SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy. Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.

1702990351854.png
 
Tunachokijua
Stendi ya Mabasi ya Magufuli ni kituo kikuu cha Mabasi ya masafa marefu kinachopatikana katika Jiji la Dar es Salaam. Kituo hiki kilizinduliwa na Hayati Magufuli mnamo Februari 21, 2021 aliyekuwa Rais wakati huo na kituo kikapewa jina lake kama heshima kwake.

Tangu Desemba 16 kumeibuka uvumi unaodai kuwa Stendi ya Mabasi ya Magufuli imebadilishwa jina na kuwa na kuitwa Dar es Salaam Bus Terminal. Uvumi huu ulianza kutokana na picha iliyotumiwa na Habari Leo wakieleza mapato ya kituo hicho kwa siku. Tazama hapa chini:

img_9962-jpeg.2846494

Picha inayosambaa ikihusishwa na kubadilika jina kwa Kituo cha Magufuli
Picha hiyo ilisambaa zaidi na kuibua mijadala katika mitandao mingine. Mathalani, katika Jukwaa la JamiiForums.com ikiwamo mleta mada hii (JF Member) na Mirindimo waliibuka na kuhoji kwa lengo la kutaka kujua uhalisia wa uvumi huo.

Je, kuna ukweli kwenye uvumi huo?
JamiiCheck imepitia vyanzo vya mbalimbali ikiwamo Google image Search na kufika kituoni hapo imebaini kuwa uvumi wa kituo cha Magufuli kubadili jina hauna ukweli wowote.

Kupitia Google image Search JamiiCheck imebaini kwamba picha hizo zinazovumi zilikuwapo mtandaoni tangu Februari mwaka 2021 na zilipigwa kabla ya kituo hicho hakijabadiliwa jina kutoka kuwa Dar es Salaam Bus Terminal na kupewa jina la Magufuli.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefika eneo la kituo hicho ili kuhakiki kama jina la kituo hicho kimebadilika lakini imekuta bado kituo hicho kinaitwa Magufuli Bus Terminal kama ilivyokuwa tangu kituo hicho kilipopewa jina hilo mwaka 2021. Hizi hapa chini ni baadhi ya picha ambazo zimepigwa leo Desemba 19, 2023:

1702969669112-jpeg.2846856

Picha ya kituo cha Mabasi ya magufuli iliyopigwa Desemba 19, 2023
Sio rahisi hilo jambo kufanyika, kumbe wengi hata hamjui matukio ya Kisiasa kulingana na nyakati.

Ina maana hamjui yule Mzee ameacha wafuasi zaidi ya 10M plus Nchini? Zile ni Kura

Na CCM inajua kitendo cha kufanya huo upuuzi kunaweza kuwanyima kura 2024 na 2025.

Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na hii Propaganda.

Kama mnadhani masihara ajitokeze mtu tuweke 500k kila mmoja tufanye betting
 
Utateseka sana lakini huwezi kubadili ukweli...
JPM alishinda kihalal na hata sasa kiwekwe kivuli chake, kitashinda

Nikikuambia uoneshe matokeo ya kura alizopata utatoa?. NEC yenyewe mpaka Leo haijaweka matokeo ya urais au kupublish matokeo haiwezi.

Nikuambie ukweli tu ujinga ule alifanya Magufuli kwenye ule uchaguzi ndio lilikuwa anguko lake. Kwa mara ya kwanza Tanzania inaingia kwenye kupiga kura kwa kuzimiwa internet, hata tulikuwa tunayasikia Uganda nikashangaa inatokea na hapa kwetu. Mara wagombea kuenguliwa na ujinga wote.
 
Mkuu JPM alishinda, Lissu alianguka tukubali hilo.
 
Basi hata JNIA ubadilishwe jina na wenyewe kama hakuna maana

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app

Kuna tofauti kubwa Sana kati ya JNIA na stendi ya Magufuli. Uwanja JNIA ulipewa Hilo jina baada ya Mwl. Nyerere kufariki ilikuwa Kama kumbukumbu na hapo awali uliitwa DIA. Kuhusu stendi ya Magufuli, stendi ilipewa jina Hilo Magufuli akiwa hai. So ni vitu viwili tofauti. Labda utafute mfano mwingine mzuri.
 
Mkuu JPM alishinda, Lissu alianguka tukubali hilo.

Kwa mazingira yetu anaweza kuwa alishinda ila alishinda kihalali?. Kumbuka Mwaka 2015 alipata kura asilimia 57% . Unadhani CCM na uroho wao wa madaraka wakaruhusu NEC itangaze hizo asilimia ilikuwa bahati mbaya?. Ina maana waliiba mpaka wakachoka, wakaishia kufuta uchaguzi Zanzibar kwa aibu.

Magufuli angeruhusu uchaguzi huru 2020 hata Mimi kile kinyongo nilichokiwa nacho kwake ningekipunguza. Ila ndio hivyo kiburi Cha uzima ni tatizo.
 
Sio rahisi hilo jambo kufanyika, kumbe wengi hata hamjui matukio ya Kisiasa kulingana na nyakati.

Ina maana hamjui yule Mzee ameacha wafuasi zaidi ya 10M plus Nchini? Zile ni Kura

Na CCM inajua kitendo cha kufanya huo upuuzi kunaweza kuwanyima kura 2024 na 2025.

Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na hii Propaganda.

Kama mnadhani masihara ajitokeze mtu tuweke 500k kila mmoja tufanye betting

CCM ilishakufa zamani. Na Kama wafuasi Magufuli amepata wafuasi wengi baada ya huyu mama kuingia madarakani na kupwaya. Rushwa, gharama za maisha zinatoa sababu za watu kuona Magufuli alikuwa Bora.
 
Basi hata JNIA ubadilishwe jina na wenyewe kama hakuna maana

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Kuweka majina ya viongozi ni desturi ya Dunia nzima, sioni ubaya kwa hilo. Nyerere alikataa sana vitu kuitwa majina yake, na vingi vimebatizwa jina hilo akiwa kastaafu uRais na vingine akiwa amekufa. Hata Mkapa ni hivyo hivyo alikataa akiwa hai.

Lakini kiongozi unapokuwa madarani unapokuwa na kiherehere cha kuyapa jina maeneo kama ambavyo Magufuli alifanya kwa rafiki zake kwenye ufisadi akina John Kijazi, Mfugale na Ndugai ndiyo haitakiwi. Naye akajipa stendi ya Mbezi Luis kwa kumuelekeza Selemani Jafo aweke jina lake. Hiyo siyo sawa
 
Mkuu usidanganye watu, wewe sema mikoa yenye wasukuma wengi!

Hata hao wasukuma ni nusu tu! Kawauliza wavuvi, wafugaji na wakulima wa pamba kilichowapata ndio utajua hujui!
Sio ndio hapo sasa, angekuwa anakubalika na wasukuma wengi hivyo asingepora uchaguzi ili ionekane anakubalika sana.
 
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy . Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.
Picha ile ni ya zamani bhana Jina alijabadilishwa kwanza yeye hakutaka ila walijipendekeza kwa hiyo hata wakilitoa haina shida ila ubaya wananchi wataendelea kuita Magufuli hilo jina limeshakaa
 
Kuweka majina ya viongozi ni desturi ya Dunia nzima, sioni ubaya kwa hilo. Nyerere alikataa sana vitu kuitwa majina yake, na vingi vimebatizwa jina hilo akiwa kastaafu uRais na vingine akiwa amekufa. Hata Mkapa ni hivyo hivyo alikataa akiwa hai.

Lakini kiongozi unapokuwa madarani unapokuwa na kiherehere cha kuyapa jina maeneo kama ambavyo Magufuli alifanya kwa rafiki zake kwenye ufisadi akina John Kijazi, Mfugale na Ndugai ndiyo haitakiwi. Naye akajipa stendi ya Mbezi Luis kwa kumuelekeza Selemani Jafo aweke jina lake. Hiyo siyo sawa
Sasa mkuu hapa umeongea nini na unakubali na kupinga nini? Magufuli hakulazimisha hilo jina bhana kila mtu anajua
 
Sio rahisi hilo jambo kufanyika, kumbe wengi hata hamjui matukio ya Kisiasa kulingana na nyakati.

Ina maana hamjui yule Mzee ameacha wafuasi zaidi ya 10M plus Nchini? Zile ni Kura

Na CCM inajua kitendo cha kufanya huo upuuzi kunaweza kuwanyima kura 2024 na 2025.

Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na hii Propaganda.

Kama mnadhani masihara ajitokeze mtu tuweke 500k kila mmoja tufanye betting
Ccm hawategemei kura kukaa madarakani, na udhibitisho ni pale dhalimu magu alipofanya siasa peke yake na chama lake la majizi, lakini ilipofika wakati wa uchaguzi na alichokiona kwenye kampeni zile ilibidi apore mchakato wa uchaguzi.
 
Sasa mkuu hapa umeongea nini na unakubali na kupinga nini? Magufuli hakulazimisha hilo jina bhana kila mtu anajua
Hakulazimisha wakati nyuma ya pazia alikuwa anaagiza, kisha akitokea hadharani anajifanya hataki. Kama alikuwa anaita nchi Tanzania ya Magufuli, Nini stand?
 
Back
Top Bottom