Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?

Hata kama bosi wake alikuwa na tabia za ubabe na kutosikiliza ushauri, lakini sidhani kama ushauri wake huo angemwambia mwendazake angekataa kuufanyia kazi hasa alivyokuwa akipigania rasilimali za hili taifa.

Inawezekana kabisa ile hotuba ya Rais jana alichanganya na kaumbea kidogo ili kunogesha kijiwe kama zilivyo tabia za wanawake wengi, awe makini huyu mama na hizi rasilimali za taifa letu, tusijekusikia tena zile habari mtoto wa fulani kakamatwa China na madawa wakaweka bond madini au gesi yetu, kuchekeana kukizidi mwishowe hugeuka msiba mkubwa.

Zaidi ya hapo naona Rais alikuwa sahihi, masuala ya mikataba ya madini tuliyoingia na wazungu lazima yapelekwe taratibu kwani yapo kisheria, bado tunawahitaji hao watu, Tanzania sio kijiji ndio maana Lissu yalimkuta aliposema haya, kulazimisha kubadilisha mikataba sasa hivi ni kujitafutia hasara tu kwa serikali yetu, kila siku ndege zetu zimekuwa zikikamatwa huko nje, hapa naamini ndio maana Rais alisema kuna baadhi ya mambo tusilazimishe kutunishiana misuli na hao jamaa, bado tunawahitaji.
Yumkini boss wake ndiye aliyekuwa anatorosha chini kwa chini alaf amwambie ili iwe nini
 
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katueleza wazi kuwa licha ya Ukuta wa Mererani, bado madini yanatoroshwa.

Pia Rais Saia akatueleza kuhusu Mkataba wetu na Kampuni ya Madini ya Barrick kuwa kuna mambo mle kwenye mkataba hayajakaa vizuri.

Sasa najiuliza, kama Mkataba ndani ya kataba wetu na Barrick bado kuna mambo ya ajabuajabu mle je kwa nini hayakutatuliwa kabla ya kusaini?

Je, kwa nini serikali ya Magufuli chini ya Waziri wake Kabudi waliuaminisha umma kuwa mkataba ule ni mzuri sana kwetu?

Kama Taifa ni lazima struggle ya kutaka tunufaike na madini yetu iendelee, na ni lazima serikali itueleze ukweli kwa sababu madini ni urithi wetu.


View attachment 1745842
Swala la madini kutoroshwa JPM alishamwambia doto wakati anamuapisha kuwa anasikia madini bado yanatoroshwa, baada ya kuapishwa tu doto alienda mererani kama unakumbuka. swala la barrick kutokana na statement ya mama inaonekana kuna baadhi ya mambo serikali na barrick bado wanavutana ndio maana mama anasema sisi ndio wahitaji. hii maana yake mama anataka tuwakubalie barrick ili mambo yaende kama kawaida. mambo gani sisi hatuyajui, je tutaumia au tutafaidika tukikubali hayo mama anayoyasema tuyamalize hatujui. mama has to be very careful, asikubali kila jambo.
 
Anaropoka tu ili na yeye aonekane ila hamna kitu specific anacho ongea, aseme kwenye mkataba mpya kuna changamoto hii na hii ? Amesharuhusu wa gesi ya Mtwara LNG waje, amesharuhusu wa Hellium waje atawapa tu kwa mikatabu yoyote wanayotaka, ameruhusu expatriates waje ovyo ovyo tu , kwa akili zake huu ndio uchumi...
Kwani mwendazake alisema kuna nini kwenye hiyo mikataba?

Wote ni wale wale,bora ya huyu anayetaka twende sawa kila mtu afurahi.
 
Inahitajika hekima sana kudeal na cartels kama Barrick na Glencore's, hawa jamaa ni zaidi ya mafia ktk kulinda maslahi yao.

Tafadhali Mama yetu mpendwa yote yawe kwa maslahi ya taifa
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Hii miktaba ifike mahali iwe open to the public.

Hii nchi imeliwa sana, mzungu hana huruma.
 
Back
Top Bottom