Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Biblia ukisoma nusu nusu hutoelewa milele hasa neno lenye uchaji wa Mungu halieleweki kwa wote. Mfano kuna watu wa itelejinsia humu huwasiliana kwa maandishi haya na wengi wetu hatujui wala kuelewa chochote, note that.
Kama sio mcha Mungu sahau kuhusu kuelewa Neno LA Mungu.
 
Hujathibitisha nililo kuuliza.

Nalusaidia kwa swali lako rahisi sana. Naizungumzia Qur'aan.

Mtume alikuwa ni katika Waarabu,na ndiyo maana Qur'aan imetermshwa kwa lugha ya Kiarabu.

Kisha ikawafikia wasio kuwa Waarabu sababu ni ujumbe kwa walimwengu wote.

Mola akajaalia ukijifunza jambo unalijua hata kama si la lugha yako. Watu wakafundishwa lugha ya Kiarabu na wakaelewa. Leo hii ukienda bara la arabu au ukisoma historia ya wajuzi wa kiarabu kiasili si Waarabu.

Sasa usiwe mjinga kukataa jambo usilo kuwa na elimu nalo.

Hakuna aliye zaliwa anajua,hata wewe bila kufindishwa leo hii usingejua kusoma wala kuandika,yaani ungebweteka.

Sasa nataka uthibitishe ya kuwa Qur'aan imeandikwa yaani imetungwa ba Mwanadamu.
 
Kila andiko unalosoma nadhani unatakiwa ufahamu nani anaambiwa. Hapa Yeremia ndio aliambiwa alijulikana tangu tumboni sasa we mbona unajiweka wewe? Au kwa imani? Soma kwa roho na akili utaelewa. Ukisikiliza tafsiri ni most likely usipate kitu
 
Hapa ndo wale akina naijua vizuri biblia watakwambia Mungu ajua ya sirini [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwahiyo hawakutajwa ili baadae tuje kujiuliza maswali ya hivi tubaki na sintofahamu au wamaanisha Mungu hakutaka tujur vyema kazi yake ya uumbaji??[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nimependa hapo kwa Adam na Eva wanatenda dhambi mungu akakasirika!
Hapo hapo unaambiwa ye ajua mwanzo na mwisho[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Kazi ngumu hii jaman
 
Quraan ni hekaya za Muhammad, sababu mara zote alipotenda kosa, ilishushwa aya kujustify makosa yake na wala sio kurekebisha au kumtaka atubu kama ambavyo ilifanyika kwa mitume na manabii wengine.
 
Quraan ni hekaya za Muhammad, sababu mara zote alipotenda kosa, ilishushwa aya kujustify makosa yake na wala sio kurekebisha au kumtaka atubu kama ambavyo ilifanyika kwa mitume na manabii wengine.
Thibitisha.

Kwahiyo hekaya ina sifa hii ? Amekwambia nani hizi habari ?

Hapa chini nakuwekea aya zinazo mkosoa Mtume wa Allah.

1. Alikunja kipaji na akageuka,

2. Kwa sababu alimjia kipofu!

3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?

4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?

5. Ama ajionaye hana haja,

6. Wewe ndio unamshughulikia?

7. . Na si juu yako kama hakutakasika.

8. Ama anaye kujia kwa juhudi

9. Naye anaogopa,

10. Ndio wewe unampuuza?

11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.

12. . Basi anaye penda akumbuke. (Abbasa : 1-12)
 
Uko sahihi kabisa ila, sometimes watu wanajadili vitu kwa ushabiki so tunahaki kutazama tu
 
Lakini hapo kwa mtiririko ni kuwa Adam alizaa wana na mabinti baadae maana unaona hapo ipo chapter 5 wakati Kaini kuogopa imetokea chapter 4.

Mtirirko haupo hapo.
 
Ushahidi wa nini na nitaupata wapi mimi sasa?
Naomba uniwekee story mbili tu kisha uthibitishe ya kuwa hizo ni ngano ? Yaani uweke na ushahidi.
 
Binadamu ana ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho.

Katika ulimwengu wa mwili formula sinajulikana tu zipo waZi ila ulimwengu wa roho sio mrahisi kuelezea hivyo basi kwenye kila jamii watu walioamua kutaka kujua nini kinaendelea kwenye ulimwengu wa roho walikuwa wakiandika mambo mazuri na mabaya waliojifunza katika ulimwengu wa roho.Lengo ni kuwasaidia watu kuuelewa ulimwengu wa roho.Jamii za wenzetu waliandika vitabu na kuchora michoro yenye maana mbali mbali.

Hivyo vitabu ndo tunaviita vya dini au uchawi kulingana na mwandishi alijifunza nini na alikusudia kufundisha nini ktk ulimwengu huo wa roho

Lugha inayozungumzia mle ni mafumbo na baadhi ya mambo lazima uingie kwenye ulimwengu wa roho ndo utayaelewa..

Shida inakuja viongozi wa dini wengi wanatafsiri mambo ya ulimwengu wa roho kama ni mambo ya ulimwengu wa nyama.

Kuna vitu havieleweki katika ulimwengu huu lkn katika ulimwengu wa roho vina maana kubwa.

Vitu km mchawi anavyopaa usiku,chumaulete,kumuua baba/mama ako hlf unaanza kuwa tajiri ni vitu ambavyo Havieleweki kabisaaa katika ulimwengu wetu lakini vipo na vinafanya kazi kweli .
Vitabu vya Dini viliamua kuelezea kidogo sana ulimwengu wa roho upande wa giza na vikawekeza kuelezea sana ulimwengu wa roho upande wa nuru.Nadhani ziliogopa kufunza watu yaliyomo ulimwengu wa roho upande wa giza

Swali ni je vitu tunavyofundishwa kwenye biblia na kuruani.Waandishi ambao tuseme wamefunuliwa na Mungu.Ujumbe wanaotupa ndo ulikusudiwa tujifunze huo au tafsiri yake imepotea.

Je usiue ya kwenye biblia ina maana gani?nisiue nini?kwasababu gani?Maana watu wa Mungu walishiriki vita nyingi!!!tunaua ili tule kila siku!!

Ufalme wa Mungu upo ndani yako,kivip?nini maana yake sahihi
 
Ushahidi wa nini na nitaupata wapi mimi sasa?
Ina maana umeropokwa tu ? Kama hivyo ndivyo wewe ni muongo au una matatizo ya akili,inakuwaje anaweka mambo usiyo yajua ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…