Hapa umeongea ukweli na lazima nikupongeze. Wanaoutunza huu muungano uwepo hadi leo ni watanganyika wakati wazanzibar pia wananufaika sana na muungano huu kwa njia mbalimbali. Binafsi ninafahamu kuwa Nyerere hakukusudia kuwa Tanzania itakuwa na Marais 2 kwa wakati mmoja. Yeye alidhani kwa kuiondoa serikali ya Tanganyika basi na wenzake wangeiondoa serikali ya Mapinduzi na kubaki serikali ya Tan(ganyika)zan(zibar)nia, haikuwa hivyo, haiko hivyo na haitakuwa hivyo kwa namna ninavyoona, na wala hakuna Mzanzibar mwenye ndoto kama hiyo.
Lakini pamoja na hayo tumekubaliana kuwa Tanzania ni nchi ya muungano wa nchi mbili ambazo zilikuwa huru kila moja, ni watanganyika wenyewe walioifuta Tanganyika yao kwa sababu zao wenyewe, hatuwezi kuwalaumu Wazanbizar hata kidogo kwenye hilo, kaeni mnyolewe kuhusu hili. Lakini haya yote hayahusiani kabisa na mkataba wa bandari. Wote lazima tukubali kuwa Tanganyika ina bandari nyingi ambazo hazitoi mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu, na hatuwezi kukunja shingo zetu upande kwa miaka 60 mingine tukitegemea kutokee muujiza; something must be done by someone among us now now today to rectify the sitution. Rais Magufuli alisema ni heri uchukue maamuzi hata kama kwa kukosea kuliko kuacha kuchukua maamuzi. Wacha Rais Samia afanye maamuzi ili kazi yetu iwe kumsaidia kuona dosari ndogo na kubwa na maamuzi yako kwa lengo la kuboresha na kusonga mbele lakini sio kumzuia na kumkatisha tambaa wakati Katiba yetu inamtaja kuwa yeye ndiye mkuu wa nchi, mtunza nchi na rasilimali zake zoooote, Amirijeshi mkuu na mfariji mkuu. Badilisha katiba kwanza kuondoa majukumu haya Rais ndio uje kunyoosha kidole. Nakumbuka Mwl. NYERERE kwa kutumia katiba hii aliweza kuchota rasilimali na kodi zetu kwenda kuzikomboa Msumbiji, Angola, Namibia, Zimbabwe, South Afrika, Comoro na hata Uganda bila kuhojiwa na mtu yeyoyote, katiba aliyoitengeneza ilimruhusu kufanya hivyo, na katiba hiyohiyo ya Nyerere ndio hiyohiyo aliyoitumia Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli kutawala. Nakumbuka Rais Magufuli alisemaga "wacha niitumie katiba hiihii kuinyoosha Tanzania na watanzania kwanza kabla haijabadilishwa.