Suala la bandari lina harufu ya chuki

Suala la bandari lina harufu ya chuki

Hayo manufaa yamefungamanishwa kwenye kifungu gan cha mkataba?

Yaani kuna pahala kwenye mkataba kumewekwa hizo targets? Na hatua za kuchukuliwa ikiwa hawajameet hizo targets?

HALAFU KWANINI BANDARI ZOTE???

PIA, KWANINI TUSIPATE HAYO PANDE ZOTE ZA MUUNGANO???
Maswali mazuri haya.
Hill ni doa kubwa sana kwa serikari ya awamu hii.
Na nguvu inayotumika kulitetea inazidisha wasiwasi zaidi.
 
Usichanganye sasa na kuwa mpole. Kwanza jielemishe kwani ports zimewekwa kwa ujumla wake. Ni wazi kwamba sio kila Bandari ataenda kuweka huo uwekezaji, no. Ports integration ndio itabainisha Bandari ili na ipi inahitajika mfumo wa uendeshaji wa kisasa.

Zanzibar yenye watu milioni moja ndio ukalinganishe Tanzania Bara+7 countries ambayo inakuwa uhakika wawatu takribani milioni 400?
Aisee kila nikirudia kusoma hiki ulichoandika nazidi kukuhurumia na kulihurumia taifa langu, hivi brother una percent kwenye hili suala? hivi kweli ndo umeona kabisa kwa akili zako timamu ushabikie hili suala au umeruhusu kushikiwa akili?

Yaani mfano bandari ni yako utaitoa kwa namna hii? Au unaamua tu liwalo na liwe kwa sababu ni ya wengi. Yatakurudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafahamika kuwa bandari zetu zinatoa huduma hafifu sana kwa wateja wake wanaozitegemea kwa huduma.

Inafahamika kuwa bandari zetu hazitoi mapato yanayokusudiwa kwa taifa kwasababu mbalimbali zikiwemo zile za:

1. Ukosefu wa utaalam wa kuendesha bandari.

2. Ukosefu wa vifaa vya vya kisiasa vya kuhudumia bandari.

3. Usimamizi mbovu wa bandari.

4. Upigaji mkubwa bandarini.

5. Uwezo wa meli kubwa na nyingi kutia nanga.

6. Wizi mkubwa

Bandari zetu zinahudumia nchi nyingi zinazotuzunguuka ambazo hazina bandari tangu wakati wa ukoloni hadi Leo hii. Huduma ni mbovu sana tangu enzi hizo lakini hakuna mtu aliyewahi kuandamana kupinga huduma mbovu zinazotolewa hata pale wateja wa bandari zetu wanapolalamikia huduma mbovu na wizi hadi kutishia kutuhama. Ubovu huu ulikuwepo kwenye awamu zote za uongozi.

Nikizotizama sura na majina ya wanaotaka kuandamana kupinga bandari isikodishwe kwa DP World kampuni kutoka Dubai Wana harufu ya wale waliokuwa wakinufaika na ulegelege wa usimamizi wa bandari, wangetaka status quo bandarini pale na ni wale wale wanaopinga kila kitu Cha uarabuni. Yaani kule uarabuni hakuna zuri lolote zaidi ya dini zao.

Hivi ni kweli tatizo la mkataba ni kukosekana ukomo wa muda TU? Mbona hata kwenye mkataba wa ndoa hakuna muda lakini wanandoa wanaachana na kutengana pia? Je, kama ukomo utawekwa mkataba utakuwa halali?

Ujinga kama huu ndio unawafanya watawala kuwa madikteta hata kama hawataki kuwa hivyo kwa watu wake. Yaani mtu Yuko radhi hali iwe hivyo hivyo kwa maslahi yake na kundi lake TU.

Wako watu wanaopinga mkataba kwa sababu za kweli, wengine ujinga TU, wengine kwa wivu wa awamu ya 6 kufanikisha, wengine kwa maslahi yao TU na wengine kwasababu za kidini TU.

Hao tunaowapa bandari yetu lazima tuwape malengo na indicators ili kufanya kile tunachokusudia kutoka kwao ni nini Cha kufanya kama malengo yanakwenda kinyume na expectations, Lakini sio kupinga uwekezaji huu.
Una uhakika na kwamba unacho kinena?
 
Manufaa ni ufasini na mapato wa bandari kuliko ilivyo Sasa. Sasa hivi wateja wetu wanalalamika kila wakati kuwa mizigogo Yao inachelewa na inaibiwa bandarini lakini hatuna Cha kufanya. Sasa Mama Samia amekuja na kitu Cha kufanya watu tuache kulalama prematurely.
Wako loliondo zaidi ya kuiba wanyama na kupeleka kwako ni nn tunapata?
 
hivi kweli ndo umeona kabisa kwa akili zako timamu ushabikie hili suala au umeruhusu kushikiwa akili?
Sishabikii ila nawashangaa nyie hamuelewi wapi lakini? Mbona hivyo vifungu mnavyopiga navyo kelele havina shida hizo mnaopayuka nazo. Believe me, issue ya Bandari kuna watu wanawaingiza king kwa interest zao. Mimi siamini kuwa watu kama akina Tundu Lissu hawajui kuwa issue sio tense kama inavyojadiliwa ila wao wana agenda zao na wengine wanataka kum frustrate Samia.

Kimsingi mimi nakuonea huruma wewe kwanini umekuwa miongoni mwa kundi la wajinga wengi wanaotishwa na mkataba.
 
Acheni kampeni hizi hazitawasaidia karekebishane mkataba uwe wa maslahi kwa taifa basi
Warekebishe au wasirekebishe mkataba hauna shida za kiiivyo badala yake Serikali iweke nguvu kwenye mikataba ya utekelezaji tu basi ambayo kwangu mimi naona ndio muhimu zaidi. Tunawaambia Zanzibar wana mfumo wao wa kuendesha Bandari yao. Bandari ni suala la Muungano kwasababu, Bandari ni mpaka hivyo kiulinzi na usalama lazima liwe suala la Muungano.

Tafuta mkataba uusome hauna shida za hivyo kama wanavyopiga kelele zaidi ya kutafuta political milage.
 
Kwani Zanzibar hapana wakazi ambao watapokea mizigo kupitia bandari? Yaani bandari ya ziwa Manyara iwe na faidia afu ya Zanzibar isiwe na faida?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi nyie mnadhani jambo la kuandika na kusaini mkataba ni la usiku mmoja? Umewahi kuwa negotiator wa mambo ya Tarde and Investment? Kuna baadhi ya articles mle huwezi kuzielewa kama wewe si negotiator and implementer.
 
Warekebishe au wasirekebishe mkataba hauna shida za kiiivyo badala yake Serikali iweke nguvu kwenye mikataba ya utekelezaji tu basi ambayo kwangu mimi naona ndio muhimu zaidi. Tunawaambia Zanzibar wana mfumo wao wa kuendesha Bandari yao. Bandari ni suala la Muungano kwasababu, Bandari ni mpaka hivyo kiulinzi na usalama lazima liwe suala la Muungano.

Tafuta mkataba uusome hauna shida za hivyo kama wanavyopiga kelele zaidi ya kutafuta political milage.
Mkataba nimeusoma wote mkuu, siwezi kusign mkataba ule, aliyeusugn namshangaa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tatizo gan kuuweka wazi mkataba? kwann unaweka blanket la all opportunities ? kwani utajuaje kama kutatokea fursa upande Zanzibar siku za baadaye? Acheni kutufanya wajinga. CCM itaondolewa na hiki kitu, Muungano utavunjwa na hili suala. Acheni kampeni hizi hazitawasaidia karekebishane mkataba uwe wa maslahi kwa taifa basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Simuoni mtu wa kuuvunja muungano huu. Binafsi sioni hata ni kwanini Zanzibar iwe na serikali Yao maana Zanzibar Ina rasilimali Chache sana ambazo asilimia kubwa ya rasilimali zake zinatumika kwenye kulipana mishahara TU baasi. Watu 1,000,000 lakini Wana msululu wa Marais wastaafu wanaolipwa, mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa vilaya, wakuu wa tarafa na kata, wakuruhenzi, na watumishi wa umma.
 
CCM ni hatari Leo wamemleta ROSTAM ili aendelee kuwafilisi

95ac32bd-1698-43ff-b6dc-442d4a6b4d9a.jpg
 
Inafahamika kuwa bandari zetu zinatoa huduma hafifu sana kwa wateja wake wanaozitegemea kwa huduma.

Inafahamika kuwa bandari zetu hazitoi mapato yanayokusudiwa kwa taifa kwasababu mbalimbali zikiwemo zile za:

1. Ukosefu wa utaalam wa kuendesha bandari.

2. Ukosefu wa vifaa vya vya kisiasa vya kuhudumia bandari.

3. Usimamizi mbovu wa bandari.

4. Upigaji mkubwa bandarini.

5. Uwezo wa meli kubwa na nyingi kutia nanga.

6. Wizi mkubwa

Bandari zetu zinahudumia nchi nyingi zinazotuzunguuka ambazo hazina bandari tangu wakati wa ukoloni hadi Leo hii. Huduma ni mbovu sana tangu enzi hizo lakini hakuna mtu aliyewahi kuandamana kupinga huduma mbovu zinazotolewa hata pale wateja wa bandari zetu wanapolalamikia huduma mbovu na wizi hadi kutishia kutuhama. Ubovu huu ulikuwepo kwenye awamu zote za uongozi.

Nikizotizama sura na majina ya wanaotaka kuandamana kupinga bandari isikodishwe kwa DP World kampuni kutoka Dubai Wana harufu ya wale waliokuwa wakinufaika na ulegelege wa usimamizi wa bandari, wangetaka status quo bandarini pale na ni wale wale wanaopinga kila kitu Cha uarabuni. Yaani kule uarabuni hakuna zuri lolote zaidi ya dini zao.

Hivi ni kweli tatizo la mkataba ni kukosekana ukomo wa muda TU? Mbona hata kwenye mkataba wa ndoa hakuna muda lakini wanandoa wanaachana na kutengana pia? Je, kama ukomo utawekwa mkataba utakuwa halali?

Ujinga kama huu ndio unawafanya watawala kuwa madikteta hata kama hawataki kuwa hivyo kwa watu wake. Yaani mtu Yuko radhi hali iwe hivyo hivyo kwa maslahi yake na kundi lake TU.

Wako watu wanaopinga mkataba kwa sababu za kweli, wengine ujinga TU, wengine kwa wivu wa awamu ya 6 kufanikisha, wengine kwa maslahi yao TU na wengine kwasababu za kidini TU.

Hao tunaowapa bandari yetu lazima tuwape malengo na indicators ili kufanya kile tunachokusudia kutoka kwao ni nini Cha kufanya kama malengo yanakwenda kinyume na expectations, Lakini sio kupinga uwekezaji huu.
Sababu zako ziko 6.
Nianze na sababu No.3,4 na 6 zinazohusu ubadhirifu na usimamizi mbovu. Kwa maoni yako haya unatushauri Kila palipo na ubadhirifu na usimamizi tulete Mwekezaji? Ripoti za CAG Kila mwaka zinagundua matumizi mabaya ya fedha za Umma kwenye Halmashauri nyingi nchini, Kwa hiyo nako tulete wawekezaji kuwa Wakurugenzi na wasimamizi wa miradi? Unaposema usimamizi mbovu unaishia ngazi gani na Kwa nini mamlaka zinazouona huo usimamizi mbovu suluhisho pekee wameona na kuleta wageni?
No.5 uwezo wa meli kubwa kutia nanga Bandarini. Hili nadhani hujajiridhisha na takwimu zako. Kina cha bandari ya Dar es salaam ni Sawa na cha Mombasa 15/15 baada ya upanuzi. Kwa hiyo hoja hii inakufa.
No.1 umeongelea utaalamu na No.2 vifaa vya kisasa. Hapa Una hoja na ndivyo Watanganyika wengi wanaolitakia mema Taifa Lao wanapotaka paingiwe ubia au serikali ifanye uwekezaji zaidi. Lakini badala yake matatizo ya bandari ya Dar es salaam yanapelekea tuingia mkataba àmbao hauturuhusu kuendeleza bandari za baharini au maziwa bila kuwauliza wao Mabwana mkubwa DPW. Na kibaya zaidi mkataba unahusisha Hadi Air space. Tunapoongea ubovu wa mkataba na nyie muwe na tafakuri, hatupingi uwekezaji Ila kuletewa mikataba ya kutupoka Uhuru wa kujiamria Mambo yetu kama nchi eti tukitaka kufanya kitu mpaka tumuulize mgeni hatutaki.
 
Mleta mada usifananishe ndoa na bandari nimeishia pale ulikosema ndoa
hapa nilipenda kukuonya kuwa sio mikataba yote inataja muda, ila kila mktaba nilazima uonyeshe utaendeaje kuwa hai na utavunjikaje.
 
Hakuna Muungano wa changuchangu Cha kwako Cha wote.
Walioanzisha Muungano walikuwa na ndoto ya Muungano wa nchi Moja ndio maana Karume alimwambia Nyerere wewe kuwa rais na Mimi makamu tuwe nchi Moja,l lakini Nyerere hakuwa na haraka alitaka vizazi vikacho vikiona faida ya Muungano vije kudai serikali Moja lakini upande mmoja unajiona wao ni waarabu na kuamua kuiuza Tanganyika kwa waarabu.
Hata Nyerere angekuwepo angevunja huu Muungano kwani tuliungana na WA Zanzibar na sio hao waarabu.
Hapa umeongea ukweli na lazima nikupongeze. Wanaoutunza huu muungano uwepo hadi leo ni watanganyika wakati wazanzibar pia wananufaika sana na muungano huu kwa njia mbalimbali. Binafsi ninafahamu kuwa Nyerere hakukusudia kuwa Tanzania itakuwa na Marais 2 kwa wakati mmoja. Yeye alidhani kwa kuiondoa serikali ya Tanganyika basi na wenzake wangeiondoa serikali ya Mapinduzi na kubaki serikali ya Tan(ganyika)zan(zibar)nia, haikuwa hivyo, haiko hivyo na haitakuwa hivyo kwa namna ninavyoona, na wala hakuna Mzanzibar mwenye ndoto kama hiyo.

Lakini pamoja na hayo tumekubaliana kuwa Tanzania ni nchi ya muungano wa nchi mbili ambazo zilikuwa huru kila moja, ni watanganyika wenyewe walioifuta Tanganyika yao kwa sababu zao wenyewe, hatuwezi kuwalaumu Wazanbizar hata kidogo kwenye hilo, kaeni mnyolewe kuhusu hili. Lakini haya yote hayahusiani kabisa na mkataba wa bandari. Wote lazima tukubali kuwa Tanganyika ina bandari nyingi ambazo hazitoi mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu, na hatuwezi kukunja shingo zetu upande kwa miaka 60 mingine tukitegemea kutokee muujiza; something must be done by someone among us now now today to rectify the sitution. Rais Magufuli alisema ni heri uchukue maamuzi hata kama kwa kukosea kuliko kuacha kuchukua maamuzi. Wacha Rais Samia afanye maamuzi ili kazi yetu iwe kumsaidia kuona dosari ndogo na kubwa na maamuzi yako kwa lengo la kuboresha na kusonga mbele lakini sio kumzuia na kumkatisha tambaa wakati Katiba yetu inamtaja kuwa yeye ndiye mkuu wa nchi, mtunza nchi na rasilimali zake zoooote, Amirijeshi mkuu na mfariji mkuu. Badilisha katiba kwanza kuondoa majukumu haya Rais ndio uje kunyoosha kidole. Nakumbuka Mwl. NYERERE kwa kutumia katiba hii aliweza kuchota rasilimali na kodi zetu kwenda kuzikomboa Msumbiji, Angola, Namibia, Zimbabwe, South Afrika, Comoro na hata Uganda bila kuhojiwa na mtu yeyoyote, katiba aliyoitengeneza ilimruhusu kufanya hivyo, na katiba hiyohiyo ya Nyerere ndio hiyohiyo aliyoitumia Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli kutawala. Nakumbuka Rais Magufuli alisemaga "wacha niitumie katiba hiihii kuinyoosha Tanzania na watanzania kwanza kabla haijabadilishwa.
 
Aisee kila nikirudia kusoma hiki ulichoandika nazidi kukuhurumia na kulihurumia taifa langu, hivi brother una percent kwenye hili suala? hivi kweli ndo umeona kabisa kwa akili zako timamu ushabikie hili suala au umeruhusu kushikiwa akili?

Yaani mfano bandari ni yako utaitoa kwa namna hii? Au unaamua tu liwalo na liwe kwa sababu ni ya wengi. Yatakurudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka bandari sio kama madini na miti ya mbao kuwa vinaisha baada ya miaka fulani ya uvunaji. Bandari ni rasilimali ambayo kama huoni tofauti/tija unaichukua hata kwa kumchinja anaekataa kuiachia. Magufuli alivunja mikataba mingapi ya ndani na nje isiyokuwa na tija kwa taifa? mbona nchi ipo na sisi tupo pamoja na mikataba kuvunjwa? Hii sio nchi ya kisulutani viongozi wote wanapita na Rais ajae anakuwa na mamlaka kamili ya kubadili chochote. Tanzania ina sulutani mmoja tu ambae ni CCM.

Kuna kuwadi mmoja wa wazungu anasema, hawa DP World wataingiza kwenye banari zetu tecnologia ya hali ya juu ya kisasa zaidi ambayo itawakosesa watanzania ajira. Hebu sikilia hoja za kijinga kama hizi wanazotumia kupinga mkataba huu. Hajui kuwa watu wengi zaidi wako kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi, na biashara kidogo na wafanyakazi wengi zaidi walioajiliwa ni walimu, wauguzi, na askari. Anashindwa kujua kwamba bandari inayoendeshwa kisasa itazaliza fedha za kuwekeza kwenye kilimo, afya na ulinzi. Na hata wamachinga watapewa mitaji ya biashara maana fedha zipo.
 
Tunataka hayo manufaa yawepo kwenye mkataba tuyapime Kwa muda maalum
 
Manufaa ni ufasini na mapato wa bandari kuliko ilivyo Sasa. Sasa hivi wateja wetu wanalalamika kila wakati kuwa mizigogo Yao inachelewa na inaibiwa bandarini lakini hatuna Cha kufanya. Sasa Mama Samia amekuja na kitu Cha kufanya watu tuache kulalama prematurely.
Hatujakataa uwekezaji

ILA kuwapa bandari kana kwamba tumewauzia yote yote milele HAPANA hapo ndio tunapopinga.

Unaweza vipi mpa mtu mali Yako muhimu sana akae nayo milele sijui miaka 100(Karne).una akili sawa sawa kweli!?

Haya sawa tumewapa na zingine zoooote!!! How comes.

Nasikia na airfield tumewapa eti!!!!

Bandari ni swala la muungano why upande wa pili wa MUUNGANO bandari zao hazipo kwenye contract!? Sio kwamba Kuna watu Fulani Fulani Wana mipango ovu dhidi mali za upande huu wa MUUNGANO!?

Vipi kuhusu suala wa usalama wetu na wataifa limezingatiwa katika terms and condition za mkataba!?

Ikumbwe kuwa bandari ni lango la nchi bidhaa na tools mbalimbali huingia nchini kupitia hapo kuna bidhaa hatarishi kama MADAWA YA KULEVYA, SILAHA HATARI ZA KIVITA, Kuna nyara za TAIFA kama meno ya ndovu, nyama za wanyama pori, na madini yetu coercive instruments walihusika kwenye kuasses haya yote na kutoa ushauri wao wa kitaalamu na kuhakikishiwa ushiriki wao pasipo ingiliwa kisias kwenye kulinda nchi dhidi ya hatari na uporaji wa rasilimali zetu!??

Sawa KITITA kitamu lakini uwe mjinga kukukubaki vitu kirahisi tu UZALENDO wako uko wapi!!???

Waache kutisha Raia Watu wanataka mambo yalinyooka na yenye kulinda maslahi ya TAIFA sio mambo ya ki-MANGUNGO na UKOLONI MAMBO LEO!!!

Umma unataka majibu yalivyooka sio porojo za wapumbavu Fulani wasiotumia akili Bali matumbo yao.
 
Back
Top Bottom