Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Suala la Madini: Serikali ya Magufuli haikutueleza ukweli wote

Alifanya vizuri, au alilazimisha tuone alifanya vizuri?
Alifanya vizuri. Kile kitendo cha kuanzisha masoko ya dhahabu ni kete nzuri sana. Kukataza usafirishaji wa makinikia nao ulikuwa mchezo mzuri sana. Kwenye Tanzanite iliyokuwa inakatwa India akasema ikatwe hapa na wabongo wakaanza kufundishwa ni kete nzuri. Kupitia mikataba ya madini nalo lilikuwa jambo zuri sana. Katika hii miaka mitano aliyokaa unataka kuniambia hajafanya zuri hata moja? Upinzani wa hivyo siyo kabisa.
 
Ni wapi nimesema hajafanya lolote zuri? Ama unasema hivyo ili kuupa nguvu utetezi wako? Sio lazima kila mtu atumie neno kufanya vizuri, mimi nakubali kabisa kuwa kuna baadhi ya mambo kafanya sawa kutokana na wajibu wake. Na kimsingi hakuna mtu ambaye hajawahi kufanya zuri lolote, hata Iddy Amini, kaburu Pieter Botha walifanya mazuri yao, tena mengi tu. Je wana sifa yoyote ya hayo mazuri yao?
 
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katueleza wazi kuwa licha ya Ukuta wa Mererani, bado madini yanatoroshwa.

Pia Rais Saia akatueleza kuhusu Mkataba wetu na Kampuni ya Madini ya Barrick kuwa kuna mambo mle kwenye mkataba hayajakaa vizuri.

Sasa najiuliza, kama Mkataba ndani ya kataba wetu na Barrick bado kuna mambo ya ajabuajabu mle je kwa nini hayakutatuliwa kabla ya kusaini?

Je kwa nini serikali ya Magufuli chini ya Waziri wake Kabudi waliuaminisha umma kuwa mkataba ule ni mzuri sana kwetu?

Kama Taifa ni lazima struggle ya kutaka tunufaike na madini yetu iendelee, na ni lazima serikali itueleze ukweli kwa sababu madini ni urithi wetu.

View attachment 1745842
Kwamba tuwanyenyekee kwa kua tunawahitaji? mama ajue wanatuhitaji zaid wao we are rich .....tunapoelekea tunaweza uzwa
 
Na safari hii mtaongea mpaka kikwenu ngedere wa kijani nyinyi.

Mlijimilikisha chama, mkataka kujimilikisha nchi, yoyote aliepinga mipango yenu aligeuka adui.

Na una bahati kadi yangu ya CCM nimeiwacha mbali ningekutumia mpaka picha.

Selikali ndio nini??

Usikifiki ndio nini??

Maenda ndio nini??

Nyinyi ndio mliomfanya Mheshimiwa hayati rais Magufuli akachukuwa kwa tamaa zenu. Mkimuabudu na kumtukuza kuliko Mungu na wengine tuliposema hii si sawa mkatutilia fitina kwamba Sisi ni wapinzani.

Tukaitwa kujieleza na mengine mengi.

Sasa tunawaambia mkae kwa kutulia tunataka kujenga nchi.

Because of you, Tanzanians have suffering for good 5 years so you can benefit your bellies.

Tulieni nyie genge la wahuni

Duuu, Mkuu nahisi ungefungiwa chumba kimoja na huyo mshamba kwa vyovyote mmoja lazima angepoteza maisha, sio kwa hasira hizi 😀😀😀
 
Kwamba tuwanyenyekee kwa kua tunawahitaji? mama ajue wanatuhitaji zaid wao we are rich .....tunapoelekea tunaweza uzwa

Uuzwe mara mbili, kuna mkataba wowote umewahi kuuona kwa macho? Uliwahi kuiona mikataba 16 ya siri JK aliyoingia na wachina?
 
Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?

Hata kama bosi wake alikuwa na tabia za ubabe na kutosikiliza ushauri, lakini sidhani kama ushauri wake huo angemwambia mwendazake angekataa kuufanyia kazi hasa alivyokuwa akipigania rasilimali za hili taifa.

Inawezekana kabisa ile hotuba ya Rais jana alichanganya na kaumbea kidogo ili kunogesha kijiwe kama zilivyo tabia za wanawake wengi, awe makini huyu mama na hizi rasilimali za taifa letu, tusijekusikia tena zile habari mtoto wa fulani kakamatwa China na madawa wakaweka bond madini au gesi yetu, kuchekeana kukizidi mwishowe hugeuka msiba mkubwa.

Zaidi ya hapo naona Rais alikuwa sahihi, masuala ya mikataba ya madini tuliyoingia na wazungu lazima yapelekwe taratibu kwani yapo kisheria, bado tunawahitaji hao watu, Tanzania sio kijiji ndio maana Lissu yalimkuta aliposema haya, kulazimisha kubadilisha mikataba sasa hivi ni kujitafutia hasara tu kwa serikali yetu, kila siku ndege zetu zimekuwa zikikamatwa huko nje, hapa naamini ndio maana Rais alisema kuna baadhi ya mambo tusilazimishe kutunishiana misuli na hao jamaa, bado tunawahitaji.
issue ni kuwa mkataba ulishasainiwa ila anaona kuwa makadirio ni makubwa sana hivyo kufikiria namna ya kupunguza ili kuleta unafuu kwa mwekezaji na si vinginevyo maana mzee Magu alikuwa harembi, ni ama madini yatunufaishe au waondoke wayaache na si vinginevyo
 
Kama
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
Kama alikua sidelined utamlaumu kwa lipi?
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Tuliaa wewe au jamaa arudi?
 
Duuu, Mkuu nahisi ungefungiwa chumba kimoja na huyo mshamba kwa vyovyote mmoja lazima angepoteza maisha, sio kwa hasira hizi 😀😀😀
Hawa jamaa ni wa kuogopa sana mkuu.

Hawa ndio walionshauri mwendazake kwamba ili atawale vizuri basi lazima auangamize upinzani kwa namna yoyote ile hata ikibidi..........

Leo rais wetu hayati Magufuli kaondoka wanataka uzandiki wao wauhamishie kwa Mama.

Tutazaa nao hawa
 
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katueleza wazi kuwa licha ya Ukuta wa Mererani, bado madini yanatoroshwa.

Pia Rais Saia akatueleza kuhusu Mkataba wetu na Kampuni ya Madini ya Barrick kuwa kuna mambo mle kwenye mkataba hayajakaa vizuri.

Sasa najiuliza, kama Mkataba ndani ya kataba wetu na Barrick bado kuna mambo ya ajabuajabu mle je kwa nini hayakutatuliwa kabla ya kusaini?

Je, kwa nini serikali ya Magufuli chini ya Waziri wake Kabudi waliuaminisha umma kuwa mkataba ule ni mzuri sana kwetu?

Kama Taifa ni lazima struggle ya kutaka tunufaike na madini yetu iendelee, na ni lazima serikali itueleze ukweli kwa sababu madini ni urithi wetu.

View attachment 1745842
We we hukumuelewa Mama, yaani kwenye huo uwekezaji wa Ubia na Barrick, JPM alibana kila kona ili Taifa linufaike kupitia madini. Mama anataka apangue vifungu ili kuwalegezea wawekezaji kwa kuondoa au kupunguza baadhi ya kodi.
 
Mama alinisikitisha sana jana kutokana na kauli zake. Hana power ya ku negotiate huyu. Na angekuwa ni Rais toka mwanzo hata hiyo 16% tusingeipata. Mimi najua ugomvi uliobaki na Barick ni kipengele cha kodi ambayo serikali inasema inawadai Barick. Sikuona haja ya kusema maneno aliyoyasema hapo. Ni kweli Business ni win win situation lakini kwa kusema hadharani eti sisi tuwanyenyekee kwasababu tunawahitaji zaidi ilifanya niumie kama Mtanzania. Unaweza ukakubaliana nao ukasema hili la kodi za nyuma tunalifuta na tunaanza upya full stop na si kuwapa wale jamaa viburi. Kila nchi Mungu amewapa rasilimali zao, wakitumia vizuri zinawatoa na kuwaaidisha. Serikali ya Hayati Magufuli anagalau walipata USD million 300 (zaidi ya Billion 700 toka Barick na tukaunda Kampuni ya pamoja ya Twiga.

Changamoto zipo lakini mama aangalie yapi ya kusema kwenye media. Mimi kwasasa kama Mtanzania nitabaki mtazamaji kwanza mpaka nimuelewe mama Philosophy yake ni ipi. Nikasikia tena juzi nilishinda mtandaoni naaangalia vitu nikasema tatizo jingine linakuja. Anaweza wasahau wengi kwa manufaa ya wachache. Uzuri hesabu hazidanganyi na Muda ni tabibu mzuri. Tusubiri tuone. Ila namtakia kila la heri. Akifanikiwa katika kazi yake wamefanikiwa kama watanzania, akiyumba tunayumba wote.

Tuanze kupambania Katiba Mpya, Reforms za Mahakama, Bunge, Sheria za Vyombo vya habari n.k. Ninatamani sana kuiona Tanzania yenye neema na iliyo mfano kwa dunia Nzima kuanzia Uchumi, Demokrasia, Usawa wa kijinsia, haki za binadamu, Siasa za Kistaarabu na enye tija kwa nchi na Uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kulinda Rasilimali zetu. Home Sweet Home Tanzania.
Una hoja inayoeleweka ila who knows?? Pengine Mama ameamua kuwa mkweli na asiwe muongo muongo na wala asiongoze nchi kwa propaganda na uongo mwingi.

Mama ameamua kunguru aitwe kunguru na njiwa aitwe njia.

Mama hataki kujifanya anafanikisha kwa fedha zetu wenyewe wakati anakopa. Kwahiyo ni Bora watanzania waelezwe ukweli, ukweli unaweza ukawauma lakini hakika utawaweka huru.
 
SSH ana wenge anataka kuuza kila kitu, hivi mkataba wa zamani wa Barrick na wa saivi upi bora? Hapo ameshawakaribisha wa gesi Mtwara LNG waje tu atawaruhusu kwa masharti yoyote, Hellium mbugani, huyu anataka kuuza kila kitu, hizo kwake ndio akili.
Kwenye mkataba wa Barrick Magufuli alipiga percent yake.
 
We we hukumuelewa Mama, yaani kwenye huo uwekezaji wa Ubia na Barrick, JPM alibana kila kona ili Taifa linufaike kupitia madini. Mama anataka apangue vifungu ili kuwalegezea wawekezaji kwa kuondoa au kupunguza baadhi ya kodi.
Wewe hukumsikiliza kabisa mama. Na kama ulimsikiliza basi ubongo wako umejaa mavi.

Ni wapi mama alisema anataka apangue vifungu ili kuwalegezea wawekezaji kwa kuondoka au kupunguza baadhi ya kodi??

Halafu hizi propaganda zenu hizi na hizo team zenu sijui team JPM hebu mukome sasa.

Mama aachwe afanye kazi
 
Naona chadema mnashangilia wee kama vile kuna chochotemna gain.

Hizi sifa zenu kwa Samia haziwezi kuwainua na chama lenu hilo.

Mngekuwa na akili mngetumia huu muda kupigani mifumo ambayo huwa mnadai ina wanyima ushindi lakini kwa kuwa nyie ni wajinga basi endeleeni kuungana na ccm kumsifia huku mkijifariji kwamba mnawakomoa mataga
Sio Chadema wanashangilia. Ni Sisi Watanzania tunashangilia. Na hata kama Chadema wanashangilia basi wanashangilia tumaini jipya lililopo mbele yao.

Wanaamini sasa hakuna atakaetekwa, wanaamini hakuna atakae nyang'anywa pesa zake na wanaamini watakapopata maafa Mama atawafariji japo kwa maneno mazuri.

Enyi wazandiki na wanafiki wa nchi hii, tambueni kuwa Sisi Watanzania tumeamua kumuachia mama afanye kazi.
 
Katika speech yake hajasema amekusudia kufanya kipi ili kudeal na hayo mambo ambayo "hayajakaa vizuri"?

Kuongeaongea sana bila kuwa na clear action plans ni sawa na bure tu. Afterall huyu alikua pembeni ya Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano. Hata kama inaonekana JPM alikuwa anamside line kwenye baadhi ya mambo, huyu hawezi kukwepa kuwajibika kwa mambo yote ya hovyo yaliyofanyika kipindi chote cha Magufuli.
Aliyeuza nyumba za Serikali aliwajibika kwa ufisadi wake ?
 
Let Great Thinkers discuss hii kitu. Wewe endelea kupiga kimya na kusoma comments. Unapoanza names calling tena kwa majina ya ajabu ajabu unaonyesha tu jinsi gani ambavyo elimu yako haikukusaidia. Hoja hupingwa kwa hoja.

Sukuma gang ni kitu gani?
Sukuma gang ni kundi la wanafiki na wazandiki ndani ya Taifa la Tanzania ambao walishajimilikisha Chama cha mapinduzi, na ambao walikuwa kwenye mchakato wa kujimilikisha nchi yetu ya Tanzania kabla ya Mungu wetu kuamua kuingilia kati na kupindua mipango yao miovu, ya kishenzi, kidhalimu, kinafiki na kizandiki.
 
Back
Top Bottom