Uchaguzi 2020 Suala la ajira ndio litamuondoa Rais Magufuli madarakani hasa vijana ambao ndio wengi

Nani kakudangaya kuwa box la kura ndio litakaloamua?
 
Wagombea wengi wanasema wataondoa tatizo la ajira,lkn hawaelezi watafanyaje fanyaje kuondoa tatizo la ajira na je hilo tatizo wataliondoa kwa mda gani,manake kila mwaka kuna vijana wapya wanaingia mtaani.

Mimi huwa naona wote wanafanya siasa ambazo zimejaa maneno na kukosa uhalisia.
 
Ni mtaji mkubwa sana watu wasikuwa na ajira since 2015. Lakini kikubwa ni watumishi wanaokatwa na bodi ya mikopo kiwango kikubwa tofauti na mkataba uluvyokuwa awali.

Malawi wametuonyesha mfano ambao tutaiga. Rais magufuli lazima aondoke hata bila vyombo vya dola kukubali.
 
Bara bara amejenga ipi?
 
Sitawahi kupiga kura ktk maisha yangu yoteeeeh.
Aseee tupo pamoja katika hili na haitakaa itokee maisha mwangu...watu wa nchi za mwenzetu yaani kura kwao ndio tiketi ya kumchagua kiongozi bora mwenye kuwatumikia wananchi wake lakini sio hapa nchini mara box ya kura feki yanaletwa vituo kupitia polis mara mabox yale ya kura yanaibiwa,huku wasimamizi wamekosa viapo,vurugu mtindo mmoja ya nn nipige kura...
 
Hayati Mwalimu Nyerere alitufundisha:
1. MAHITAJI MUHIMU YA BINADAMU.
--Chakula
--Mavazi
--Mahala pa kulala.
2. MAADUI ZETU.
---Ujinga
---Maradhi
---Umaskini
Ili uweze kupata mahitaji yako muhimu ni lazima uwashinde maadui hawa watatu.
Pia alisema ili uweze kumsaidia maskini , somesha MTOTO wake , tena mpe elimu nzuri.
Wakati Mwalimu Nyerere anayatekeleza haya, aliyatekeleza kwa tija kubwa.
Yule aliyempa elimu ya msingi alihakikisha anakuwa na shughuli ya kufanya au ajira.
Hakika wale waliomaliza shule za Sekondari walipangiwa kazi au kuendelea na masomo ya juu mara baada ya matokeo ya mitihani yao.
Wale waliomaliza elimu za juu, kati na kawaida ajira ziliwafuata wakati bado wako chuoni.
Kumsomesha mtu bila kuwa na malengo mengine naye ni sawa na poor resource management au uwekezaji usio faa.
Pesa nyingi zinazotumika kuwasomesha vijana wetu bila kuwapa elimu nzuri zingetumika katika kuanzisha viwanda vidogo vodogo na kulima kilimo cha kisasa. Wale wachache wanaosomeshwa na kupewa elimu nzuri wawe na uhakika wa ajira
Unamsomesha MTOTO kwa pesa nyingi na baada ya hapo anarudi kuwa mzigo kwa wazazi wake.
Mtoto aliyesoma chuo kikuu huwezi kumwambia tena ashike jembe la mkono na kulima masaa nane.
Huwezi ukamwambia akachunge ng'ombe.
Tufike mahala tujaribu kuwekeza kwenye elimu yenye tija kwa manufaa mapana ya Taifa,
 
Vijana wote inatakiwa tuunde forum ya kuhamasishana watu tuko mtaani na hatueleweki kwa sababu ya MTU mmoja hii ni nchi yetusote,piga chini jiwe
 
Bila kwanza kupiga chini sisiemu hizo zitabakia ndoto za alinacha
 
Hatuta mpigia kura Ila labda waibe tu. Mana haiwezekani engineer , mwalimu , Daktari yani five years tunachoma mahindi kitaa na ajira za temple nazo tunafukuzwa pamoja na kuwa na kubachelor.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…