Suala la Bandari TEC hawakupata kama walivyozoea

Dah huyu mzee nadhani anasumbuliwa na tatizo lilelile... ni vizuri akawaona madaktari bingwa pale hospitali karibu na gereza kuu dodoma wakamsaidia tatizo lake
 
😂😂ila hili lizee linapitia kipindi kigumu sana....yaan jambo la kawaida kabisa atalitafutia mtazamo wa kidini lionekane kama Kuna competition flan hv ya waislamu na wakristo...
Yuko obsessed sana na udini mpaka aibu, maana hata busara za kawaida tu zinazotakiwa kwa mtu mwenye umri wake, hakuna, ni upumbavu mtupu
 
Yuko obsessed sana na udini mpaka aibu, maana hata busara za kawaida tu zinazotakiwa kwa mtu mwenye umri wake, hakuna, ni upumbavu mtupu
Watu wanalumbana vipengele vya kimkataba yeye anaangalia how to "dinilise"😂
 
Ni kweli unayosema na kwa kuongezea tu Historia haiandikwi bali inawasilishwa. Historia hujiandika yenyewe sisi wanadamu tunainukuu nakuiwakilisha kama ilivyotokea na si kama tunavyodhani
Kimsingi ilitakiwa iwe hivyo, lakini kwa bahati mbaya historia nyingi zimeandikwa kimaslahi. Nitakupa mifano michache tu.
Hivi unaamini kuwa katika historia tulikuwa tunasoma kuwa ZIWA VIKTORIA, TANGANYIKA nk yaligunduliwa na wazungu...... Licha ya kukuta watu katika maeneo hayo wakiishi na kuvua samaki. Hali kadhalika mlima Kilimanjaro...na ....na...na.
Unajua kuwa katika vitabu vya historia vya Afrika Kusini wakati wa utawala wa wazungu kabla ya Mandela kuingia madarakani: Viliandika kuwa Watu wote Afrika ya kusini ni wahamiaji.......(sasa imefutwa)- Hii iliwekwa kwa lengo maalum, kuwa Afrika kusini hakuna wazawa (native). Hali kadhalika huko Australia.....

Ndugu yangu, Historia ndio mahali pekee kwa watawala husika kuelekeza matakwa yao na kuyarudia mara milioni mpaka mkaamini hivyo. Sijasema ya ziwa Nyasa au Ziwa Malawi. Niishie hapo.
Unaweza kuwa sahihi, lakini kwa bahati mbaya wachangiaji ndio wamevutika huko. Pengine ungemshauri abadili kichwa cha habari. Kwa sababu kwa ajenda 1,2 na 3 ni pana sana na ni vigumu kwa wachangiaji kuelewa wajikite kwa Chadema/uislam/ukatoliki au Uarabu na DP N.K.

Binafsi sikuona busara kumshauri afute bandiko. Haya ni maoni yangu.
 
Hekaya za Mohamed Said
Nan...
Hakika ni Hekaya za Abunwas.
Nakuelewa kwa nini akili yako inakataa kuamini kama hii ni kweli.

Hata picha unaziona lakini huamini.

Wale walioamini historia hii kwangu walikuja na maswali mengi ya kutaka kujua zaidi historia hii.

Wananiuliza imekuwaje hao akina mama wanne na mabaibui na huyo msichana wakamsindikiza Mwalimu Nyerere Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza ya Mwalimu UNO?

Dhifa ya kumuaga Mwalimu Nyerere ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Picha hiyo yuko Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed,
Nawaeleza kuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa alikuwa mke wa Shariff Abdallah Omar Attas na huyu Shariff Attas kajuana na Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes kwani wote wakifanya kazi Kariakoo Market.

Abdul akiwa Market Master na Shariff Attas Mkusanyaji wa Ushuru wa Nafaka hapo sokoni.

Hawa walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU na Bi. Chiku yeye ndiye alikuwa akiwakusanya na kuwahamasisha wanawake kujiunga na TANU na kuhudhuria mikutano ya TANU Mnazi Mmoja kuujaza uwanja na kutia nderemo.

Watoto wawili wa Bi. Chiku, Sakina na Fatina bint Arab walikuwa walimu wakifundisha Al Jamiatul Islamiyya Muslim School.

Hawa mimi ni shangazi zangu si kwa nasaba bali kwa ujamaa kwani kaka yao Mustafa alikuwa rafiki wa baba yangu.

Huyu Mustafa alimuoa mtoto wa Max Mbwana ambae yuko kwenye picha ya tatu na Nyerere pamoja na Mwinjuma Mwinyikambi na Mshume Kiyate.

Bi. Tatu bint Mzee yeye alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU Mwenyekiti akiwa Clement Mohamed Mtamila.

Siku hizo TANU katiba yake ilikuwa na nafasi ya Mwenyekiti na Rais.

Bi. Tatu bint Mzee alihudhuria kikao cha kujadili barua ya Mwalimu Nyerere alioandikiwa na Wamishionari wakimtaka achague moja katika mawili, ualimu au siasa.

Hii ilikuwa baada ya kurejea kutoka UNO.

Prof. Haroub Othman alikutana na Mwalimu baada ya kusoma kitabu cha Abdul Sykes na akamsihi aandike historia yake kwani historia ambayo ndiyo hii hapa naieleza imegeuza si historia ya uhuru wa Tanganyika bali hata historia yake Mwalimu.

Ndugu yangu unaghadhibishwa na historia hii ya wazee wangu ambao wewe huwajui mimi ndiyo nawajua na Mwalimu anawajua na ushahidi ni hizo picha unaiita historia hii hekaya.

Hivi ndivyo inavyokuwa ninapoisomesha historia hii kwa wanafunzi wengine wao wanakuwa na maswali ya kutaka kujua zaidi.

Nyinyi historia hii inawaudhi mnatamani kama nisingeiandika Tanganyika ikabaki kuwa nchi isiyo na historia yake ya wapigania uhuru.
 
Ngumu kupona hilo tatizo
Tresor...
Kila miaka inaposonga mbele katika kujadili suala la historia ya uhuru wa Tanganyika yanakuja mambo mapya.

Binafsi mambo haya yananifurahisha sana.
Kwanza siamini kama kwa dhati ya nafsi zao wanaamini wanachosema.

Nikifika hapa najiuliza sasa ikiwa hivi kwa nini wameona waseme kuwa nina tatizo la upungufu wa akili?

Nikiwa hapa akili yangu sasa inaniambia mimi hawa wenye fikra hii ya kuniona mimi nina tatizo la akili wao bongo zao ziko sawa?

Wanaweza kusimama na mimi, ''toe to toe'' katika uwezo wa matumizi ya akili zetu zao na zangu?

Nani ataibuka mshindi?
Au ni yale ya akutukanae akuchagulii tusi na mdomo haumkatai bwana wake?


 
Ndio maana ni ngumu hii kitu kukutoka kichwani kila uonapo au kusikia hayo we unaghadhibika kw ulaghai huo

Uzuri nimekua nakusoma kila bandiko nani mpz wa hizi history zako ILA KUJA KUWA UNAVYOTAKA NDIO KUGUMU
 
Zawadi...
Nawawekea hiyo clip hapo chini ya usajili wa chama cha TANU mwezi Agosti 1954.

Nawauliza swali moja tu.
Walipata kuisikia historia hii mahali popote ikielezwa?:

 
Ndio maana ni ngumu hii kitu kukutoka kichwani kila uonapo au kusikia hayo we unaghadhibika kw ulaghai huo

Uzuri nimekua nakusoma kila bandiko nani mpz wa hizi history zako ILA KUJA KUWA UNAVYOTAKA NDIO KUGUMU
Tresor...
Sijapatapo kughadhibika.
Pitia post zote tazama nani anatukana na nani anakejeli na nani anaweka vitisho.
 
Kwani kwenye Biblia imeandikwa mungu aliwaambia wakristo walinde muungano ?? Huu muungano si wa hiari ?? Wazanzibari wakati wote wanasema hawautaki muungano , kwa nini yeye atake kuulinda tena na kumhusisha Mungu ??
Jaribu kuwaza nje ya box. Muungano uliasisiwa na watu kwa hiari yao. Na jambo likishakubaliwa na wengi kiimani ni mpango wa Mungu. Je, wewe ulitaka Askofu Pengo achochee watu kanisani wapinge muungano? Kuutaka muungano au kutoutaka ni jambo la kisiasa na si jambo linaloshughulikiwa na Kanisa.
 
Mohammed, unajitahidi sana kuandika, hakuna anaekataa hao akina mama kumsindikiza Nyerere uwanja wa ndege siku anaenda UNO kwa mara ya kwanza. Ndiyo walimsindiki so what? Kipi cha kujifunza ktk usindikizaji wao huo? Swala hapa je, hao akina mama walimsindikiza kwasababu ya uanchama wao ndani ya TANU au kwasababu ya Uislam wao? Ukitofautisha haya mambo mawili Sheikh utakuwa kwenye mstari.
 
Mwanzoni nilikuwa napinga watu walivyokuwa wanakusema wewe ni mdini ... Haunaga mada Wala Chochote zaidi ya udini ... pathetic
 
Sasa naamini hata wapumbavu mnazeeka ..... Sio kila Mzee ana hekima ...wewe ni mpumbavu ....kila Andiko lako ni udiniudini udini ....
 
Mbussi,
Ilikuwaje basi historia hii ya mashujaa hawa waliopigania uhuru wa Tanganyika ikawa haisomeshwi?

Leo historia hii imekusanywa na kuandikwa kwa nini inapigwa vita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…