Sawa. Nadhani utaendelea kutokubaliana na kocha mwenzio Gomez hadi pale Simba itakapobadili mfumo wa ushambuliaji (itakapoanza kuwatumia washambuliaji wawili).
Bila kuathiri maoni yako, maoni yangu ni kwamba Kagere akichezeshwa kama mshambuliaji pekee pale mbele dhidi ya timu kubwa (achana na mechi dhidi ya hawa akina Ihefu na Gwambina), huwa anateseka sana. Anaonekana kama ''anakimbiakimbia huku na kule''.
Sisi sote tunaamini kwamba ni lazima kwanza mtengeneze nafasi kisha ndio mfunge (you first create chances then you score).
Kama Mugalu anao uwezo wa kukaa na mpira kisha akasubiri viungo wake wasogee (idadi ya wachezaji wa Simba kuongezeka katika shambulizi dhidi ya idadi ndogo ya walinzi, timu itatengeneza nafasi nyingi zaidi).
Timu ikitengeneza nafasi nyingi, hapa ndipo zinapatikana nafasi za ''kufunga'' na za ''kuchezea''. Mugalu ana enjoy kutapanya mali katika mazingira kma haya. Mugalu ni mtoto wa tajiri anayetupa chakula jalalani maana kipo kingi sana.
Ukimtumia Medie Kagere, asiyekua na uwezo niliousema hapo juu, maana yale ni kwamba timu itatengeneza nafasi chache sana kutokana na uchache wao katika shambulizi dhidi ya walinzi.
Kwa mantiki hiyo ni kwamba, hapa unataka kufunga goli bila kutengeneza nafasi. It is very rare in football.
Na ndio maana Kagere hapati nafasi za ''kutapanya mali'' kama mwenzie Mugalu.
Lakini pia kama timu haitengenezi nafasi, pia uwezekano wa kupata magoli kutoka kwa akina Chama, Luis na Bwalya unakua ni mdogo.
Kwahiyo kupanga ni kuchagua na wewe umeshafanya chaguo lako kwamba potelea mbali acha timu ikajaribu kufunga magoli ''bila kutengeneza nafasi'' lakini lazima Meddie Kagere acheze.
Kupanga ni kuchagua.
Gomez amechagua, wewe umechagua. Wote mko sahihi kwa utashi wa kila mmoja wenu.
Siku ya mechi ya mwisho kati ya Simba na AS Vita, Mugalu alikosa magoli hadi Kocha nilimwona akimkasirikia.
Ilivyo kosa goli la mwisho akambadilisha na kumwingiza Bwalya huku nafasi ya Mkude akamwingiza Nyoni.
Kabla ya hapo tulikuwa tunawaongoza goli 2 kwa 1 na huku tukiwa tunashambuliwa kila wakati wakitaka kurudisha goli.
Baada ya kumtoa huyo Mugalu wenu Simba ilishinda goli mbili za haraka haraka. Goli la tatu likifungwa na sub ya Mugalu, Bwalya. La nne Chama.
Hapa inaonekana wazi jinsi Mugalu alivyotugharimu na kutukaba siku hiyo maana angeendelea kubaki uwanjani huenda angeendelea kukosa nafasi muhimu za kufunga hivyo Vita kuweza kusawazisha na pengine kushinda.
Kocha sio kwamba anamtumia Mugalu kwa kuwa ni mzuri ila hana namna. Kegere kaisha makali, Boko ni majeruhi.
Wakati wa Kocha kishingo alikuwa anamtumia John Boko ambaye ni mzuri kupita Mugalu na Kagere. Huyo Mugalu alikuwa anakalia benchi tu na Simba ilikuwa inapata matokeo mazuri.
Ni kwamba sasa hivi Simba tumekosa mfungaji mahiri.
Hapa hatuzungumzii footwork wala kuhold mipira, wala fomesheni ya mpira.
Hapa tunazungumzia mshambuliaji mfungaji wa Magori.
Kwa ma mild field wa Simba akina Chama, Luiz, Kagata, Bwalya, Morrison nk, pale Simba namba tisa angesimama hata Papaa Morringa angefunga magoli ya kumwaga.
Leo hii mfungaji bora wa ligi yetu anatokea Azam FC, Prince Dube.
Huyo ndiye mfungaji.
Hii inaonesha wazi kuwa pamoja na ubora wake Simba bado haina mshambuliaji mahiri wa kufunga magoli.
Kocha Gomez kumtumia mtu haina maana ndiye anayefaa, ni kwamba kakosa mtu anayestahiri katika hiyo namba.
Mugalu uwezo wa kufunga magoli hana.
Hayo mambo ya kuhold mipira na kugawa kwa wengine ni mada nyingine. Sijawahi kusikia mshambuliaji anapewa tuzo ya kuhold mipira na kugawa kwa wengine.
Mwambieni Mugalu wenu sisi tunataka afunge magoli maana ndio mshambuliaji tegemeo kwa sasa.
Siamini kwamba alisajiriwa ili ahold mipira.
Awe siriaz uwanjani na sio kutafuna Big G kila wakati.