Pre GE2025 Suala la maslahi ya Tanganyika tunataka liwe addressed kampeni 2025!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
No reform no election ni kauli mbiu nyingine inayokuja na kupita, ni sawa na zile za Mbowe alizobuni kila kukicha na kupiga pesa kutoka kwa wazungu.
Kweli, unadhani hivyo?
Tusubiri tutayaona matokeo yake. Mambo yamebadilika sana. Pengine huko uliko wewe ndani ya CCM mmepofushwa na utamu mnao ufaidi.
 
Sidhani kama mtu wa kawaida kule Munjebwe au Tandahimba ni mmoja wa wale wanaokerwa na uwepo wa muungano.

Watanzania wengi wa huko mikoani wanazo shida zao ambazo zikitatuliwa watakuwa hata hawahitaji kujua Kiembe samaki au mwanakwerekwe ni sehemu ya JMT.

Nyingi ni nadharia tu za humu mitandaoni katika maisha halisi ya kawaida ambayo Mtanzania anapata yale mahitaji muhimu ya kimaisha simuoni yoyote mwenye hata kuumiza kichwa kuzijadili hizo kero za muungano.

Hii ni mada ambayo msingi wake mkuu unamlenga Samia na awamu yake ya sita.
 
Dah!
Mmenogewa hadi mnajitoa ufahamu kiasi hiki?
 
Kweli, unadhani hivyo?
Tusubiri tutayaona matokeo yake. Mambo yamebadilika sana. Pengine huko uliko wewe ndani ya CCM mmepofushwa na utamu mnao ufaidi.
Watanzania nawajua vizuri na nina uzoefu wa siasa zetu, Mbowe alipiga kelele kuhusu maandamano wakajitokeza watu wawili tu, yeye na binti yake tena wote wakakamatwa.

Watu wanazo shida zao na CCM inafahamu mbinu zote za kuwavutia ili siku ya uchaguzi waende wakapige kura.
 
Endel ea kudhani hivi, mkuu 'steve'. Sijui kama vitenge mnavyo wapa na kibaba cha unga vitaendelea kuwaziba akili hawa watu mnao wadharau kiasi hiki!
 
SAWA mkuu, nami ninao uzoefu wa kutosha kwa kukufahamu kupitia kwenye mijadala yetu hii.
 
EeeenHeeee Heeee!
Umetoa mfano sahihi kabisa wa huyo Mbowe na mwanae!
Hivi hukuwahi kudadisi kwa nini ilikuwa hivyo, na kama uliwahi kujiuliza; ulipata jibu kuwa hali itabaki kuwa hivyo milele?

Bila shaka nyinyi watu wa CCM mtakuwa mmewaroga hawa waTanzania daima warukwe na akili vichwani mwao!
 
Ndio maana machadomo mnapuuzwa,Tanganyika ndio Nchi gani tena? 😁😁
Pumbavu sana wewe, hatukuwa na zanzibar baada ya muungano tulikuwa na Tanzania visiwani. Kama ilionekana Zanzibar iriudi,unawezaje kusema Tanganyika ndo nini!
Tanganyika ni nchi kama ilivyo Zanzibar.
 
Alieanzisha wazo la ajira za bara 20% watoke Zanzibar alikosea sana na sijui alilenga nini hasa! Vijana wetu wanaandamana hawana ajira, kwenye halmashauri huku bara wamejaa wazanzibar tupu! Kweli inauma sana!
 
Heko sana kiongozi kwa kuona mbali.
 
Kuungana kuna faida kuliko kutengana na mpaka leo heri wanaoungana kuliko wanaotafuta sababu za kutengana.
Kuungana kuna faida lakini lazima iwe ''win-win situation'' . Kwasasa Zanzibar si mshiriki wa Muungano

Nisaidie kuelewa hapa, ni faida gani inazopata Tanganyika au Zanzibar kwa muundo huu wa Mungano!
Nitajie chache tu! kama unazo
 
Sasa Mhuni Lissu atalielezeaje kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025 wakati yeye hautaki huo uchaguzi?
Kupitia 'no reform no election' ndipo hoja kama hizi zinaelezeka

Tundu Lissu (TAL) kaanza kulieleza suala hili kifundi sana.Ni wenye kutumia vichwa kwa usahihi na ukamilifu wanamwelewa. TAL akasema moja ya reform wanazotaka ni ugawaji wa majimbo ya uchaguzi

TAL akasema mfumo unaotumika sasa unazingatia miundo mbinu , na si population, akatoa mfano,Wapiga kura wote wa Zanzibar ni 500,000 wakiwa na majimbo 50 (yaani Wabunge 50).

Dar es Salaam peke yake in Wapiga kura Milioni 3 ikiwa na Wabunge 10. Usawa upo wapi?

TAL akatoa mfano, wastani wa jimbo la Zanzibar ni wapiga kura 11,000. Jimbo la Ubungo lina wapiga kura Laki 3. Kwa maneno mengine, Wabunge 30 wa Zanzibar wanawakilisha idadi sawa na Mbunge wa Ubungo.

TAL akauliza, imeandikwa wapi kwamba Zanzibar lazima iwe na Wabunge kadhaa! hivyo kufanya hata idadi yao kuwa na Wapiga kura 3,200 (Jimbo la Donge) Idadi ndogo kuliko Wanafunzi wa UDOM au UDSM

TAL anasema Mbunge wa Zanzibar anapata mshahara sawa na Mbunge wa Nyamagana, Ilala, au Arusha.
Kubwa Zaidi, Mbunge wa Zanzibar anapewa pesa za mfuko wa Jimbo kama yule wa Temeke au Tunduru!

Zaidi ya hapo, pesa za mfuko wa jimbo zinatoka JMT ambayo ni walipa kodi wa Tanganyika.
SMZ haina mfuko wa jimbo kwasababu Wabunge wake wanapata kutoka Dodoma.

Ndio maana TAL anasema lazima kuwe na reform za uchaguzi na muundo! hadi hapo hujamwelewa?
 

Kwa sasa hakuna mtu wa kuitetea Tanganyika. Walioko CCM hawana ujasiri, na wengine wamelambishwa asali au waoga. Nje ya CCM wanatengenezewa zengwe kama Dr Slaa alivyofanyiwa.
 
Kuungana kuna faida lakini lazima iwe ''win-win situation'' . Kwasasa Zanzibar si mshiriki wa Muungano

Nisaidie kuelewa hapa, ni faida gani inazopata Tanganyika au Zanzibar kwa muundo huu wa Mungano!
Nitajie chache tu! kama unazo
Kule kuungana peke yake ni faida kubwa, unajua kitu gani kinachompa jeuri Donald Trump mpaka anafukuza wamexico wakiwa na pingu miguuni na mikononi?, ni muungano wa majimbo yanayounda kitu kinachoitwa USA.

Kumbuka kuwa kuna wapemba wameoa wandendeule wa kule Nyasa.

Kumbuka kuwa kuna watumbatu wameoa waha wa Kigoma,

Kumbuka kuwa kuna Wakerewe wameoa wakojani.

Hawa wote ndio nguvu kazi ya Taifa la JMT na ndio faida za kivitendo za uwepo wa muungano wetu.

Umeshawahi kuyafikiria madhara ya chuki inayoweza kuzaliwa baada ya muungano kuvunjika?. Busara za Mwalimu Nyerere bado zinaishi.
 
Huyo mhuni na Mropokaji atawapotosha hadi siku akili zinawaingia mtakuwa mnatoka Mirembe.
 
Inaonekana somo hili kwa Watanganyika hasa wale wa ccm ni gumu kwao.Mawazo fikirishi kwao yanayowatala ni masifu kwa viongozi.Hili jambo litatesa sana nchi yetu maana Watanganyika tumelala acha Wazanzibar wafaidi Muungano pamoja na viongozi wa ccm.
 
Kule kuungana peke yake ni faida kubwa, unajua kitu gani kinachompa jeuri Donald Trump mpaka anafukuza wamexico wakiwa na pingu miguuni na mikononi?, ni muungano wa majimbo yanayounda kitu kinachoitwa USA.
Nchi zinaungana kwasababu mahususi. Nchi zilizojaribu kuungana kwa maelezo yako hapo juu zimeishia pabaya. Tatizo si kuungana bali muundo wa Muungano unaofanya Zanzibar kuwa 'special''
Ni eneo linalowabebesha Watanganyika mzigo.

Mfano, Pesa za maendeleo kwa mkoa wa Dar es Salaam unaochangia 86% ya GDP ni ndogo kuliko zile zinazopelekwa Zanzibar! Kwanini Simiyu, Njombe au Geita ambayo ni mikoa michanga sana isipewe kipaumbele kama Zanzibar licha ya kuchangia Uchumi, Zanzibar ikichangia 0%.
Kumbuka kuwa kuna wapemba wameoa wandendeule wa kule Nyasa.
Kuna Waha wameoa Wamanyema wa DRC
Kumbuka kuwa kuna watumbatu wameoa waha wa Kigoma,
Kuna Watanzania wameoa Wakikuyu
Kumbuka kuwa kuna Wakerewe wameoa wakojani.
Kuna Wakurya wameoa Wamakonde
Hawa wote ndio nguvu kazi ya Taifa la JMT na ndio faida za kivitendo za uwepo wa muungano wetu.
Nguvu kazi haipatikani kwa kuoleana. Wazanzibar ni 1.5M , Watanganyika ni milioni 60. Ni upuuzi kudhani Muungano unasimamishwa na ndoa. Tumeoa Kenya, Musmbiji, na akina JUX wameoa Nigeria!
Umeshawahi kuyafikiria madhara ya chuki inayoweza kuzaliwa baada ya muungano kuvunjika?. Busara za Mwalimu Nyerere bado zinaishi.
Hakuna chuki! itoke wapi? Wazanzibar hawataki Muungano! waachwe warudi kuijenga Nchi yao kama ile ya Wakati wa Sultani. Wanataka iwe kama Dubai, wapewe fursa

Swali langu linabaki pale pale! Nje ya Muungano, Mtanganyika anapoteza nini! Ni swali tu
 
Kama haijabadilika sera ya CCM ni serikali mbili kuelekea moja. Hii iliwekwa hadharani lilipozuka kundi la G55. Sababu ya kuganda kwenye hatua ya serikali mbili hatuelezwi.

Labda ni mpango wa muda mrefu unaohusisha kubadilisha mchanganyiko wa wanaoishi Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…