Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kumbe ilikua awe yeye!
Ndio maana amesimamishwa aweke sawa, hata sauti yake inaonyesha hana furaha sana na uteuzi huu.
 
Pinda ni mtu wa katavi vijijini. Tangu ameingia madarakani hakufanya maendeleo yoyote. Jamii yao ni watu wasiopenda maendeleo hata kijiji anachotoka watu wanaomiliki biashara kilimo na ufugaji sio wazawa. Miundo mbinu ni mibovu lakini hakuna anaejali. Inasemekana ni jamii ya wale wazee wa sumbawanga wanaoogopwa. Kupewa umakamu mwenyekiti kunaweza kuwa ni sababu ya kulinda kiti cha mwenyekiti kama kuna watu wanakiwania akiwepo pinda hawatoboi.
 
kwa nafasi za kuteuliwa tena zisizo hitaji utaalamu vijana kutoboa ni ngumu

kdg zile za kuhitaji utaalamu wanaweza tokeza kichwa ila hizi za kusifu na kuabudu wanapena wenyewe
 
Stephen Wassira Vs Tundu Lissu, ngoma inogile, ni vibe, amshaamsha za kisiasa mwanzo mwisho. kabla ya uchaguzi mkuu waandaliwe kipindi studioni ijulikane nanh gwiji wa siasa nchini
 
Duuuu kuna shida mahali aseee Wasira? Wanataka afie kwenye kwenye chama? Daaaa
 
Chama Cha Mapinduzi kimempendekeza Ndugu Stephen Masatu Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la mwanasiasa mkongwe nchini
Stephen Wassira kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wa Taifa unaofanyika Jijini Dodoma, kwa ajili ya kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyemiti wa CCM Bara.

Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Wasira ni miongoni mwa wana CCM waliowahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ni mmoja wa viongozi wakongwe wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM, ambapo tangu mwaka 2007 amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011.

Rekodi yake ya uongozi na uchapakazi wake, imemuweka kuwa katika nafasi nzuri ya kuonekana kama nguzo muhimu ndani ya CCM.

View attachment 3205242
Safi sio kama wale wengine walikuwa na mipango Yao ya Siri
 
Back
Top Bottom