Kuna baadhi ya vitu alivizungumza jana nikashindwa kumuelewa, kwa mfano aliposema kuhusu madini kutoroshwa kupitia chini ya ardhi kama ni kweli alijua hili alichukua hatua gani kumwambia bosi wake?
Hata kama bosi wake alikuwa na tabia za ubabe na kutosikiliza ushauri, lakini sidhani kama ushauri wake huo angemwambia mwendazake angekataa kuufanyia kazi hasa alivyokuwa akipigania rasilimali za hili taifa.
Inawezekana kabisa ile hotuba ya Rais jana alichanganya na kaumbea kidogo ili kunogesha kijiwe kama zilivyo tabia za wanawake wengi, awe makini huyu mama na hizi rasilimali za taifa letu, tusijekusikia tena zile habari mtoto wa fulani kakamatwa China na madawa wakaweka bond madini au gesi yetu, kuchekeana kukizidi mwishowe hugeuka msiba mkubwa.
Zaidi ya hapo naona Rais alikuwa sahihi, masuala ya mikataba ya madini tuliyoingia na wazungu lazima yapelekwe taratibu kwani yapo kisheria, bado tunawahitaji hao watu, Tanzania sio kijiji ndio maana Lissu yalimkuta aliposema haya, kulazimisha kubadilisha mikataba sasa hivi ni kujitafutia hasara tu kwa serikali yetu, kila siku ndege zetu zimekuwa zikikamatwa huko nje, hapa naamini ndio maana Rais alisema kuna baadhi ya mambo tusilazimishe kutunishiana misuli na hao jamaa, bado tunawahitaji.