Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Lakini unamlinganishaje Prof. Assad kuendesha ist na Makonda aliyesema gari aina hiyo ni kuhongwa? Je, watu wamlaani Prof na kumfagilia makonda kuhusu mitazamo yao juu ya ist?

Kwa taarifa yako hakuna mtanzania anayedhani eti Prof hawezi kuwa na "kipando" chenye hadhi zaidi ya Toyota ist.
 
Kwa taarifa yako mleta mada hiyo ist bei yake ya soko iko juu kuliko lile benz jekundu alilokuwa akiliendesha enzi zile mlimani.
 
Soko la kimbiji.? Usije ukaongea hili jambo umekaa na watu wazima.

Kwa taarifa yako mleta mada hiyo ist bei yake ya soko iko juu kuliko lile benz jekundu alilokuwa akiliendesha enzi zile mlimani.
 
Mkuu nakuheshimu lakini hii post ingefaa Kule Facebook siyo hapa, hizi post za kujadili watu na matukio ni za watu wa chini sana
 
Toka Jumapili 03 Novemba tulipotangaziwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG ) amemaliza kipindi chake cha miaka mitano imeibuka mijadala kila eneo.

Naomba niulize kwa hapo ilipofikia iwe hajatimiza miaka (60) au amekatishwa mkataba kabla ya wakati wake, Au vinginevyo.... ni zipi Stahiki anazopaswa kupewa au kutopewa.
 
Unajuaje kwamba Profesa Assad anatumia IST kwa sababu ya kucheza na akili za Watanzania, na si kwamba anatumia IST kwa kutaka gari simple tu mwenyewe, au kwa kukagua mahesabu yake na kugundua IST inatumia mafuta vizuri kuliko Land Cruiser?


Hiyo habari ya kuchezea akili za Watanzania ni tuhuma kubwa.

Carl Sagan said "Extraordinary claims require extraordinary evidence".

Where is your evidence?
 
Kwani katiba inasemaje? Afuate sheria ya nssf.
 
It’s too personal Achana na hayo
 
Tanzania inatakiwa kustaafu wakat una umri gani

Ukipata jibu hili basi mafao ya huyo unae muuliza yapo au hayapo
 
(Anaandika Muheshimiwa mwenye heshima zake *Othman Masoud Othman* aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar) Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa FBI nchini Marekani, James Comey, ameandika katika kitabu chake A HIGHER LOYALTY maneno ya kuleta tafakuri kubwa. Amendika _“it is very hard to leave a group of people who are committed only to doing the right thing”

Alikuwa anaeleza ugumu wanaopata watu waadilifu katika utumishi wa umma kutenda mambo kwa kufata sheria na taratibu. Mara nyingi hujikuta wapo peke yao. Athari ya wanayokutana nayo ni kuzidisha hofu kwa wengine wenye ujasiri na hatimaye kuendelea kuporomoka kwa maadili ya utendaji wa umma.

Katika hili la CAG, imeonyesha wazi kwamba wanasheria katika ngazi mbali mbali hawakutimiza wajibu wao.
Ibara ya 144 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeeleza wazi kama ifuatavyo:

*_"144 (1) bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka siti au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge”_*

*_“(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake(ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya [4] ya ibara hii”_*

Ibara hiyo ya Katiba inaeleza wazi kwamba umri wa kuacha kazi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni miaka 60. Hata hivyo Bunge limepewa uwezo wa kubadili umri na sio muda wa kazi wa Mdhibiti na Mkaguzi. Ni kanuni ya msingi ya kutafsiri sheria kwamba neno linapokuwa na maana mahsusi, haliwezi kutaftiwa tafsiri nyengine mbadala inayopingana na maana mahsusi ya neno hilo. Ibara ya 144 (1) ilikusudia kuweka umri wa kustaafu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kama ulivyowekwa umri wa kustaafu wa Majaji chini ya ibara ya 110 ya Katiba ambao nao ni miaka 60.

Ibara ya 144 haitoi mwanya kwa Bunge kutunga Sheria ya kuweka muda wa kuendelea na kazi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ambao utamfanya aondolewe kazini kabla ya muda uliowekwa na Katiba au kuongezwa na Sheria [miaka 65].

Hili linathibitishwa zaidi na ibara ya 144 (6) ya Katiba inayosema:
*_“ Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano”_*

Kwa ibara hiyo, Profesa Musa Assad hawezi hata kukaimu nafasi yoyote katika utumishi wa umma, na hivyo atakuwa amestaafishwa katika utumishi wa umma kabla ya umri wa kustaafu. Hakuna kiumbe cha namna hiyo katika utumishi wa umma. Ikitokea hivyo, tafsiri sahihi ni kuwa mtu huyo amefukuzwa au kukatishwa utumishi wake. Na hilo, ni batili ya wazi kwa vile inakiuka masharti ya ibara ya 144(2) na (3) ya Katiba.

Sheria au tafsiri inayotoa mwanya kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuondolewa kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria na kwa matakwa ya Rais bila ya kufuata masharti ya wazi ya utaratibu wa kumuondoa kabla ya kufikiksha umri wa kustaafu chini ya ibara ya 144(3) na (4), inavunja msingi wa kinga ya kikatiba [security of tenure].
Inasikitisha sana unapoona wanasheria katika mazingira kama haya, ambapo kuna mgongano baina ya Katiba na Sheria, wanaanza kutafsiri Sheria kuipindua Katiba na sio kutafisiri Katiba ili kuipindua Sheria inayopingana na Katiba kama inavyoelekezwa na ibara ya 64(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mwanasheria yeyote aliyemshauri Rais kumuondoa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kutumia Sheria inayoweka masharti ya vipindi bila kuzingatia masharti ya wazi ya ibara ya 144(1) ya Katiba amemkosea sana Rais, amewakosea sana Watanzania na ameifedhehesha sana taaluma ya Sheria.

Fedheha kubwa zaidi kwa taaluma ya sheria ni pale wanasheria watapoanza kutofautiana katika kutafsiri masharti hayo ya wazi ya Katiba kwa itikadi au mirengo ya kisiasa au kwa baadhi kufanya hivyo kwa kupotosha ili kumfurahisha mteuzi.
Athari ya jambo hili haitokuwa kwa Profesa Mussa Assad. Athari kubwa ni katika mfumo wetu wa kikatiba, utawala wa sheria na matumizi ya mamlaka ya umma.
*OTHMAN MASOUD OTHMAN*
 
Nioneshe post inayojadili wanyama na bila kuwepo tukio. Ukinionesha ntaomba nipigwe ban maana nmekuja kwenye siasa nmejadili watu na matukio badala ya wanyama,ndege au wadudu.

Mkuu nakuheshimu lakini hii post ingefaa Kule Facebook siyo hapa, hizi post za kujadili watu na matukio ni za watu wa chini sana
 
Start with your evidence to support those two claims.

Kuwa anataka IST gari simple tu.

Kuwa kakagua mahesabu kaona IST inatumia mafuta vizuri kuliko land cruiser

Ukinipa hizo evidence nami nakupa zangu.haya anza kutoa.😁😁😁😁

 
Katiba imefanyiwa marekebesho na Raisi hivi sasa na itasema kuwa;

"HAKUNA ALIYEPEWA UWEZO WA KUTEUA AKANYIMWA WA KUTENGUA"

Kwa maana hiyo hata Chief Justice anaweza kutenguliwa tu.
 
Una washwa washwa sana ww, stahiki ni zake, ww inakuhusu nini? Kiherehere tu
Mleta nada kaleta swali la msingi, hapa Kuna mkanganyiko, sheria ya mafao inasema umri wa kustaafu Ni miaka 60, sheria ya cag inasema umri wa kustaafu Ni miaka 65, katiba inasema cag anapaswa kustaafu akiwa na miaka 60, Sasa sheria ipi itatumika kumlipa mafao? Sheria inasema akistaafu hapaswi kuajiriwa kokote Sasa atakula Nini?
 
Soko la kimbiji.? Usije ukaongea hili jambo umekaa na watu wazima.
Machizi wenzako wote hawana maarifa sioni haja ya kukujibu maana umepita kiwango kile cha machizi wanaotoa kinyesi chao chini na kuki recycle kwa kukirudisha mdomoni kwako mpaka ukayaona ni maarifa!!
 

Mawe ni mawe

Jamaa kuna kipindi litashitakiwa na kunyongwa hadharani!

Wait and see
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…