I know, we see eye to eye on this. I was asking the confusion between you and whoever is failing to master the fundaments of the English language and the rudimentary logic of kindergarten comprehension reading.I don’t see where the confusion is [with you].
I’m not arguing with you about that.
Chige seems to be still confused, though.
Aisee umeandika makorokocho kibao mpaka yanaboa kusoma, yaani nakereka sana mtu anapopotosha vitu kwa makusudi au sio kwa makusudi lakini anijifanya anajua, kumbe hajui.Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi ya Taifa Na. 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 6(1) "basic tenure" ya CAG ni miaka mitano na sheria inasema anaweza (Shall) kutumikia vipindi viwili vya miaka mingine mitano.
CAG anaulinzi mkubwa kisheria na moja ya ulinzi wake ni kuwa akiwa katikati ya tenure yake hawezi kuondolewa hivi hivi bila masharti kadhaa kufuatwa, lazima utumie masharti ya Ibara ya 144(3) ya Katiba au yeye mwenyewe achukue hatua under subsestion 2 ya hiyo Sheria ya Ukaguzi niliyoitaja hapo juu. Lakini kwa ujumla anaweza kuondolewa, si ngumu. Nitaeleza.
View attachment 1253918
Matumizi ya neno "Shall" lililotumika katika Sheria ya Ukaguzi kwenye kifungu cha 6 .
Kwa heshima na taadhima, Sheria hapo haijakusudia ulazima na ndio maana sheria haifasiriwi kwa matakwa ya mtu bali sheria zenyewe zinavyokusudia kufasiriwa katika muktadha wa jambo husika na lengo la mtunga sheria.
Katika muradi wa sheria na taratibu za kiutawala (admimistrative law point of view) sheria zinajulikana kuwa zitajitafsiri zenyewe na msingi unaokubalika ni kuwa kila ambapo tenure inapomalizika na kuwepo kwa kanuni ya kuongezewa tena kipindi cha pili neno "Shall" halina maana kama ilivyo katika Sheria ya Kufasiri Sheria (The Interpretation of Laws Act), hapa maana huwa ya kimazingira zaidi (contextual meaning) na haiwi LAZIMA bali INAWEZA.
Na moja kwa moja ni kuwa kuongezewa kipindi cha pili Mtendaji yeyote mwenye vipindi viwili na hata Rais mwenyewe sio "automatic" lazima kuwe "subject to good performance."
Na anayeamua akuongezee tenure ya pili, hiyo sheria haijambana, ni yule yule mwenye mamlaka ya kuteua na kukutengua.
Rais anapewa mamlaka hayo kwa CAG na watendaji wengine Serikali aliowateua kwa sheria yoyote kwa mamlaka aliuonayo katika Ibara ya 36. Tena 36(3) ndio inampa mamlaka ya jumla zaidi ya kudeal na tatizo lolote kwa nia ya kuweka utulivu katika utumishi kwa kuweza kumtengua mtu yeyote aliyemteua.
View attachment 1253920
Ukifasiri neno "shall" katika Sheria ya Ukaguzi ili kumtetea CAG Assad kwamba ilikuwa lazima aendelee miaka mitano ya pili ni kuleta dhahama kubwa nchini inayoweza kushawishi hata Uchaguzi Mkuu wa Mwakani usifanyike. Najua utashangaa!!!
Ndio, tafsiri ya Zitto na wenzake ni ya hatari zaidi kwa nchi kwani ukisoma Ibara ya 40 ya Katiba inapozungumzia Rais aliyeko madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ya mwanzo kuwa anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano ya pili na ya mwisho neno lililotumika ni "shall."
View attachment 1253921
Kama tafsiri SISISI na "#shallow" ya ACT ni ya kufuatwa basi kwa muktadha wa neno "Shall" pia katika Ibara ya 40 ya Katiba, Rais Magufuli naye mwakani hakuna haja ya kupimwa utendaji wake kwa kurudi katika sanduku la kura, aendelee tu, kusiwe na uchaguzi, aapishwe moja kwa moja kuendelea na Urais maana "shall" ina maana ya LAZIMA.
Lakini hapana, muradi wa "shall" katika masuala ya utawala sio kama inavyotumika katika sheria za kawaida, hapa bado dhana ya mhusika kuwa "subjected to good performance" kwa kutazamwa utendaji wake kama unaridhisha mamlaka ya uteuzi (kwa kesi ya CAG) na kwa kurudi kuomba kura tena kwa wananchi (kwa kesi ya Rais) ndio utaratibu kabla ya kulamba awamu ya pili.
Kitaalamu ni kuwa CAG aliyemaliza muda wake hakuonewa na kama ni kuonewa au aliyemteua ana nia mbaya angeweza kuondolewa hata kabla hajamaliza miaka hii mitano.
Ibara ya 144(2) inampa madaraka Rais kumuondoa CAG kwa sababu ya utendaji mbovu, maradhi au sababu nyingine yoyote.
View attachment 1253922
Nimeona wengi wanasema Rais hawezi kufanya hivyo mpaka aunde Tume, si kweli. Watanzania tuachane na kasumba ya kutosoma kwa umakini.
Tuzisome sheria vyema na tunaposhindwa kuelewa tuwatafute wataalamu sio wanasiasa.
Katika Ibara ya 144(3) Rais ataunda Tume (If) kwa maana ya "kama" ataona kuchunguza sababu hizo za kumuondoa CAG kunafaa kuchunguzwa. Maana yake akijiridhisha hana haja ya kuunds Tume.
View attachment 1253923
Kisheria na Kikatiba, namsifu sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Magufuli na wataalamu wake wa sheria, hakika ni wabobezi, wanazisoma sheria zetu kwa utulivu na kuzifasiri kwa mujibu wa viapo vyao.
Naamini Rais Mhe. Dk Magufuli hakuwa na jambo baya la kutaka kumfukuza CAG isipokuwa "subject to good performance" anahitaji kasi zaidi katika eneo hilo na utulivu zaidi na kuaminika zaidi kwa kiongozi wa muhimili huo ambako Assad alishafeli kwa kufikia hatua ya kugombana na mhimili wa Bunge.
Kwa uchambuzi huu kudai Rais kavunja Sheria ni uchochezi mkubwa usiofaa kufumbiwa macho.
/chanzo Wakili wa Kujitegemea fb
Kama hapa hajaelewa hataelewa tena hata utumie maneno gani, safi hongera kwa ufafanuzi mzuri na rahisi.Kuna namna hizi za CAG kuondoka kwenye cheo hicho, katiba inaainisha.
Kwa vifungu ulivyovileta wewe mwenyewe, nimevinukuu hapo juu.
1. Kwa uchunguzi wa impeachment truibunal kama inavyosema article 144 (3)
2. Akifika umri wa miaka 65.
3. Akijiuzulu -i) kwa sababu za afya au nyingine zozote ambazo rais atazikubali au -ii) Kwa kumpa rais notisi ya miezi sita.
Hizi ndizo namna pekee zilizoainishwa kikatiba.
Sasa Assad.
1. Hajaundiwa impeachment tribunal
2. Hajafikisha umri wa miaka 65
3. Hajajiuzulu
Rais katumia kifungu gani cha katiba kumuondoa?
Chige mchokozi sana! Amefanya nimecheka kwa sauti alivyomjibu Nyani Ngabu!Hahahaaa........ Jf bhana hadi raha.
Ngabu anaamini kujua kizungu ndio kujua sheria......bure kabisa!
Hapo pia ni sawa tu na kule. Hapo kuna maneno mawili "eligible" na "election" Eligibility ya Rais inapatikana ibara ya 39, kwahiyo kama atakuwa na sifa neno Shall litatumika kwamba ni lazima uchaguzi ufanyike. Kama hana sifa hatoendelea na kugombea.Mkuu hiyo ni interpretation yako tu!
Na hii je?
40.-(1) Subject to the other provisions of this Article, any person who holds office as President shall be eligible for re-election to that office. (2) No person shall be elected more than twice to hold the office of President.
Dadavua SHALL pia hapa!!
Hapo pia ni sawa tu na kule. Hapo kuna maneno mawili "eligible" na "election" Eligibility ya Rais inapatikana ibara ya 39, kwahiyo kama atakuwa na sifa neno Shall litatumika kwamba ni lazima uchaguzi ufanyike. Kama hana sifa hatoendelea na kugombea.
The same pia kwa CAG, kuna maneno mawili "eligible" na "renewal". Eligibility ya CAG inapatikana ibara ya 144(3) kama sijakosea. Asiwe na zaidi ya miaka 60 ambapo Bunge limeongeza na kuwa 65, vipindi mwisho ni viwili vya miaka mitano mitano. Kama kuna hoja ya underperformance, katiba haijampa uhuru mteuzi kupima kwa jinsi atakavyoona inafaa. Anatakiwa kuunda tume ili kupitia ktk findings za tume hiyo ndipo afanye maamuzi. Kwahiyo eligibility ya CAG hivi ndivyo inavyopatikana.
Kwahiyo kama CAG yupo chini ya miaka 65, sio mgonjwa, amehudumu kipindi cha kwanza cha miaka mitano, hajaundiwa tume ya kumtuhumu kutokana na underperformance au misbehaviour au kuvunja maadili, CAG atakuwa "ELIGIBLE" kupewa kipindi cha pili cha miaka mitano mingine, hapo ndipo neno "Shall" linatumika. Kwamba ni lazima apewe mkataba mwingine.
Hakuna ibara kwenye Katiba inamlazimisha Rais kuunda Tume ibara ya 144(3) ni discretion yake kuunda ama la ndiyo maana inasema If the president considers ...... hapo hamlazimishi kuunda Tume mkuu!Hapo pia ni sawa tu na kule. Hapo kuna maneno mawili "eligible" na "election" Eligibility ya Rais inapatikana ibara ya 39, kwahiyo kama atakuwa na sifa neno Shall litatumika kwamba ni lazima uchaguzi ufanyike. Kama hana sifa hatoendelea na kugombea.
The same pia kwa CAG, kuna maneno mawili "eligible" na "renewal". Eligibility ya CAG inapatikana ibara ya 144(3) kama sijakosea. Asiwe na zaidi ya miaka 60 ambapo Bunge limeongeza na kuwa 65, vipindi mwisho ni viwili vya miaka mitano mitano. Kama kuna hoja ya underperformance, katiba haijampa uhuru mteuzi kupima kwa jinsi atakavyoona inafaa. Anatakiwa kuunda tume ili kupitia ktk findings za tume hiyo ndipo afanye maamuzi. Kwahiyo eligibility ya CAG hivi ndivyo inavyopatikana.
Kwahiyo kama CAG yupo chini ya miaka 65, sio mgonjwa, amehudumu kipindi cha kwanza cha miaka mitano, hajaundiwa tume ya kumtuhumu kutokana na underperformance au misbehaviour au kuvunja maadili, CAG atakuwa "ELIGIBLE" kupewa kipindi cha pili cha miaka mitano mingine, hapo ndipo neno "Shall" linatumika. Kwamba ni lazima apewe mkataba mwingine.
Hebu nipe tafsiri ya hiki kipengele na hiyo Article 4 inayoongelewa hapo kama unaifahamu.Hakuna ibara kwenye Katiba inamlazimisha Rais kuunda Tume ibara ya 144(3) ni discretion yake kuunda ama la ndiyo maana inasema If the president considers ...... hapo hamlazimishi kuunda Tume mkuu!
Chige mchokozi sana! Amefanya nimecheka kwa sauti alivyomjibu Nyani Ngabu!
ila kamwambia ukweli!
Nafahamu kwamba watu wengi wameanzisha threads wakijaribu kuelezea suala la CAG Kisheria! Hata hivyo, wengi wao kama sio wote walichofanya ni kurundika vifungu vya kisheria bila kutoa ufafanuzi!
Mbaya zaidi, hawatoi ufafanuzi wa matumizi ya neno SHALL kwa mujibu wa sheria zetu! Nimelazimika kuanzisha uzi huu ili kuondoa mapungufu yote hayo.
Tuendelee.
Bila kujaza vifungu vingi, Katiba yetu Ibara ya 144 (1) inasema wazi kwamba:-
Kwamba, CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 60 au umri mwingine wowote utakaotajwa na sheria zilizotengenezwa na Bunge!
SWALI 1: Je, Profesa Mussa Assad amefikisha miaka 60?! Jibu HAPANA kwa sababu kumbukumbu zinaonesha amezaliwa Oktoba 06, 1961... kwa maana nyingine, atafikisha miaka 60 Oktoba 5, 2021.
SWALI 2: Je, Bunge limetaja huo UMRI MWINGINE WOWOTE?!
Jibu linapatikana kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, yaani Public Audit Act ya mwaka 2008, Ibara ya 6(2)(a) inayosema:-
Kumbe, Bunge likatunga sheria kwamba badala ya miaka 60, hatimae CAG ATALAZIMIKA kuachia ofisi akifikisha miaka 65. Tumeona Prof Assad ndo kwanza ana miaka 58.
SWALI 3: Nini hutokea CAG akimaliza miaka 5 ya kwanza?!
Hapa tena jibu linapatikana kutoka Public Audit Act 2008 Ibara ya 6 (1) inayosema:-Hapo kwenye neno SHALL ndipo panapozua mgogoro!!
Watetezi wa uamuzi wa Rais wanasema neno SHALL sio shuruti! Kwa bahati mbaya sana, tafsiri yao wanaitoa kichwani na sio kwa mujibu wa sheria zetu!
Kwa mujibu wa sheria zetu, na kwa kuangalia Interpretation of Laws Act Ibara ya 53 (1&2) inasema kwamba:-
Kumbe, kwa mujibu wa sheria zetu, pasipo na SHURUTI hutumika neno MAY lakini linapotumika neno SHALL, hiyo ni SHURUTI!
Kwa maana nyingine, Public Audit Act inaposema "...and shall be eligible for renewal for one term only. Hapo suala la renewal ni SHURUTI kama ilivyosema Interpretation of Laws Act 53 (2).
Itakuwa sio SHURUTI either kama ameshafikisha miaka 65, au kama ambavyo 2008 Public Audit Act Ibara ya 6(2)(a) inavyosema kwamba:-Kwa maana nyingine, kwavile Prof Assad hajafikisha miaka 65, hapo tafsiri yake ni kwamba AMETUMBULIWA na sio kwamba muda wake umeisha!!
Na CAG atatumbuliwa "...Unless the question of removal becomes the subject of investigation in terms of Article 144(3) of the Constitution."
Hiyo Ibara ya 144(3) ya Katiba yetu inasemaje? Jibu ni hili:-If the President considers that the question of the removal of the Controller and Auditor-General from office under the provisions of this Article needs to be investigated, then the procedure shall be as follows:Kama tulivyoona hapo juu, CAG atalazimika kuachia ofisi endapo atakuwa amefikisha miaka 65, kinyume chake anaweza KUTUMBULIWA kabla ya huo umri ikiwa ametenda jambo linalohitaji investigation.
Hivyo basi, ni ama Rais atengue uamuzi wake wa awali wa kuteua CAG mwingine, au tuone akiunda Tume ya Kijaji ya Kumchunguza CAG kwa kosa analojua yeye na timu yake!!
CAG akiongezewa miaka mingine 5, ataimaliza akiwa na umri wa miaka 63... umri halali kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008!!
Weka vifungu tuvijadili hapa.The Constitution and The Public Audit Act, Pitia Ibara na vipengele husika kwa umakini utaona .
Akiweka uni tag chiefWeka vifungu tuvijadili hapa.
Mimi nineweka vifungu vya katiba vinavyoeleza namna CAG anavyoweza kuondolewa, weka vyako.
Sasa ni kwanini hafuati hiyo process iliyoandikwa kisheria iwapo ana nia ya kumtumbua??Uwezo wa kumtumbua kweli anao, ila sio anaamka tu anajisikia anatumbua, kuna process lazima afate imeandikwa kabisa, ataunde tume na watapata proof kua ni kweli CAG ana makosa then anatumbuliwa kisheria.