Suala la Iran limeshakuwa gumu? Trump anadai kuna nchi hazina shauku ya kuisadia Marekani

Suala la Iran limeshakuwa gumu? Trump anadai kuna nchi hazina shauku ya kuisadia Marekani

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Suala Iran linaonekana limeanza kuwa gumu kwa Marekani, Trump leo ametema Nyongo na kuzishutumu baadhi ya nchi kutokuwa na shauku za kuisaidia Marekani kutatua changamoto ya mfereji wa Hormuz, licha ya kuwa nchi hizo zilikuwa zinaitegemea Marekani kiulinzi kwa zaidi ya miaka 40.
Trump anadai
"Kwa miaka 40, tunawalinda, na hamtaki kushiriki.”

Trump, ameamua kuzitupia lawama baadhi ya nchi kwa kutotaka kujihusisha na mgogoro wake unaoendelea Mashariki ya kati na akizitaja baadhi kuwa na vikosi vyenye askari wa Kimerakani zaidi 40,000 wakilinda usalama katika nchi hizo, lakini bado hizo nchi zimekuwa nzito kwenye kulipa fadhira hiyo.
Trump anataja kuna baadhi ya nchi aliziomba vifaa vya kutegua mabomu ya kutegwa kwenye maji, lakini zilimjibu kuwa "Ni vyema zisingejihusisha na mgogoro huo".


Kwambali naona kabisa kijembe hiki kimepigwa kwa ndugu zetu Wajerumani... Mapema leo Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani bwana Boris Pistorius aliweka wazi msimo wa nchi hiyo kuwa "hiyo vita sio ya wajerumani na sio tatizo letu, hivyo halituhusu"




Ugumu unatokea wapi?

Wachambuzi wadai kuwa licha ya Marekani kuwa na vifaa vya kisasa kuizidi Iran, vita hii inaweza kuwa ngumu kwasababu tu ya utofauti wa mikakati na mbinu za kivita ambazo haziwezi kufanikisha malengo ya mazingira ya vita yaliyopo Iran.

  • Mbinu ya Marekani ya Shock and Awe haiwezi kuwa mbadala wa kuuangusha utawala wa Iran, Ni lazima kuwe na vita vya ardhini tofaouti kabisa na huu mkakati wa Shock and Awe ambao umejikita kwenye kuonesha mabavu ya kijeshi pamoja na kutawala anga la nchi adui.
  • Vikwazo vya uhalali wa vita, Suala la maamuzi ya kufanya mashambulizi ya vikosi vya miguu linaoneka kususua, kitu ambacho watu wanadhani ni kutokuwepo kwa uhalali wa vita hiyo kwasababu Trump, hakuomba baraka za Congress kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo.

Changamoto ya mabomu ya kutegwa kwenye maji. Ni wazi suala la kudhibiti lango la Hormuz lilikuwa suala gumu kwa nchi ya Iran, hii ni kutokana na uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo ukilinganisha na uwezo wa Marekani. Hali imebadilika baada Iran kuanza kutumia Mabomu ya kutega majini, kuzuia meli kupita katika eneo hilo. Hii imefanya ugumu hata kufanya dolia za kulinda meli katika lango la bahari la Hormuz.

Ni kweli suala la Iran limeanza kumpwelepweta Trump?
Kuna watu wanaweza kudhani hii kazi imekuwa ngumu na haina Mbadala, Binafsi sitaki kuamini hivyo. Mapema wiki hii Marekani imehamisha kikosi chake namba 31 cha Wanaji (31st Marine Expeditionary Unit) kutoka Okinawa, Japan na kuelekea Mashiriki ya kati. Hii inaashiria maandalizi ya vita vya ardhini nchini Iran..

da113cb2-6ffe-41b5-a431-c921b84924c3.png


31st MEU si kikosi tu cha askari wa majini, bali ni askari wenye mafunzo yanayoendana kabisa mahitaji kufanya operation za vikosi vya miguu kwenye ardhi ya Iran. Hiki ni kikosi cha Wanamaji chenye askari wapatao 2,200 wenye mafunzo ya kufanya operation za haraka.
Kikosi hiki kimeundwa na sehemu kuu tatu:
  • Kitengo cha Mapigano ya Ardhini: (Watoto wa miguu/Magari ya kivita na uvamizi wa kupitia fukwe - AAV).
  • Kitengo cha Mapigano ya Angani: (Ndege za MV-22 na F-35B).
  • Kitengo cha Usafirishaji na Ugavi (Logistics).
Kikosi hiki kinajumuisha wataalamu wa kijeshi (Military Occupational Specialty (MOS)) waliobobea katika uvamizi wa kutokea majini, upelelezi, na kutoa msaada wakati wa majanga. Kiufupi wanaendana kabisa na mahitaji ya kivita kwa hali kama iliyopo Iran,


Taaluma za Kijeshi (MOS) za Askari wanaunda kikosi cha 31st MEU
Screenshot_16-3-2026_215139_docs.google.com.jpeg


Hatahivyo kikosi hiki kina askari wanaokadiliwa kufikia 2200 tu, pekayao wanaweza wasifanye chochote, Matumaini makubwa yapo kwenye utayali wa Wanamgambo wa Kikurdi ambao wadai kuwa mchawi ni Droni za Shahed 136, ila wakipata msaada wa ulinzi wa anga, muda wowote wanaweza kuanza kukinukisha. Maswali ni mengi juu ya utayali wa Kikurdi kipindi ambacho hatawao wameshaanza kupata vikwazo kutoka makundi yanayofadhiliwa na Iran yalipo nchini Iraki.

Wakuu, hii ngoma ni mbichi sana kwa mtazamo wa kijeshi.
 
Trump ana kigeugeu kama kinyonga haaminiki na Ulaya hawako tayari kupeleka watoto wao wakafe kwasababu ya vita isiyowahusu. Marekani wametishia mara ngapi kujitoa NATO? Wao ndio chanzo na chokochoko ya vita ya Ukraine iliyofanya mamilioni ya Euro za kodi za wananchi ziende huko.
Donald Trump hana uhusiano mzuri na EU kwa kiburi na madharau yake. Viongozi wa nchi za Ulaya wana akili timamu na wengi wao sio supporters wa Netanyahu.
Analaumu kuhusu msaada wa vita wakati biashara za wamarekani EU zinafungwa? Huyu mzee kapagawa na Ulaya hakubaliki labda mafashisti kama yeye wachache
 
Kweli kuna nchi zimeitegemea kiulinzi kwa zaidi ya miaka 40
Lakini Je wanalinda bure? Au wanalipwa?
Nijuavyo mimi wanalipwa tena hela ndefu kwa uwepo wao kama nchi za mashariki ya kati
Na sio Marekani pekee bali nchi nyingi zinalinda
 
Kweli kuna nchi zimeitegemea kiulinzi kwa zaidi ya miaka 40
Lakini Je wanalinda bure? Au wanalipwa?
Nijuavyo mimi wanalipwa tena hela ndefu kwa uwepo wao kama nchi za mashariki ya kati
Na sio Marekani pekee bali nchi nyingi zinalinda
Anazungumzia NATO
 
Mtu kalikoroga mwenyewe bila sababu zozote Leo anataka msaada kutoka kwa watu wengine wasio husika,ulaya nao wanashindwa kuungana wakaishusha USA kama superpower nation.
 
Back
Top Bottom