Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Anaropoka tu ili na yeye aonekane ila hamna kitu specific anacho ongea, aseme kwenye mkataba mpya kuna changamoto hii na hii ? Amesharuhusu wa gesi ya Mtwara LNG waje, amesharuhusu wa Hellium waje atawapa tu kwa mikatabu yoyote wanayotaka, ameruhusu expatriates waje ovyo ovyo tu , kwa akili zake huu ndio uchumi...
Hata mm nilishangaa

Nikajiuliza alijuaje kama hayo mambo yanafanyika ina maana alikuwa anajua kitambo au?
Jamani , wafuasi wa Jiwe hamuamini macho yenu. Jiwe halinyanyuki tena . Limetumbukia shimoni .

Mlipoambiwa na wapinzani kuwa katiba yetu ni mbaya hamkuelewa. Katiba yetu inamfanya Rais bila kujali ni nani kujifanyia chochote akitakacho. Na ndiyo maana watawala hawataki ibadilishwe ili Rais awekewe kidhibiti mwendo

Odhis *
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.

He! Tena azungumzie nitty gritty za kila sekta wale viongozi wangeondoka pale saa ngapi?

Haya ni lazima yametoka huko kwenye source na yeye amehighlight ili yafanyiwe kazi, otherwise unavyotaka wewe angejiteua pia kuwa Waziri wa Madini.
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Weka hizo nakala za mikataba yote miwili tuchambue ili tujue upi ni bora. Ila kama hauna na wewe umesikia sikia tu wa sasa bora kutoka kwa Mwendazake basi tulia, nafikiri Rais anajua zaidi kuliko zizi wapiga kelele na mapambio.

Suala la LNG, hilo sio suala geni kwani kiwanda cha kuchakatwa tayari kipo mbioni kujengwa na watu wameshaanza kulipwa fidia tangu mwaka jana. Plan ipo 2022 kiwanda kianze kujengwa.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
kisa hiki kina husu zama za kiongozi mbabe Joseph Stalin.
Ni kwamba baada ya kifo cha Joseph Stalin, alirithiwa na Nikita Khrushchev, Khrushchev alirithi kiti cha uraisi na ukuu wa baraza kuu la kijamaa Katika taifa la Urusi, Siku moja Nikita akiwa anahutubia Kamati Kuu huku akipinga sera nyingi za mtangulizi wake, mjumbe mmoja bila ya kujitambulisha alikereka na akamundikia ki note cha kumshutumu na kumlaumu, "We Nikita ulikua msaidizi wa
Stalin kwa nini hukusema haya kipindi hicho Stalin akiwa hai?"
Nikita Khrushchev akakisoma ki-note na akaomba mjumbe aliyeandika anyooshe mkono juu ili amtambue ndipo amjibu.
Hakuna mkono ulionyooshwa..!!
Khrushchev akasema "Kinachokushinda wewe kunyoosha mkono leo, ndo hicho hicho kilicho nishinda mimi kusema enzi hizo".
Kipi umejifunza hapa!!
Asante, well noted.
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
Magufuli alihitaji usaidizi wa Nani? Kwa hili nitamtetea yeyote anayeinesha kujitambua baada ya kifo cha Dikteta yule. Yeye mwenye aliwahi kusema mkimshauri ndo mnaharibu kabisa, sasa Nani angeendelea kutoa ushauri anaojua hata robo yake haitapokelewa?
 
Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?

Hata kama bosi wake alikuwa na tabia za ubabe na kutosikiliza ushauri, lakini sidhani kama ushauri wake huo angemwambia mwendazake angekataa kuufanyia kazi hasa alivyokuwa akipigania rasilimali za hili taifa.

Inawezekana kabisa ile hotuba ya Rais jana alichanganya na kaumbea kidogo ili kunogesha kijiwe kama zilivyo tabia za wanawake wengi, awe makini huyu mama na hizi rasilimali za taifa letu, tusijekusikia tena zile habari mtoto wa fulani kakamatwa China na madawa wakaweka bond madini au gesi yetu, kuchekeana kukizidi mwishowe hugeuka msiba mkubwa.

Zaidi ya hapo naona Rais alikuwa sahihi, masuala ya mikataba ya madini tuliyoingia na wazungu lazima yapelekwe taratibu, bado tunawahitaji hao watu, Tanzania sio kijiji ndio maana Lissu yalimkuta aliposema haya, kulazimisha kubadilisha mikataba sasa hivi ni kujitafutia hasara tu kwa serikali yetu, kila siku ndege zetu zimekuwa zikikamatwa huko nje, hapa naamini ndio maana Rais alisema kuna baadhi ya mambo tusilazimishe kutunishiana misuli na hao jamaa, bado tunawahitaji.
Huwezi jua, yawezekana Boss wake ndiye mhusika mkuu wa utoroshaji wa hayo madini.

Kuna tetesi zilikuwa zinasema kuna walinzi toka PK wanalinda kule Mererani na madini yanatoroshwa kwenda Rwanda chini ulinzi mkali.

Sasa unafikiri kwenye tuhuma hizi, mwendazake anakwepaje wizi wa madini?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mama asikiri udhaifu ameshaanza kukiri unyonge unadai kodi yako halafu unaweka mikono nyuma hii haiwekani hata kidogo
Dai kodi mikono umeweka mfukoni maana wewe mama ni mwenye nyumba
 
Mimi matabiri leo 2025 vijana wengi na vigogo wengi wataenda upizani
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Mama Samia anachotaka kufanya ni kufufua mazungumzo yaliyokuwepo tayari lakini yalizimwa kutokana hayakuwa na maslahi, hivyo bora mazungumzo yafanyike na timu za wataalamu wetu ili ikiwezekana kufanyika kifanyike kama hakiweekani basi, hajasema kuwa yeye awape rukhsa ya kufanya wanayoyataka kufanya hao wawekazaji, HAPANA. Nchi inataka fedha ili tuweze kuendelea hizo pesa mtazitoa wapi? Wafanya biashara wameshakamuliwa tuliyobaki ni sisi raia wa kawaida na tena tuna bahati lakini tungeanza kulipa kodi ya kichwa kama zamani.
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
Unajua kitu kinacho itwa "highlight speech".....huwezi kutatua kila jambo kwenye public speech alicho fanya ni ku highlight vitu muhimu atakavyo shughurikia.... ila mataga mnateseka sanaa
 
Mama Samia anachotaka kufanya ni kufufua mazungumzo yaliyokuwepo tayari lakini yalizimwa kutokana hayakuwa na maslahi, hivyo bora mazungumzo yafanyike na timu za wataalamu wetu ili ikiwezekana kufanyika kifanyike kama hakiweekani basi, hajasema kuwa yeye awape rukhsa ya kufanya wanayoyataka kufanya hao wawekazaji, HAPANA. Nchi inataka fedha ili tuweze kuendelea hizo pesa mtazitoa wapi? Wafanya biashara wameshakamuliwa tuliyobaki ni sisi raia wa kawaida na tena tuna bahati lakini tungeanza kulipa kodi ya kichwa kama zamani.
Hakikia tuna bahati kweli.
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
Magufuli ndiye aliyekuwa rais na kauli ya mwisho. Sukuma Gang kubalini tu zamu yenu imekwisha
 
Back
Top Bottom