1. Engineering ya Mungu imefanyika kwa mahesabu ya interdependence kati ya creatures na nature.. Ndio maana hata ukitazama ecosystem unaona chain ilivyo kimkakati - au huo nao utauita udhaifu?.
Mungu angekuwepo, kungekuwa hakuna entropic increase in the world, global warming, pandemics, earthquakes, tsunamis, desertification visingekuwepo.
Mungu angekuwepo, ecosystem isingekuwa na food chain ya mwenye nguvu kumla asiye na nguvu, hiyo ni injustice kwa asiye na Mungu, inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aweke ecosystem isiyo na justice kwa asiye na nguvu?
2. Labda useme tu unahitaji uthibitisho gani. Mungu yupo kupitia ishara zake. Kwa mfano, tazama yale madhara yanayoshindikana tiba hospitalini lakini yanaponyeka kwa kutumia neno la Mungu.
Hospitali kuwepo ni ushahidi Mungu hayupo. Mungu angekuwepo, kungekuwa hakuna hospitali, kwa sababu kungekuwa hakuna ugonjwa.
Unamsifia Mungu kwa kutibu ugonjwa wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ugonjwa hauwezekani kuwepo?
Unamsifia mwizi kaiba mabilioni, unasema ni mtakatifu sana, eti kwa sababu karudisha mia aliyoiba (ambayo ataiiba tena).
Yale mabilioni ambayo hajarudisha vipi?Wwale mabilioni waliokufa vipi? Na huyo aliyepona hatakufa?
Huyo Mungu yupo au hadithi tu?
Hujawahi kushuhudia miracles zozote ambazo hata kisayansi ni ngumu kuthibitika? Mfano, hujawahi kuona Mtu anapandisha mashetani na kumudu kuongea kwa ufasaha lugha ambayo hana hata ujuzi nayo?
Miracle ni nini? Vitu vingi tusivyovielewa tunaviita miracles, maana yake hatuvielewi, hilo halithibitishi Mungu yupo.
Mababu zetu waliamini Wazungu ni miungu, kwa sababu wanatabiri jua kupatwa, wana gramophone zinatoa muziki bila mtu kupiga ala.
Wwaliona muujiza. Sasa hilo lilimaanisha kutabiri kupatwa kwa jua na gramophone kupiga muziki ni muujiza? Hayo yalithibitisha Mungu yupo?
Kama bado, Mungu akujaalie Siku ukutane na miracle yoyote maybe it will change your way of thinking mzee baba..
Thibitisha Mungu yupo kwanza.