Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
"Mimi sishauriki, ukinishauri ndiyo naharibu kabisaaaa" - Jiwe-2016
Hapo ulitaka Mama afanyeje ndugu Taga?
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.

Ningekuwa mimi ningeanza kuwauza Mataga wote nikianza na wewe, sijui kwanini Mama anawalea sana
 
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katueleza wazi kuwa licha ya Ukuta wa Mererani, bado madini yanatoroshwa

Pia Rais Saia akatueleza kuhusu Mkataba wetu na Kampuni ya Madini ya Barrick kuwa kuna mambo mle kwenye mkataba hayajakaa vizuri.

Sasa najiuliza, kama Mkataba ndani ya kataba wetu na Barrick bado kuna mambo ya ajabuajabu mle je kwa nini hayakutatuliwa kabla ya kusaini?

Je kwa nini serikali ya Magufuli chini ya Waziri wake Kabudi waliuaminisha umma kuwa mkataba ule ni mzuri sana kwetu?

Kama Taifa ni lazima struggle ya kutaka tunufaike na madini yetu iendelee, na ni lazima serikali itueleze ukweli kwa sababu madini ni urithi wetu.

View attachment 1745842
Mama alinisikitisha sana jana kutokana na kauli zake. Hana power ya ku negotiate huyu. Na angekuwa ni Rais toka mwanzo hata hiyo 16% tusingeipata. Mimi najua ugomvi uliobaki na Barick ni kipengele cha kodi ambayo serikali inasema inawadai Barick. Sikuona haja ya kusema maneno aliyoyasema hapo. Ni kweli Business ni win win situation lakini kwa kusema hadharani eti sisi tuwanyenyekee kwasababu tunawahitaji zaidi ilifanya niumie kama Mtanzania. Unaweza ukakubaliana nao ukasema hili la kodi za nyuma tunalifuta na tunaanza upya full stop na si kuwapa wale jamaa viburi. Kila nchi Mungu amewapa rasilimali zao, wakitumia vizuri zinawatoa na kuwaaidisha. Serikali ya Hayati Magufuli anagalau walipata USD million 300 (zaidi ya Billion 700 toka Barick na tukaunda Kampuni ya pamoja ya Twiga.

Changamoto zipo lakini mama aangalie yapi ya kusema kwenye media. Mimi kwasasa kama Mtanzania nitabaki mtazamaji kwanza mpaka nimuelewe mama Philosophy yake ni ipi. Nikasikia tena juzi nilishinda mtandaoni naaangalia vitu nikasema tatizo jingine linakuja. Anaweza wasahau wengi kwa manufaa ya wachache. Uzuri hesabu hazidanganyi na Muda ni tabibu mzuri. Tusubiri tuone. Ila namtakia kila la heri. Akifanikiwa katika kazi yake wamefanikiwa kama watanzania, akiyumba tunayumba wote.

Tuanze kupambania Katiba Mpya, Reforms za Mahakama, Bunge, Sheria za Vyombo vya habari n.k. Ninatamani sana kuiona Tanzania yenye neema na iliyo mfano kwa dunia Nzima kuanzia Uchumi, Demokrasia, Usawa wa kijinsia, haki za binadamu, Siasa za Kistaarabu na enye tija kwa nchi na Uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kulinda Rasilimali zetu. Home Sweet Home Tanzania.
 
Huwezi jua, yawezekana Boss wake ndiye mhusika mkuu wa utoroshaji wa hayo madini.

Kuna tetesi zilikuwa zinasema kuna walinzi toka PK wanalinda kule Mererani na madini yanatoroshwa kwenda Rwanda chini ulinzi mkali.

Sasa unafikiri kwenye tuhuma hizi, mwendazake anakwepaje wizi wa madini?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Hisia hizi japo zinaweza kuwa kweli, nakupa 50/50.
 
Anaropoka tu ili na yeye aonekane ila hamna kitu specific anacho ongea, aseme kwenye mkataba mpya kuna changamoto hii na hii ? Amesharuhusu wa gesi ya Mtwara LNG waje, amesharuhusu wa Hellium waje atawapa tu kwa mikatabu yoyote wanayotaka, ameruhusu expatriates waje ovyo ovyo tu , kwa akili zake huu ndio uchumi...
Kuna mmoja alijenga International Airport kijijini kwake akidhani ndiyo uchumi, Mataga zamu hii lazima mtage kabisa, hama nchi mkuu
 
Ukiwa VP kuna Taarifa hupati, anapata raisi tu
Sasa mama amekuwa Rais kaelezwa kila kitu na anatueleza Ukweli, Na I hope atachukua hatua!, Ndiyo kwanza ana wiki tatu tu madarakani!

Hata Magufuli naye alipoukwaa urais alitueleza baadhi ya madudu aliyoyakuta hususan Hayahaya ya madini!
Usijigeuze msemaji wa Rais, wacha hoja mezani ijadiliwe.
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Unaropoka ndugu, kuna mahali amesema anataka kuvunja mkataba? Alichokisema kuna mambo ya Kodi hayako sawa inawezekana tunalipwa midogo au kuna mkanganyiko wa kulipa kodi
 
Mama alinisikitisha sana jana kutokana na kauli zake. Hana power ya ku negotiate huyu. Na angekuwa ni Rais toka mwanzo hata hiyo 16% tusingeipata. Mimi najua ugomvi uliobaki na Barick ni kipengele cha kodi ambayo serikali inasema inawadai Barick. Sikuona haja ya kusema maneno aliyoyasema hapo. Ni kweli Business ni win win situation lakini kwa kusema hadharani eti sisi tuwanyenyekee kwasababu tunawahitaji zaidi ilifanya niumie kama Mtanzania. Unaweza ukakubaliana nao ukasema hili la kodi za nyuma tunalifuta na tunaanza upya full stop na si kuwapa wale jamaa viburi. Kila nchi Mungu amewapa rasilimali zao, wakitumia vizuri zinawatoa na kuwaaidisha. Serikali ya Hayati Magufuli anagalau walipata USD million 300 (zaidi ya Billion 700 toka Barick na tukaunda Kampuni ya pamoja ya Twiga.

Changamoto zipo lakini mama aangalie yapi ya kusema kwenye media. Mimi kwasasa kama Mtanzania nitabaki mtazamaji kwanza mpaka nimuelewe mama Philosophy yake ni ipi. Nikasikia tena juzi nilishinda mtandaoni naaangalia vitu nikasema tatizo jingine linakuja. Anaweza wasahau wengi kwa manufaa ya wachache. Uzuri hesabu hazidanganyi na Muda ni tabibu mzuri. Tusubiri tuone. Ila namtakia kila la heri. Akifanikiwa katika kazi yake wamefanikiwa kama watanzania, akiyumba tunayumba wote.

Tuanze kupambania Katiba Mpya, Reforms za Mahakama, Bunge, Sheria za Vyombo vya habari n.k. Ninatamani sana kuiona Tanzania yenye neema na iliyo mfano kwa dunia Nzima kuanzia Uchumi, Demokrasia, Usawa wa kijinsia, haki za binadamu, Siasa za Kistaarabu na enye tija kwa nchi na Uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kulinda Rasilimali zetu. Home Sweet Home Tanzania.
Nyie Sukuma Gang mulishindwa mkaendekeza ukanda ukabila pamoja ba limbukeni zenu sasa munaanza kupiga lamuli duh....kweli ndani ya wiki tatu unataka Mama atekeleze nini? Mumeibia nchi wee kwa kujificha nyuma ya mgongo wa kizalendo eti munasaidia wanyonge.......ila Mungu sio Osman Meko kaanga dunia
 
"Mimi sishauriki, ukinishauri ndiyo naharibu kabisaaaa" - Jiwe-2016
Hapo ulitaka Mama afanyeje ndugu Taga?
Actually ni ufinyu wa mawazo kumuita "taga" au "nyumbu" yeyote aliye na mtazamo tofauti na wa kwako. Huu ni ugonjwa.
 
Back
Top Bottom