Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa CCM amemtangaza Mhe. Pinda ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu kuwa mrithi wa Kinana. Wajumbe na wanachama sambamba na wananchi wameonekana kutopokea positive pendekezo hili au wameshtuka kwa kilichotokea. Je, walimtegemea nani?

Tukumbuke cheo hiki hakuna kugombania bali linapelekwa jina moja ambalo litapata kura za ndio na hawana. Lakini pia historia inaonyesha kila pendekezo la Mwenyekiti huwa linapita kwa asilimia 90+ hivyo ni wazi Pinda ndiye makamu mwenyekiti ajaye wa CCM Bara.
Ni Steven Wasira, acha upotoshaji.
 
Msikilize mzee pinda anakupa neno lako 😂
 
Chama Cha Mapinduzi kimempendekeza Ndugu Stephen Masatu Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la mwanasiasa mkongwe nchini
Stephen Wassira kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wa Taifa unaofanyika Jijini Dodoma, kwa ajili ya kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyemiti wa CCM Bara.

Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Wasira ni miongoni mwa wana CCM waliowahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ni mmoja wa viongozi wakongwe wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM, ambapo tangu mwaka 2007 amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011.

Rekodi yake ya uongozi na uchapakazi wake, imemuweka kuwa katika nafasi nzuri ya kuonekana kama nguzo muhimu ndani ya CCM.

View attachment 3205242
Hapa nami namuunga mkono mama Samia. Steven Wasira hana makundi.
 
Wajumbe pigeni kura za hapana. Mzee wa watu apumzike tafuteni damu changa nyenye mawazo chanya, vinginevyo chama kinazidi kudhoofu mtasaisiwa hadi lini wakati wa chaguzi ndugu zangu. Kwamba unawatakia heri sisiem?
 
Back
Top Bottom