Suala la bandari lina harufu ya chuki

Kwa nin wanaharaka sana katka swala Hilo? Wanasheria, wanauchumi, na wanadiplomasia why wasipewe muda wa kutosha kushea katika hili Kwa gharama za serikali Ili waujadr mkataba, watoe maagizo Kwa serikari juu ya maeneo yanayotakiwa kuboreshwa
Ukichelewa sana mwekezaji anaweza kughaili na kwenda nchi nyingine. Uwekezaji huu ni tishio kwa bandari za Mombasa, Beira, Angola na hata Durban.
 
Haieleweki hoja yako ni ipi
Hoja ni kwamba tumuache Mama aitumie katiba hiihii ya iyenaiyena waliyoitumia wenzake waliomtangulia kulifikisha nchi hapa ilipo Sasa. Kifupi Wacha wanyoonye wezi wa bandarini ili apate fedha nyingi kutoka bandarini za kuihudumia nchi na watu wake. Hakuna taifa linaweza kununuliwa kwa njia hii. Bandari sio kama madini na mbao kuwa vinaisha, hapana. Waarabu wakituzingua huko mbele tunaweza kuwanyang'anya kama vile tulivyowanyang'anya IPTL, Barick, Richmond, maji, solution group, ATCL, nk.
 
Nchi ina demokrasia sasa, maana wakati wa Magufuli huyu sasa hivi angekuwa anatafutwa na ndugu zake.
 
kila mwanaume Dar atapewa IST bure. 😀 chezea mwarabu weye.
Mama asirudi nyuma wala kutazama nyuma kwenye hili, awe kama dereva wa lori kama watangulizi wake, maana "the ends justify the means". kama ukitaka kufanikisha jambo ambalo wewe unaamini ni kwa nia njema, upendo na kusaidia basi it is better to be feared than loved (Niccolò Machiavelli)
 
Hayo yote yanaonekana kufeli kwa serikali, kwanini tusikabidhi jukumu la kuongoza nchi kwa DPW.
 

Wataalamu wanaongelea vifungu vya MOU wewe unaongelea matatizo ya bandari ni vitu tofauti kabisa! Kama huchukii vile vifungu haujaelewa watu
 
Wataalamu wanaongelea vifungu vya MOU wewe unaongelea matatizo ya bandari ni vitu tofauti kabisa! Kama huchukii vile vifungu haujaelewa watu
Mimi nikwambie kwenye kanuni za uchumi na maendeleo hakuna nafasi ya demokrasia. Engine ya uchumi na maendeleo ni kuziwahi fursa zote kwa wakati, nia njema na uwaminifu. Bara la Ulaya, Asia na USA hawakufika pale pale walipo kiuchumi na maendeleo kwa kutumia demokrasia ya nani anataka na nani hataki. Hata Magufuli alifanya mengi kwa muda mfupi kwasababu aliiweka Kando na kuipiga teke demokrasia kwenye kujenga kupiga kura, kujenga reli na barabara, kusambaza umeme vijijini, kuhamia Dodoma, kufukuza wafanyakazi hewa, kuvunja mifuko ya hifadhi ya jamii, nk.

Kama Rais anataka kufeli kwenye mipango yake ni kuipa siasa na demokrasia kwenye mipango yake. Baba wa taifa hakuhitaji maoni ya mtu kama Tanganyika na Zanzibar ziungane, kama Tanzania isaidie ukombozi wa bara la Afrika, kama Tanzania iende kumpiga Idd Amin, kama wananchi wanakubali kujiunga kwenye vijiji vya ujamaa, alipeleka viberiti TU kuchoma nyumba za wakorofi wasiotaka kuhamia kwenye vijiji vya ujamaa.

Demokrasia inatumika kuzorotesha maendeleo na uchumi. Demokrasia ni silaha ya nchi za magharibi kupenyeza uovu wao kwenye nchi maskini. China Ina raia 1.5b, hivi kama watu wote hao ukiwapa Uhuru wa kuongea, kuamua na kutenda wanavyotaka kitatokea nini?
 
Wengi wanaokuja kupinga uwekezaji wa DPW ni hao hao wanaolia kuona barabara hazijengwi na kukarabatiwa.

Ni hawa hawa wanaolia madawa kukosekana mahospitalini, ni hawa hawa wanaolalamika serikali ya CCM ina miaka 46 haijafanya chochote.

Lakini ni hawa hawa wanaotumia nguvu nyingi kupinga uwekezaji kwa hoja za wanasheria wabobezi wanaochambua baadhi tu ya vifungu vya mikataba na kuacha vingine!.

Wakati tunajikita kwenye siasa za majibizano, Zambia wanaanza upya michakato ya kuitumia bandari ya Angola na kuachana na sisi tunaoshikiwa akili na kina Maria Sarungi na baadhi ya wazee wenye heshima zao mbele ya jamii.

Ni taifa fulani kama ukiweza uliombee kwa Mungu kila unapopiga magoti kanisani au misikitini.
 
Ukifungua milango ya demokrasia unaenda kujihakikishia kushindwa. Humo humo kwenye uhuru wa maoni watakuja watu wa kupinga kile unachokwenda kufanya, kwa nia tu ya roho ya kutaka kuona unashindwa kufika popote!.

Hata kama kile unachokwenda kukifanya kinawahakikishia ubora wa maisha wao watajiweka katika kupinga hoja na malengo yenye nia njema kwao.

Samia ni mwanafunzi wa JK, na anapita mle mle alimopita JK, anazo siasa za usikivu na uungwana. Lakini anajiwekea ugumu yeye mwenyewe kwani anapokwenda kupoteza mteja wa bandari gharama za kuja kumpata mwingine wa kiwango kile kile cha aliyepotea huwa ni kubwa na huchukua muda kuja kuleta tija ya kueleweka.
 
Tunahoji mkataba wa bandari lakini hatuhoji mkataba wa Swissport pale uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam. Akipewa Mzungu sawa lakini akipewa Mwarabu si sawa! Udini utaipeleka pabaya hii nchi.
 
Tunahoji mkataba wa bandari lakini hatuhoji mkataba wa Swissport pale uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam. Akipewa Mzungu sawa lakini akipewa Mwarabu si sawa! Udini utaipeleka pabaya hii nchi.

Ilisikia swissport ilikuwa na IGA
Hata na hao wange linge wapa mkataba badala ya tiss wala isingekuwa tatizo
 
Ilisikia swissport ilikuwa na IGA
Hata na hao wange linge wapa mkataba badala ya tiss wala isingekuwa tatizo
Suala ni IGA au maslahi tunayopata kwenye mkataba? Kwahiyo, kama Swisport siyo IGA kama unavyosema hatuna haki ya kujua tunanufaika vipi? Kuna IGAs ngapi nchi hii hatuzihoji mbona tumekomaa na hiyo ya Dubai? Mlishawahi kuhoji ile mikataba 19 tuliyoingia na Wachina? Kinachowasumbua nyie ni udini na vinginevyo.
 
Kuna guarantee gani kuwa DPW wataperform na kupata faida kama tunavyotegemea!?

Mikataba mingapi umeingia na tumepata faida kama tulivyotegemea!? So far none. Kama upo tuambie. Sasa kuna guarantee gani kuwa hawa DPW wako tofauti na wengine!?

Huoni kuwa kama serikali ingetangaza tender kungekuwa na mashirika mengi ambayo yangeapply. DPW siyo the best so far In the world. Je kama hayo mengine yangekuja na bid nzuri kuliko ya DPW tusingeyakubali?

So far hatujui what DPW will bring about. Kama ingekuwa ni tender tungejua exactly watakuja na nini na faida gani tutapata. So far tunapewa mategemeo tu. Where is their business plan!?
 
Sio wao bali wanatumiwa na wabaya wetu. Hawa watu ndio aliokuwa anapambana nao Rais Magufuli wakati wake. Watu hawa wapo na watakuwepo, wanapinga kila kitu kwa manufaa Yao binafsi. Walipinga bwawa kujengwa, walipinga watu kuhamishwa ngorongoro kwenda msomela wakati hata Wazungu waliwahamisha watu hawa kutoka Serengeti kwenda ngorongoro. Yaani hata pale ngorongoro sio kwao waliletwa TU. Mama Samia asigeuke nyuma.
 
Sentensi yako ya mwisho ina maana kubwa kwa upande wa serikali, kutorudi nyuma hata kidogo.

Hawa wapiga kelele wengi wao hata bandarini hawaingii, hawana shughuli ya kuwapeleka huko.
 
Ni kweli baadhi ya vitengele vina lugha yenye ukakazi kwa mwenye mali, lakini baadhi ya vipengele na lugha ya mkataba huu vinatokana na kiasi cha gharama za uwekezaji utakaofanywa, kiwango chetu na aina yetu ya demokrasia tuliyonayo na namna mikataba ya uwekezaji kutoka nje inavyoandikwa. Mfano, hakuna mwekezaji anaetaka kuwekeza fedha zake nyingi sana mahali ambako hana uhakika mtaji wake utalindwa vipi usipotee. Pili, DP World hana uhakika sana ni lini mradi utabreak even (utaanza kuzalisha faida), hivyo kwenye makubaliano haya ya awali hawezi kukubali umpe muda wa miaka 5, 10 au 20 bila kujua kama hela yake itakuwa imesharudi na kupata faida au vipi, maana bandari zinazoizunguuka bandari za Tanzania ziko nyingi pia, wateja unaowalenga (DR Congo, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia) wanaweza kushawishiwa kuhamia bandari za nchi nyingine. Hivyo kila mwekezaji wa fedha nyingi ni lazima afanye risk register na risk analysis ili kunusa vyanzo vinavyoweza kusababisha fedha zake kupotea. Hawa wanaopiga kelele wengi wao hawana mradi hata wa kufuga kuku. Hivyo mwekezaji hawezi kuwa na mkataba wenye lugha nyepesinyepesi kama vijamaa vinavyotaka uwe.
 
Sentensi yako ya mwisho ina maana kubwa kwa upande wa serikali, kutorudi nyuma hata kidogo.

Hawa wapiga kelele wengi wao hata bandarini hawaingii, hawana shughuli ya kuwapeleka huko.
Watanzania tunapenda kuongea sana, tunawalazimisha viongozi wawe madikteta hata kama hawapendi. Watanzania tunasahau kuwa katiba yetu inamruhusu Rais kuwa dikteta kama akipenda kuwa dikteta. Wanaopiga kelele wanasahau kuwa kila mtu ameteuliwa na Rais hata wale wa mihimili mingine. Nadhani wanamuona Mama Samia badala ya Rais Samia.
 
Kwani ni watanzania wangapi wanaopinga mkataba? Wanaopinga wanamwakilisha nani? Wametumwa na nani? Tumekubaliana kuwa bunge ndicho chombo kikuu kinachowakilisha sauti, mawazo na matakwa ya wananchi wote, hawa akina Slaa, shivj na wengine wanapinga kwa niaba ya nani? Mzee shivj alikuwepo wakati katiba ya aina hii inatungwa na kupitishwa, sheria za vyama vingi zinatungwa na kupitishwa, sheria za uchaguzi zinatungwa na kupitishwa lakini alikuwa kimya Sasa tunaomba aendelee kukaa kimya Sasa na milele bunge na Rais wafanye kazi zao.

Tanzania Ina bandari nyingi, Hakuna mwekezaji mwenye akili timamu atakubali kuweka mapesa yake mengi kwenye bandari ya dar Leo halafu kesho Tanzania inampa mwekezaji mwingine kwenye bandari ya Tanga na keshokutwa anapewa mwekezaji mwingine kwenye bandari ya mtwara watakaoshindana na bandari ya dar kufanyakazi ileile kwa muda uleule. Au serikalini yenyewe ikaamua kuboresha bandari zake nyingine kwa kiwango Cha juu kiasi Cha kutoa upinzani mkubwa na mwekezaji wa bandari ya DSM. Hali ikiwa hivyo yule wa bandari ya dar atarejeshaje fedha yake kwa miaka mingapi? Tusifikiri wakezaji ni wapumbavu kama sisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…