Suala la bandari lina harufu ya chuki

Mbona unajichanganya? Utawapaje malengo na indicators kama mkataba ulioingia nao haukupi haki ya kufanya hivyo? Hilo ni mojawapo ya mapungufu ambayo hao unaosema wamejaa chuki wanayapigia kelele! Kwa hiyo tuseme na wewe umejaa ujinga na udini kwa sababu umeona upungufu huo?

Amandla...
 
Ni kwa nini makubaliano ya awali (MOU) yalipitishwa kimya kimya na huu mkataba ukajadiliwa kwa spidi bungeni. Why? Unaweza ukawana nia njema ila namna ya utekelezaji wako ukatia shaka
 
Bandari za Zanzibar hazina kazi yoyote ngumu kulinganisha na bandari za Tanganyika. Rwanda, Zambia, Burundi, Malawi, Uganda na DR Congo zinazitegemea bandari zetu pamoja na tz yenyewe. Hivyo bandari za bara lazima ziwe efficient kuliko za Zanzibar.
 
Hivi ni kweli tatizo la mkataba ni kukosekana ukomo wa muda TU? Mbona hata kwenye mkataba wa ndoa hakuna muda lakini wanandoa wanaachana na kutengana pia? Je, kama ukomo utawekwa mkataba utakuwa halali?
Mada yako ingejikita hapo na masharti mengine yaliyomo kwenye makubaliano, hiyo mada ingekuwa na nguvu zaidi.

Badala yake umerudi kule kule wanakoingia wote wanaotetea makubaliano kwa kukazia faida zinazotokana na utendaji mzuri kwenye bandari, mambo ambayo watu hawayapingi, kwa sababu wanajua uzuri wake.

Kwa bahati mbaya vile vile, nawe umejiingiza kulaumu, hata wakati hujui kwa nini wanaokataa hili jambo wanalikataa kwa sababu zipi.
 
Hebu tueleze athari za kiusalama kwa kuwapa bandari DP WORLD. Vilevile tueleze athari za kiuchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba wageni watatujua kuwa tumeingiza nchini silaha gani na gani kwaajili ya jeshi letu? Miaka 60 ya Uhuru bandari inanufaisha Koo Chache tu, redio za magari ya watu zinapotelea bandarini, upigaji wa kutosha, kila siku tunabadilisha watendaji wa bandarini bila mafanikio. Mimi naunga mkono kubinafsifa lakini tuwape malengo, indicators na consequences kama hawatatimiza, lakini lazima tuwape bandari watu wenye ujuzi, uzoefu na mitaji.
 
1. Nchi zinazotegemea bandari ya Dar es salaam watahama watatafuta alternative.
2. Mamluki na kuingiliwa katika nchi itakuwa wazi wazi.

Leo sina mzuqa wa kuandika. Nitafute asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Nchi zinazotegemea bandari ya Dar es salaam watahama watatafuta alternative.
2. Mamluki na kuingiliwa katika nchi itakuwa wazi wazi.

Leo sina mzuqa wa kuandika. Nitafute asubuhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo sio kweli bwana mdogo. Hivi wewe unadhani Tanzania ni wajinga kiasi hicho? Yaani wawaachie wageni bandarini zote huru kabisa wao waende kulala fofofo kule lugalo? Yaani unataka kuwaaminisha watu kuwa TIS, JWTZ, JKT, Polisi, Uhamiaji, Magereza, FFU, mgambo na hata sungusungu wetu wote watapigwa marufuku kukanyaga bandarini. Upuuzi kama huu haujengi taifa. Dunia imeendelea sana, unaweza kupigwa hata adui akiwa Singapore.
 
Ni rahisi sana kusema hawa wanaopinga wanatumwa na watu wenye maslahi makubwa na uendeshaji wa bandari wa sasa. Kuna watu na taasisi zilizokuwa zinaingiza na kutoa mizingo bandarini bila kutozwa ushuru Sasa hivi Wana hofu kubwa, Kuna watu na taasisi ambazo zilikuwa na maslahi ya moja kwa moja na uozo wa uendeshaji wa bandari Sasa hivi Wana wasiwasi kubwa, Kuna watu na taasisi ambazo zilikuwa zinatoa ajira kwa watu wao kwa upendeleo nao Wana hofu kubwa na mkataba huu, wanahofia kitu kinaitwa "change". Watu kama hawa ni hatari sana kwenye taifa. Rais Magufuli rip alipambana nao kwa nguvu zake zote alizojaliwa nazo. Ni watu hatari sana kwa taifa, miaka 62 ya Uhuru taifa limezunguukwa na maji lakini maskini sana lakini hawaandani kupinga umaskini huo, ila wanataka kuandamana kupinga yule anaetaka kuiondosha hali hiyo.

Kuwaongoza waafrika ni kazi ngumu kwelikweli. Mtu anataka kuwekeza matrillion yake ya dollar kwenye bandari zako, je unataka kumpa mkataba wa miaka 10? atazilindaje fedha zake hizo zisipotee? Fedha yake itarudi baada ya muda gani? Yaani unataka mkata unaoweza kuvunjwa na wahuni wakati wowote ili mwekezaji apoteze fedha zake kilevi?

Tunachotakiwa sisi ni kumpa malengo, targets, indicators na miiko baasi ambayo Ina consequences zake kwenye mkataba.
 
Bandari za Zanzibar hazina kazi yoyote ngumu kulinganisha na bandari za Tanganyika. Rwanda, Zambia, Burundi, Malawi, Uganda na DR Congo zinazitegemea bandari zetu pamoja na tz yenyewe. Hivyo bandari za bara lazima ziwe efficient kuliko za Zanzibar.
Hujanielewa, si mmesema bandari zote zilizopo na zitakazokuwepo (zitakazotokea baadaye) zote zipo kwenye mkataba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleza vizuri sana, KAMA TU MALENGO NI HAYA, basi tuendelee! lakini lakini lakini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majizi yaliyodumaza bandari yetu ndo yanayopiga kelele, Samia asisikilize hizo kelele maana zitaendelea kudumaza maendeleo ya nchi
 
Majizi yaliyodumaza bandari yetu ndo yanayopiga kelele, Samia asisikilize hizo kelele maana zitaendelea kudumaza maendeleo ya nchi
Akisikiliza zile kelele za huyo huyo, huyo huyo mchinje mchinje hatafanya maendeleo. Nyingi ya Kelele hizo zinapigwa na majizi, wakwepa ushuru, Wala rushwa, wenye misamaha ya kodi, walionyang'anywa madili, wanasiasa uchwara na makuwadi wa bandari shindani kwenye eneo la East Africa na SADC.

Hata Nyerere angesikia kelele za huyo huyo mchinje mchinje asingejenga vijiji vya ujamaa, asingetaifisha ardhi, asingetoa elimu bure kwa watu wake. Rais Mwingi asingetoa ruksa kwenye uchumi maana Mwl. Nyerere na wajamaa walimkalia kooni. Mkapa asingeuza nyumba na mashirika n migodi na tanesco, kikwete asingeruhusu demokrasia kustawi na Magufuli asingejenga bwawa, reli ya kisasa, kuhamia Dodoma na kujenga barabara ya ubungo - Kibaha.

Huu ni wakati wa Rais kuonyesha kuwa yeye ndiye Rais mbeba maono wa wakati huu. Hivi wahuni wanataka kutuaminisha kuwa bandari zetu zinauzwa?
 
Umesema sahihi kabisa mkuu
 
Bandari za Zanzibar hazina kazi yoyote ngumu kulinganisha na bandari za Tanganyika. Rwanda, Zambia, Burundi, Malawi, Uganda na DR Congo zinazitegemea bandari zetu pamoja na tz yenyewe. Hivyo bandari za bara lazima ziwe efficient kuliko za Zanzibar.
Hizi Bandari za Zanzibar zikiwa Efficient kuna shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…