Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katueleza wazi kuwa licha ya Ukuta wa Mererani, bado madini yanatoroshwa.

Pia Rais Saia akatueleza kuhusu Mkataba wetu na Kampuni ya Madini ya Barrick kuwa kuna mambo mle kwenye mkataba hayajakaa vizuri.

Sasa najiuliza, kama Mkataba ndani ya kataba wetu na Barrick bado kuna mambo ya ajabuajabu mle je kwa nini hayakutatuliwa kabla ya kusaini?

Je, kwa nini serikali ya Magufuli chini ya Waziri wake Kabudi waliuaminisha umma kuwa mkataba ule ni mzuri sana kwetu?

Kama Taifa ni lazima struggle ya kutaka tunufaike na madini yetu iendelee, na ni lazima serikali itueleze ukweli kwa sababu madini ni urithi wetu.

IMG_20210407_153341.jpg
 
Pia Rais Saia akatueleza kuhusu Mkataba wetu na Kampuni ya Madini ya Barrick kuwa kuna mambo mle kwenye mkataba hayajakaa vizuri.
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
 
Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?

Hata kama bosi wake alikuwa na tabia za ubabe na kutosikiliza ushauri, lakini sidhani kama ushauri wake huo angemwambia mwendazake angekataa kuufanyia kazi hasa alivyokuwa akipigania rasilimali za hili taifa.

Inawezekana kabisa ile hotuba ya Rais jana alichanganya na kaumbea kidogo ili kunogesha kijiwe kama zilivyo tabia za wanawake wengi, awe makini huyu mama na hizi rasilimali za taifa letu, tusijekusikia tena zile habari mtoto wa fulani kakamatwa China na madawa wakaweka bond madini au gesi yetu, kuchekeana kukizidi mwishowe hugeuka msiba mkubwa.

Zaidi ya hapo naona Rais alikuwa sahihi, masuala ya mikataba ya madini tuliyoingia na wazungu lazima yapelekwe taratibu kwani yapo kisheria, bado tunawahitaji hao watu, Tanzania sio kijiji ndio maana Lissu yalimkuta aliposema haya, kulazimisha kubadilisha mikataba sasa hivi ni kujitafutia hasara tu kwa serikali yetu, kila siku ndege zetu zimekuwa zikikamatwa huko nje, hapa naamini ndio maana Rais alisema kuna baadhi ya mambo tusilazimishe kutunishiana misuli na hao jamaa, bado tunawahitaji.
 
Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?...
Hata mimi nilishangaa

Nikajiuliza alijuaje kama hayo mambo yanafanyika ina maana alikuwa anajua kitambo au?
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.

Anaropoka tu ili na yeye aonekane ila hamna kitu specific anacho ongea, aseme kwenye mkataba mpya kuna changamoto hii na hii ? Amesharuhusu wa gesi ya Mtwara LNG waje, amesharuhusu wa Hellium waje atawapa tu kwa mikatabu yoyote wanayotaka, ameruhusu expatriates waje ovyo ovyo tu , kwa akili zake huu ndio uchumi...
 
Ukiwa VP kuna Taarifa hupati, anapata raisi tu
Sasa mama amekuwa Rais kaelezwa kila kitu na anatueleza Ukweli, Na I hope atachukua hatua!, Ndiyo kwanza ana wiki tatu tu madarakani!

Hata Magufuli naye alipoukwaa urais alitueleza baadhi ya madudu aliyoyakuta hususan Hayahaya ya madini!
 
Anaropoka tu ili na yeye aonekane ila hamna kitu specific anacho ongea, aseme kwenye mkataba mpya kuna changamoto hii na hii ? Amesharuhusu wa gesi ya Mtwara LNG waje, amesharuhusu wa Hellium waje atawapa tu kwa mikatabu yoyote wanayotaka, ameruhusu expatriates waje ovyo ovyo tu , kwa akili zake huu ndio uchumi...
Sasa mwendazake angekuwa amefanya homework yake vizuri kwenye ishu ya madini, hayo madudu ya madini kutoroshwa huko Mererani, na Ishu ya mkataba wenye madudu na Barrick vingetoka wapi?
 
Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?...
kama alimwambia mara kadhaa boss wake na hamna hatua iliyochukuliwa je?
au kama kapenyezewe hivi karibuni asiseme?

si afadhali yy anaonyeshe bati linavujia wapi, wakt tuliaminishwa tupo safi
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
Jiwe hakuwahi kumshirikisha Mh. Samia.
 
Katika sekta ambazo Mwendamseke alifanya vizuri ni sekta ya madini.
 
Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?

Hata kama bosi wake alikuwa na tabia za ubabe na kutosikiliza ushauri, lakini sidhani kama ushauri wake huo angemwambia mwendazake angekataa kuufanyia kazi hasa alivyokuwa akipigania rasilimali za hili taifa.

Inawezekana kabisa ile hotuba ya Rais jana alichanganya na kaumbea kidogo ili kunogesha kijiwe kama zilivyo tabia za wanawake wengi, awe makini huyu mama na hizi rasilimali za taifa letu, tusijekusikia tena zile habari mtoto wa fulani kakamatwa China na madawa wakaweka bond madini au gesi yetu, kuchekeana kukizidi mwishowe hugeuka msiba mkubwa.

Zaidi ya hapo Rais alikuwa sahihi, masuala ya mikataba ya madini tuliyoingia na wazungu lazima yapelekwe taratibu, bado tunawahitaji hao watu, Tanzania sio kijiji ndio maana Lissu yalimkuta aliposema haya, kulazimisha kubadilisha mikataba sasa hivi ni kujitafutia hasara tu kwa serikali yetu, kila siku ndege zetu zimekuwa zikikamatwa huko nje, hapa naamini ndio maana Rais aliposema kuna baadhi ya mambo tusilazimishe kutunishiana misuli na hao jamaa, bado tunawahitaji.
kisa hiki kina husu zama za kiongozi mbabe Joseph Stalin.

Ni kwamba baada ya kifo cha Joseph Stalin, alirithiwa na Nikita Khrushchev, Khrushchev alirithi kiti cha uraisi na ukuu wa baraza kuu la kijamaa Katika taifa la Urusi, Siku moja Nikita akiwa anahutubia Kamati Kuu huku akipinga sera nyingi za mtangulizi wake, mjumbe mmoja bila ya kujitambulisha alikereka na akamundikia ki note cha kumshutumu na kumlaumu, "We Nikita ulikua msaidizi wa
Stalin kwa nini hukusema haya kipindi hicho Stalin akiwa hai?"

Nikita Khrushchev akakisoma ki-note na akaomba mjumbe aliyeandika anyooshe mkono juu ili amtambue ndipo amjibu.
Hakuna mkono ulionyooshwa..!!

Khrushchev akasema "Kinachokushinda wewe kunyoosha mkono leo, ndo hicho hicho kilicho nishinda mimi kusema enzi hizo".
Kipi umejifunza hapa!!
 
Back
Top Bottom