Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Story gani katika kitabu cha dini yako unafikiri ni hadithi ya ngano tu?

Tumepigwa mchana kweupeee
Mkuu tumepigwa Sana tu Kuna ule mstari Yesu alitamka kuwa mtu akiwa anaimani ndogo hata Kama punje ya haradani(hiyo punje sidhani Kama nimeipatia kuiandika) Basi kwa imani ndogo kiasi hicho tu mtu anaweza kuuamrisha mlima ung'oke na ukajitupe baharini!! Sasa kwa hii billions of people hakuna mwenye hiyo imani..?? Wagonjwa badala waende wakapate uponyaji lkn wengi wao utawakuta mahospitalini..😀
 
Uumbaji ni ngano Bora iliyochanganywa na tangawizi. Try to compare Genesis and Darwinism.
 
Wataalam eti wanasema...inawezekana Adam alipata watoto wengine zaidi ya Kaini, abeli na Seth ambao watakuwa wa kike. Means kaini alizaa na dada yake.
Zamani wanawake walikuwa hawatambuliki hata kuandikwa kwenye vitabu
Nisaidie kuwauliza hao wataalam wako wanifafanulie ile stori ya safina ya NUHU.

Maana aliweka wanyama wa kila aina... vua likapiga la kufa mtu... Hivi Simba walikuwa wanamwangalia swala bila kuwala? Jaribu kupata picha namna NUHU alivyokuwa anamshawishi Chui aingie kwenye safina... au alivyombembeleza nyoka koboko aingine safinani....

Maana kama lile vua liliijaza dunia mpaka miti kuzama, niambie huyu mwamba alitumia mbinu gani kumshawishi mwewe na mkewe kuingia kwenye safina? Siafu, nzige, sisimizi na panzi hiyo utauliza siku nyingine maana bado nafanyia kazi uingiaji wa nyati, tembo, kiboko na kangaroo...
 
Wataalam ni noma, inawezekana Simba wa zamani hakuwa mkali kama sasa hivi. Swali lingine kwa wataalam...Je Kati ya hao wanyama Kitimoto alikuwepo? Na Kama alikuwepo iliwezekana vipi Mungu aruhusu mnyama haramu aingie? Kwanza kwanini alimuumba huyu kiumbe?? Mitego tu
 
Mi sehemu napokikubali ni pale Masiha alipogeuza divai kuwa damu yake... sijui kwanini hakutumia maji... hii imetuhalalishia wapiga gambe kushinda vita ya mdahalo wa pombe sio dhambi...
 
Binafsi kwenye kitabu cha dini yangu ya Kikristo, yaani BIBLIA TAKATIFU, sijawahi wala sitarajii kusikia Ngano humo ndani. Yote yaliyomo humo ni kweli tupu. Ni mafundisho ya kweli na ya UHALISIA.
Ile ya yakobo kuwa na wake watatu na kutandika wadogo wa wake zake wote watatu, pia na suleiman kuzaa na vijakaza n.k wake buku (1,000)
 
Quran tu ndo kitabu pekee kinachoeleweka na hakina shaka kabisa.
Mtume alichumbia katoto ka miaka nane na hapo bado akaowa kikongwe na hiyo ikapitishwa kama suna... Hapo napo ni chai kwa jamii zetu na tamaduni zetu
 
Kwamba Mungu aliumba dunia na kila kilichomo (sawa) kisha akaumba mwanaume na kuumba mwanamke kwa kumtoa ubavu mmoja mwanaume (sawa).

Kisha hao wawili (Adam na Eva/Hawa) wakazaa watoto wawili (Kaini na Abeli) - (sawa).

Kisha Abeli akawa mfugaji na Kaini akawa mkulima (sawa). Lakini Mungu alipendezwa zaidi na sadaka za Abeli kuliko za Kaini (sawa). Kaini akamuua kaka yake kwa wivu (sawa).

Mungu akampa adhabu Kaini kwa kumfukuza bustanini awe anatanga tanga huku na huko duniani (sawa).

Kaini akamwambia Mungu kuwa akitangatanga watu atakaokutana nao watamuua (shida inaanza kuja hapa). Mungu akamwekea alama usoni ili walimwengu wasimuue (shida inaendelea). Kaini akaenda huko nchi ya Nodi mashariki mwa Eden.

Kisha kaini akalala na mkewe akamzaa mtoto aitwae Henoki. (Sio sawa).

Reference: Soma kitabu cha Mwanzo 4:1-17.

Hii story haija balance kabisa hasa hapo mwishoni. Kama Mungu aliumba Adam na Hawa na wakazaa watoto wawili tu ina maana duniani palikuwa na watu wanne tu. Je hao watu aliokuwa akiwaogopa Kaini ni akina nani? Je huyo mwanamke alielala na Kaini na kuzaa nae mtoto alitoka wapi?

Wataalamu hebu naomba mtusaidie hapa.
Ukielewa tu kuwa biblia haaikuandikwa katika mtiririko(yaani chronological order)hiki kitu kidogo hakitakusumbua kukielewa
 
Mi sehemu napokikubali ni pale Masiha alipogeuza divai kuwa damu yake... sijui kwanini hakutumia maji... hii imetuhalalishia wapiga gambe kushinda vita ya mdahalo wa pombe sio dhambi...
Dah
 
Story ya Mussa kutumia miaka 40 kutoka Misri hadi Israel ni uongo mtupu, hata kama zamani hawakua na Ndege au Magari lakini pale sio mbali ki hivyo.
Mh ila kumbuka kabla ya hiyo miaka walifanya uchunguzi mara mbili na kuona kwamba haiwezekani kwenda moja kwa moja
 
😀😀😀😀😀

Aisee
Siyo kweli kuwa Mungu alimuua mwanae wa pekee, Yesu Kristo! This is a misquote or a misunderstanding ya hilo andiko. Yesu Kristo "aliuwawa" na Wayahudi SIYO MUNGU. Bali Mungu ALIMTOA MWANAWE PEKEE ili atuokoe kutoka dhambini na hatimaye kutupatanisha na Mungu wetu baada ya lile anguko la binadamu kule Bustani ya Eden kutokana na fitina za Ibilisi. Hiyo ndiyo tafsiri sahihi ya hilo andiko.
 
Et dini yako😄😄 kama ww ni mzungu ni sawa. Lakini kama ww ni wa hapahapa basi usijifanye unaijua sana kuliko walioianzisha bwa shee. Hujui chochote zaidi ya mapokeo
Sawa hata kama nimeipokea basi nimeisha i customize na kuwa yangu na zaidi ya yote, naiamini kuwa ni IMANI yangu sahihi na kuwa Yesu Kristo aliye HAI nai Mwokozi wangu. Vipi hapo UTAKEREKA ZAIDI au vipi?!
 
Kuna sura na mstari kwenye kitabu cha yohana mtakatifu, unasema kama biblia ingeandika kila kitu basi isingetosha wala kujaa, hivo naamini pia kuna watu waliokuwepo ambao hawakuongelewa ktk kipengele hicho cha Kain, huenda ikawa pia ni wale jamii ya wanefili ambao kwenye mwanzo wanatajwa tu lkn hawakuonglewa kwa undani sana
Kama biblia ni product ya mungu mwenye nguvu ya kufanya chochote basi isingeshindikana kila kitu kuandikwa na kueleweka. Kushindikana kuandikwa kila kitu kwenye biblia ni ushahidi tosha iliandikwa na wanadamu ambao uwezo wao wa kiundashi upo limited.
 
Back
Top Bottom