Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Mbona unajichanganya? Utawapaje malengo na indicators kama mkataba ulioingia nao haukupi haki ya kufanya hivyo? Hilo ni mojawapo ya mapungufu ambayo hao unaosema wamejaa chuki wanayapigia kelele! Kwa hiyo tuseme na wewe umejaa ujinga na udini kwa sababu umeona upungufu huo?Inafahamika kuwa bandari zetu zinatoa huduma hafifu sana kwa wateja wake wanaozitegemea kwa huduma.
Inafahamika kuwa bandari zetu hazitoi mapato yanayokusudiwa kwa taifa kwasababu mbalimbali zikiwemo zile za:
1. Ukosefu wa utaalam wa kuendesha bandari.
2. Ukosefu wa vifaa vya vya kisiasa vya kuhudumia bandari.
3. Usimamizi mbovu wa bandari.
4. Upigaji mkubwa bandarini.
5. Uwezo wa meli kubwa na nyingi kutia nanga.
6. Wizi mkubwa
Bandari zetu zinahudumia nchi nyingi zinazotuzunguuka ambazo hazina bandari tangu wakati wa ukoloni hadi Leo hii. Huduma ni mbovu sana tangu enzi hizo lakini hakuna mtu aliyewahi kuandamana kupinga huduma mbovu zinazotolewa hata pale wateja wa bandari zetu wanapolalamikia huduma mbovu na wizi hadi kutishia kutuhama. Ubovu huu ulikuwepo kwenye awamu zote za uongozi.
Nikizotizama sura na majina ya wanaotaka kuandamana kupinga bandari isikodishwe kwa DP World kampuni kutoka Dubai Wana harufu ya wale waliokuwa wakinufaika na ulegelege wa usimamizi wa bandari, wangetaka status quo bandarini pale na ni wale wale wanaopinga kila kitu Cha uarabuni. Yaani kule uarabuni hakuna zuri lolote zaidi ya dini zao.
Hivi ni kweli tatizo la mkataba ni kukosekana ukomo wa muda TU? Mbona hata kwenye mkataba wa ndoa hakuna muda lakini wanandoa wanaachana na kutengana pia? Je, kama ukomo utawekwa mkataba utakuwa halali?
Ujinga kama huu ndio unawafanya watawala kuwa madikteta hata kama hawataki kuwa hivyo kwa watu wake. Yaani mtu Yuko radhi hali iwe hivyo hivyo kwa maslahi yake na kundi lake TU.
Wako watu wanaopinga mkataba kwa sababu za kweli, wengine ujinga TU, wengine kwa wivu wa awamu ya 6 kufanikisha, wengine kwa maslahi yao TU na wengine kwasababu za kidini TU.
Hao tunaowapa bandari yetu lazima tuwape malengo na indicators ili kufanya kile tunachokusudia kutoka kwao ni nini Cha kufanya kama malengo yanakwenda kinyume na expectations, Lakini sio kupinga uwekezaji huu.
Amandla...