Nisaidie kuwauliza hao wataalam wako wanifafanulie ile stori ya safina ya NUHU.
Maana aliweka wanyama wa kila aina... vua likapiga la kufa mtu... Hivi Simba walikuwa wanamwangalia swala bila kuwala? Jaribu kupata picha namna NUHU alivyokuwa anamshawishi Chui aingie kwenye safina... au alivyombembeleza nyoka koboko aingine safinani....
Maana kama lile vua liliijaza dunia mpaka miti kuzama, niambie huyu mwamba alitumia mbinu gani kumshawishi mwewe na mkewe kuingia kwenye safina? Siafu, nzige, sisimizi na panzi hiyo utauliza siku nyingine maana bado nafanyia kazi uingiaji wa nyati, tembo, kiboko na kangaroo...