Naona umemshikia bwana kiranga bendera yake sasa na kuwa unalirudia swali hili mara nyingi sana na huyu bwana tulishamjibu ila tu kama unavojua huwa ana ubishani wa kitoto ule wa kizamani zamani.
Jawabu linakuja na maelezo marefu kama ifuatavyo.
Swali lako linasema KAMA MUNGU KAUMBA ULIMWENGU VIPI KUWE NA MAPUNGUFU NA MAJANGA MBALI MBALI?
NI hivi bwana
Behaviourist
Kwanza kabisa katika mjadala wowote ule unapojenga hoja basi unajenga hoja hiyo kwa kuiamini kabisa kwamba ni hoja,huwezi ukajenga hoja ambayo hata mwenyewe huiamini labda kwa kubainisha tu(nitafafanua)
Mfano ukisema kwamba Rais magufuli kasema Nchi haina pesa hivyo hawezi kuongeza mishahara,wewe au mimi nikijenga hoja kwamba kama Nchi haina pesa vipi kanunua Ndege kubwa kapata wapi pesa hizo?
Hapa hoja yako ni Ndege kununuliwa bila shaka utakuwa na ushahidi na imani juu ya hoja yako hiyo.huwezi kusema unajengea hoja ambayo hata mwenyewe huiamini huo utakuwa ni uzwazwa.
Sasa mfano mtu akuulize vipi unaamini kama ndege imenunuliwa wewe useme aaaah siamini kama Ndege yenyewe imenunuliwa.hii inakuja kiakili?
Labda kwa watu ambao hukimbizana na makalio yao wenyewe wanaweza kusema hivyo.
Tunarudi pale pale kwamba hoja unayoijenga lazima uiamini kwanza ndipo utaitegemea kama hoja.
Sasa tukirudi katika swali lako kuwa "KAMA MUNGU NDO MUUMBA VIPI KUWE NA MAPUNGUFU MBALI MBALI?"
Hapo swali lako lina sehemu tatu.
Kuna Mungu
uumbaji
Mapungufu.
Sasa hapa tukitizama swali lako tunaona kuwa UNAAMINI KWAMBA MUNGU HAWEZI KUUMBA KITU CHENYE MAPUNGUFU ...au uongo?
Ikiwa hauamini vipi unajenga hoja ambayo hata mwenyewe huiamini?
Kusema unaamini sitokuambia kama unakubali Mungu yupo usiogope sina usulubu huo....
Bali nataka nihoji tu kwamba IMANI YAKO YA KUAMINI MUNGU HAWEZI KUUMBA MAPUNGUFU UMEITOA KWA MUNGU MWENYEWE (vitabu)AU UMEITOA AKILINI MWA WATU?
kama umeitoa katika Vitabu vya Mungu basi UTUPE KAULI NYINGINE YA MUNGU IKIBAINISHA ANASEMA KWAMA KIFO,MATETEMEKO N.K NI KATIKA MADHAIFU HAYO.
kama UMETOA akilini kwa watu sio kwa vitabu vya Mungu VIPI ITAKUWA HOJA HIYO WAKATI HILO HAKULISEMA MWENYEWE MUNGU?
Kisha unaposeema MGONGANO manake ni kwepo kwa vitu vyenye asili moja vinavopingana
Mfano leo Magufuli aseme tanzania ni Nchi tajiri kisha baadae Aseme Tanzania ni Nchi masikini.
Huu ndiyo mgongano kwa sababu mmoja huyo huyo anatoa kauli zinazopingana.
Haiwezekani ukasema kuna mgongano kwa sababu kauli moja inasema Tanzania ni Nchi tajiri kisha kuna kauli ya pili ya asiyekuwa magufuli anasema tanzania Nchi masikini.hapa huwezi kusema magufuli anagongana kauli zake.kwa sababu lazipa papatikane vitu(kauli)viwili vyenye asili moja(magufuli)
Sasa unaposema kuna mgongano kuhusu Mungu una maana kauli ama uumbaji wa Mungu unapingana.
Tuambie huko kupingana kwake.