Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Pre GE2025 Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chama Cha Mapinduzi kimempendekeza Ndugu Stephen Masatu Wassira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasilisha jina la mwanasiasa mkongwe nchini
Stephen Wassira kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM wa Taifa unaofanyika Jijini Dodoma, kwa ajili ya kupigiwa kura kuwa Makamu Mwenyemiti wa CCM Bara.

Wasira aliyezaliwa Julai Mosi, 1945 wilayani Bunda Mkoa wa Mara, kwa zaidi ya nusu karne amejijengea heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii.

Wasira ni miongoni mwa wana CCM waliowahi kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ni mmoja wa viongozi wakongwe wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM, ambapo tangu mwaka 2007 amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2011.

Rekodi yake ya uongozi na uchapakazi wake, imemuweka kuwa katika nafasi nzuri ya kuonekana kama nguzo muhimu ndani ya CCM.

View attachment 3205242
Cheki Kinana anavyotia huruma 😂😂😂👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/DE9l0j5NvI0/?igsh=MWdibWc4bGdyOXBtNw==
 
Kumbe ilikua awe yeye!
Ndio maana amesimamishwa aweke sawa, hata sauti yake inaonyesha hana furaha sana na uteuzi huu.
Mtu amekuwa waziri mkuu, ana pensheni ya uwaziri mkuu, umri umeenda anataka nini tena?

Kweli madaraka ni madawa ya kulevya.
 
Leteni Picture Ya Wasira Aliyofinga Vifungo Vya Koti Hovyo Akiwa Waziri Enzi Za JK
 
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, Samia. Yupooooooo,😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
Vijana bado hamuaminiki kushika nafasi za juu za chama. Jifunzeni siri hizi kwa wazee kama Wassira. Achaneni na show off.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
CCM kwa nini mnaogopa vijana kuwapa madaraka ya kukiongoza chama. Huyu mzee wa miaka 80 na ushee kweli. Yaani hata kama si kazi ya matofali lakini....
Wasira amepewa mamlaka akiwa na miaka 25.

Salim Ahmed Salim amepewa mamlaka makubwa akiwa na umeri wa miaka 18.
Nyerere amekuwa rais akiwa na miaka 39.

Sasa kwann wanaogopa kumkabidhi umakamu mwenyekiti wa chama kijana ??

Kwa uteuzi huu hata Mbowe kapata uchochoro wa kutokea
 
Mwenyekiti wa CCM amemtangaza Mhe. Pinda ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu kuwa mrithi wa Kinana. Wajumbe na wanachama sambamba na wananchi wameonekana kutopokea positive pendekezo hili au wameshtuka kwa kilichotokea. Je, walimtegemea nani?

Tukumbuke cheo hiki hakuna kugombania bali linapelekwa jina moja ambalo litapata kura za ndio na hawana. Lakini pia historia inaonyesha kila pendekezo la Mwenyekiti huwa linapita kwa asilimia 90+ hivyo ni wazi Pinda ndiye makamu mwenyekiti ajaye wa CCM Bara.
mafunzo ya uzushi umeyapatia bavicha au bazecha gentleman 🐒
 
Mwenyekiti wa CCM amemtangaza Mhe. Pinda ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu kuwa mrithi wa Kinana. Wajumbe na wanachama sambamba na wananchi wameonekana kutopokea positive pendekezo hili au wameshtuka kwa kilichotokea. Je, walimtegemea nani?

Tukumbuke cheo hiki hakuna kugombania bali linapelekwa jina moja ambalo litapata kura za ndio na hawana. Lakini pia historia inaonyesha kila pendekezo la Mwenyekiti huwa linapita kwa asilimia 90+ hivyo ni wazi Pinda ndiye makamu mwenyekiti ajaye wa CCM Bara.
Mbona huku wamesema Wasira

Leteni Picture Ya Wasira Aliyofinga Vifungo Vya Koti Hovyo Akiwa Waziri Enzi Za JK
1737194803510.png
 
makongoro nyerere akuje aone jamaa awamu ya sita yumo tena

mganga wa wasira anajua sana
 
Mwenyekiti wa CCM amemtangaza Mhe. Pinda ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu kuwa mrithi wa Kinana. Wajumbe na wanachama sambamba na wananchi wameonekana kutopokea positive pendekezo hili au wameshtuka kwa kilichotokea. Je, walimtegemea nani?

Tukumbuke cheo hiki hakuna kugombania bali linapelekwa jina moja ambalo litapata kura za ndio na hawana. Lakini pia historia inaonyesha kila pendekezo la Mwenyekiti huwa linapita kwa asilimia 90+ hivyo ni wazi Pinda ndiye makamu mwenyekiti ajaye wa CCM Bara.
Wazee wa hekima wamerudi mahala pake
 
Ila tuache utani jamani CCM ina hazina kubwa ya viongozi
 
Huyu mzee ana miaka 80 jamani angewachwa apumzike!!
 
Back
Top Bottom