Mimi nafkiri, tusiconclude hivyo, Nia ya Serikali ni njema sana kwenye hili swala, na nafkiri hakuna anayekataa, kwani ni kweli kabisa bandari zetu hazionyeshi improvement yoyote ile katika ufanisi. Mh.Rais aliwahi kusema siku moja ya kwamba, tukitumia bandari yetu kwa ufanisi hata kiasi chote cha bajeti kinatakiwa kitoke kwa mapato yanayokusanywa bandarini (Customs etc).hapo ukiongeza sekta nyingine zenye rasilimali tulizopewa na Mungu kama Utalii,Madini,maliasili etc inaonyesha yote hayo ni mambo mema sana kwani hata huku ndani (domestic taxes kwa wananchi) hatutabanana sana 😂.So juhudi husika za serikali kutafuta mbia,na kumpata DP world ambaye kati ya wabia wote waliokuwa evaluated yeye hakuna ubishi ni the best,hivyo ni swala jema sana hilo.Ila tu kinachozungumzwa na kutia doa hivyo kufanya hata wasiotakia nia njema kutembea humo humo, ni baadhi ya vipengele katika uandishi wa Mkataba wa IGA, kwakuwa hili ni swala la kitaifa, linalohusisha maslahi ya nchi na wananchi, ni vyema kwa serikali kujishusha kidogo na kuangalia vile vipengele ambavyo wananchi na wasomi wamevitilia shaka, kujaribu kuwasiliana na Emirati, viwekwe sawa zaidi ili kuondoa ambiguities na vieleweke hasa zaidi kwa wananchi, halafu revised edition itolewe publicly kupitia Bunge wananchi waridhike, then mikataba mingine iendelee.Hiii itajenga confidence kwa wananchi na kujibu hizi hoja,kwani likiachwa hivi, wale wabaya watatambaa na hoja za upotoshaji hivyo kufanya jambo zima kuonekana baya(kwani ndio ajenda zao kwa sasa) wakati nia ni jema sana,na Mbia husika DP World hakuna shaka yoyoye ya financial and technical powers alizonazo hivyo kututoa hapa tulipo.Nawasilisha