America is in a survival mode, doing exactly what General Eisenhower did in 1957 when the coalition of Israel, Grear Britain and France chose to invade Egypt without America's authorisation. America made an example and every nation in Europe was frightened and ended up complaining, but to no avail.
Labda tukumbushane kidogo mambo ya msingi ambayo waungwana wengi wa dunia hii hawayafahamu wala kutaka kuyakubali.
Mosi, serikali ya D.J.Trump ndiyo iliyoipa nchi ya Ukraine silaha nzito, fedha na mafunzo makubwa kiasi cha kuifanya iwe ndiyo nchi yenye jeshi bora kabisa barani Ulaya. Ukraine alikuwa na jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa kuliko Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Sasa unaposema D.J.Trump ni pandikizi unakuwa na maana gani labda ?
View attachment 3246225
Tokea mwaka 2016 hadi 2021, serikali ya Trump ambayo ndiyo imemgeuka Zelensky sasa, ndiyo ilikuwepo madarakani na kuipa Ukraine hizi silaha nzito za kupambana na Urusi. Hivyo hapa Joe Biden hahusiki kabisa, ni Trump na unafiki wa kimarekani. Mtu yoyote mwenye ufahamu hawezi kukubali kwamba hizi silaha zilikuwa kwa ajili ya mapambo.
Pili, Vladmir Putin amewekewa vikwazo vingi za US CONGRESS siyo THE PRESIDENCY, hivyo mambo mengi anayofanya Trump hayako kisheria. Mfano mzuri ni vikwazo vya kiuchumi, ambavyo vimedhihirisha udhaifu mkubwa wa US+G7 kwamba, nguvu walizokuwa wanaamini wanazo kiukweli hawanazo.
Urusi kawekewa vikwazo zaidi ya 20,000, lakini mpaka sasa ndiyo taifa ambalo limeongoza kukua kiuchumi mwaka 2023-2024 na kuwa la kwanza kiuchumi barani Ulaya tukitumia kikokotoo cha Purchasing Power Parity, ambacho kinatumika na IMF. Ila ukiangalia upande wa pili, vikwazo vimeyadhuru zaidi mataifa ya Ulaya kama Ujerumani ambalo mpaka sasa limeingia rasmi kwenye mdororo wa uchumi (Recession).
US+G7 walitegemea kwamba vikwazo pekee vingeweza kuiangusha Urusi na kama akipigana vita basi lazima itakula kwake na NATO watabada Urusi kwenye kona, ili waanze kushughulika na Uchina.
Matokeo yamekuwa tofauti kabisa. Uchina na Urusi ziko karibu kupita kiasi, Urusi ndiyo taifa lenye jeshi kubwa lenye uzoefu wa vita likiwa tayari limezifahamu mbinu za kijesho za NATO na matumizi ya vifaa vyao, na kubwa kuliko hilo viwanda vya Urusi vya kijeshi ambavyo mwaka 2021 vilikuwa vimefilisika, leo hii viko hai na vinazalisha silaha kwa haraka na wingi kuliko taifa lolote lile duniani.
Tatu, tulifanya mjadala mwaka 2022 kule PM nikakwambia ufanya utafiti kuhusu The Bretton Woods I (1945), The Bretton Woods II (1971) na The US Dollar Exorbitant Privilege. Ambapo nikakwambia kabisa kama ukishafahamu haya, utajua ni kwanini mwisho wa siku Marekani amefika hapo alipo, na vikwazo vya uchumi vitakuwa na madhara makubwa kwa mataifa yote duniani.
Marekani mpaka sasa, hawezi kumtishia URUSI na vikwazo vingine, wala hawezi kujaribu kutuma vikosi nchini Ukraine. Kiuchumi hayuko vizuri katika kipindi hiki (In Industrial Terms), hivyo ni mpaka ajipange kwa muda kidogo.
Nne, Marekani anamvuta Urusi akitegemea atafanikiwa kufanya kile ambacho Kissinger alikifanya mwaka 1972 baada ya kutumia mwanya wa mgogoro baina ya USSR na PRC (SINO-SOVIET SPLIT), na kufanikiwa kuyetenganisha mataifa makubwa ya kikomunisti duniani. Uchina alimgeuka Urusi vibaya sana na kuwa upande wa Marekani.
Wataalamu wanasema kwamba, Vladmir Putin ambaye ni msomi mzuri wa historia anafahamu madhara ya kuwatenganisha Urusi na Uchina, hivyo hawezi kurudia hayo makosa. Kiufupi ni kwamba Urusi akicheza vizuri atakuwa anakula BREAKFAST, Washington DC, LUNCH Brussels na DINNER Beijing.
Rubio kasema wanampango wa kuondoa vikwazo (Sijui kama Congress itaruhusu) na kurudisha makampuni ya Marekani Urusi. Ukifuatilia kwa undani utafahamu, huu mkakati walianza nao kule India, baada ya kutaka kumzima Uchina kwa kutumia India ila ikashindikana kwasababu mazingira ya India ni tofauti na Uchina.
Hivyo mpango ni kuondoa viwanda Uchina na kuvipeleka Urusi. Urusi ni tofauti na Schengen Zone, kwasababu kuna Cheap Labour, Investor Friendly Climate, Unlimited and Infinite number of Cheap Resources, Available Energy and Powerful Intellectual Base.
Hivyo, Marekani akiwekeza Russia kwa nguvu, ni rahisi sana kumgeuza Urusi kuwa mshindani mkubwa wa biashara wa Uchina. Uchumi wa Urusi ambaye ni mzungu, ukifungamanishwa na G7 na EU, ni rahisi kugeuza URUSI tajiri na yenye nguvu kijeshi kama LAUNCH-PAD in a coming struggle against CHINA.
Swala ni kwamba: Je wataweza kuifanya Urusi hivyo ???
Sidhani kama Russia inaweza ikakubali hilo kwa sababu ikiwa hilo litatokea itakuwa si hatari kwa China pekee bali hata na Russia pia. Ukizingatia haya mataifa yanasaidia kuwepo kwa balance ya dunia, hali ikiwa tofauti athari itakuwa mpaka kimataifa kiujumla.
Ikiwa Russia itakubali hilo tafsiri yake ni kukubali mabadiliko ya kiuchumi, kidiplomasia na ushawishi wa kimataifa na kijeshi na kiusalama kwa upande wake na kwa upande wa China pia kimataifa kiujumla.
Russia kwa sasa inategemea sana China kwa biashara ya gesi asilia na mafuta. Uwekezaji mkubwa ambao tumeushuhudia uliyofanyika baina yake na China kwenye hilo. Kumkwepa China itakuwa ni pigo kubwa sana kwa sasa kiuchumi kwa Russia ukizingatia wamagharibi si wa kuaminika wakiwa na malengo yao.
Halikadhalika, Russia itapoteza ushawishi kimataifa kwani China ni mshirika wake muhimu sana. Ikiwa kama Russia ikiingia kwenye mkakati utakaofanyika kupunguza nguvu za China, kwa upande wa kimataifa itasababisha Russia kujikuta imejitenga kimataifa.
Kwa upande wa China nao itakuwa ni tishio kwa kupungua ushawishi wake kimatifa kwani haitakuwa na mshirika mwenye nguvu kama Russia hususani ukiangalia Marekani na UK wanaweza kuongeza ushawishi wao katika Asia.
Kimsingi, kutokuwa pamoja kwa Russia na China kwao wote pamoja wanaweza kupata tishio la kiuchumi na kiusalama. Nafikiri Russia ata balance kama ulivyosema lunch atakulia kwa wamagharibi na dinner kwa Xi Jin Ping.
--------------
Aidha, athari za kwa mfumo wa kimataifa, migogoro ya kikanda itaongezeka. Kufanya hivyo ni kuipa nguvu NATO, hivyo migogoro itazidi na ukizingatia NATO walivyokuwa na michezo ya kihuni wanaweza kugusa mpaka sehemu zenye maslahi yao yaani China na Russia.
Ushirikiano wa China na Russia umesaidia kuleta usawa katika siasa za kimatifa kwa kiasi chake. Ikiwa Russia itakubali kutumikia huo mpango wa magharibi dhidi ya China maana yake ni kupunguza huu ushirikiano kati yao na hali ambayo inaweza kusababisha kuongeza migogoro hapa duniani.