa sana wa Mwanasoka ambaye amekubalika kuwa bora aliyewahi kutokea duniani Edson Arantes do Nascimento almaarufu Pele.

Waswahili wengi wamekuwa wakiweka picha kwenye status zao za whatsapp na maneno kama RIP King na majina mengine mazuri.

Swali ni je, nani anaona hizo status? Lengo ni nini?

Ama ni trend ambayo usipofanya utaonekana mshamba na uliyenyuma ya mambo?

Ni kweli ulimjua Pele kiasi cha kumuweka kwenye status zako?

Nifunzeni wanajamii tafadhali.
 
Nashangaaa ,najiulizaa ni ulimbukenii ama ni nini hivi ukiwa na huzuni kupita kiasi utaweka hata status,mtu huyo ukimwuliza tu pele ana wastani wa goal ngapi kwa match moja hana jibu ila anataka kuonekana anajua vitu

Daaah apumzike kwa amani
 
Nyie mnaoshangaa hao wanaoweka status (mwanandinga Pele) ndo waajabu. Hivi unawashwa nini na ushamba wa mtu mwingine, kwanza hujachangia bando lake, humjui na hata kama unamjua kwa nini uingilie starehe yake?
 
Nina status 500+ hapa naona vipicha vya Pele na sija view hata moja maaanina
 
Back
Top Bottom