Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Swala la kuzikiwa Zanzibar au Bara ni la familia. Ni kweli mzee Mwinyi ameishi muda mrefu bara na hata kufikia hatua ya kutaka azikiwe kwao Mkuranga, ila ninachosema huenda familia yake ilikaa ikamshauri akubali kuzikiwa Zanzibar wanapoona alioa, kuzaa na kukulia huko. Lakini pia inaweza kuwa ni sababu za kisiasa zimechangia.

Hata hivyo mtu akifa amekufa haijalishi anazikiwa Tanzania, Ufaransa au Marekani. Kikubwa azikwe udongoni alipotokea. Maana tunaambiwa tulitoka mavumbini na tutarudia huko huko mavumbini ambapo ni popote kwenye mchanga au udongo.
 
Mwanaume hawezi kwenda kuzikwa alipoolea, hiki kitu hakipo.

Kama familia ilikaa ikaamua kufanya hivyo, basi watakuwa wamefanya hivyo kwa maslahi ya kisiasa ya mtoto wao, sijui ni kitu gani wameogopa mpaka kuamua hivyo.

Mambo ya kelele za kisiasa siku zote huja na kupita, hao wapinzani wake wangepiga kelele lakini mwisho wa siku hawana nguvu ya kumzidi mwenyekiti wa chama chao kama akiamua kufanya jambo lake.

Hilo la kusema mtu akifa amekufa anaweza kuzikwa popote, unaonesha ulivyo mchanga, mwanadamu sio mbuzi au kondoo, uliza waliokuzidi umri hapo ulipo wakupe sababu ya umuhimu wa mtu akifa kuzikwa kwao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Swadakta kabisa. Kila mtu anajifanya kukumbushia usia wa kuzikiwa Mkuranga utafikiri na wao ni watoto wa marehemu.
Wabongo wengi ni watu wa kupenda stories za kuungaunga.

Unaweza kufanya experiment kujitungia tu story ukapost, utashangaa kuna watu watajifanya wanaijua hiyo na kuongezea kabisaaa.

Familia ya Mwinyi ikikubali baba yao azikwe Zanzibar, wewe nani ubishe?

Maneno mengi kuhusu wosia ambao hata hatujauona, hatujausikia kutoka kwa marehemu, hatujui kama ni wa kweli au ni majungu ya kutungwa ya wabongo tu!
 
Mkuu Kwa heshima zote..
Naomba nikukosoe kuhusu Miaka ya Mwinyi aliyoishi Bara na zanzibar..
Alipoenda zanzibar alirudi mwaka 1962akiwa na umri wa miaka 37

Mwaka 1962 na akashika Vyeo vya Uwaziri na nyadhifa mbalimbali za chama na nchinikiwemo waziri wa mambo ya ndani,Waziri wa Elimu,Katibu mkuu elimu N.k

Alihamia Bara na Mwaka 1984 alikuwa Makamu wa Rais wa Tanzania na mwaka 1985 alichaguliwa na kuwa Rais wa 3 wa zanzibar..

Baada ya hapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania hivyo aliamua kujiuzuru urais wa zanzibar Na kuja kutumikia Urais wa Tanzania baada ya hapo hakuwahi kurudi tena zanzibar..

Kwa akili yangu na Hesabu za haraka bara amekaa kwa miaka 70 jumlisha na miaka aliyozaliwa mpaka kuomdola kwenda kusoma zanzibar akiwa na miaka 8...

na zanzibar kwa miaka 28 tu ...
 
Mkuu,

Wapo wanaume Watanzania ambao ni watu wanaooa Ulaya, Asia na Marekani wanaishi huko na kamua kuzikwa huko.

Itakuwa hapo Zanzibar tu hata huhitaji passport kwenda?
 
Nakubaliana na wewe kuwa huenda na siasa imechangia mno katika swala hilo.
 
Hata wakitaka kumzika kwenye makaburi ya Makkah sawatu wampeleke.
Kelele hizi naona hazina tija.

Kama ameacha wosia achomwe moto bado wapo watakaosema sio wosia alioacha.
Suala hilo nilakifamilia iachiwe familia
 
Hizi ni hisia zako sio ukweli
 
Hahaha ni kweli mkuu Kiranga
 
Hesabu tangu alipoanza kuwa waziri wa mambo ya ndani mpaka leo ambapo ameishi bara.
 
Hapa sio suala la maneno mengi yasiyo na msingi, ni suala la desturi zetu na kuzifuata. Kawaida desturi zetu inaonesha zinaenda kinyume na kile familia walichoamua.

Jiulize; vipi kama Dr. Mwinyi asingekuwa Rais wa Zanzibar leo, baba yake still angezikwa huko Zanzibar peke yake awaache ndugu zake wengine wazikwe Mkuranga? Jibu ni hapana.

Politics imeamua destiny ya Mzee Mwinyi kwa manufaa ya kisiasa ya mwanae.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu,

Wapo wanaume Watanzania ambao ni watu wanaooa Ulaya, Asia na Marekani wanaishi huko na kamua kuzikwa huko.

Itakuwa hapo Zanzibar tu hata huhitaji passport kwenda?
Wengi wanatakiwa wajifunze kupitia majibu yako. Shukran sana mkuu kwa kutoa darasa la bure kwa vijana.
 
Hizi ni hisia zako sio ukweli
Vipi wanaopinga Mwinyi kuzikwa Zanzibar huku wakidai kuwa mzee Mwinyi ali usia akifa azikwe Mkuranga. Wewe ushawahi kuuona au kuusikia huo usia wa Mkuranga kutoka katika kinywa cha Mwinyi mwenyewe?
 
Mkuu,

Wapo wanaume Watanzania ambao ni watu wanaooa Ulaya, Asia na Marekani wanaishi huko na kamua kuzikwa huko.

Itakuwa hapo Zanzibar tu hata huhitaji passport kwenda?
Hebu tutazame hili jambo kwa upana wake, issue hapa sio passport, hao watu wanaozikwa huko nje mostly hushindwa kurejeshwa nyumbani kuzikwa kwasababu za ukosefu wa kifedha, nyie diaspora huwa mnajichangisha mwisho wa siku mambo huwa magumu.

Lakini kwa Mzee Mwinyi, hakuna chochote walichokosa kushindwa kumzika Mzee Mkuranga walipozikwa ndugu zake wengine, kwenda kumzika Zanzibar ninaona kabisa hajatendewa haki, na sitaki kuamini kama yale yalikuwa maamuzi yake.

Jiulize, kwanini baada ya Mzee kufariki familia ikakaa kuamua wapi azikwe? kwani kwa kawaida hawajui mtu akifariki anatakiwa kuzikwa kwao? hizi ni siasa ndio zimeamua hatma ya Mzee Mwinyi (RIP) wala sio maamuzi binafsi ya marehemu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Usihofu, mtoto wa mzee MWINYI akiitwa HASSAN nae amezikwa Zanzibar, kwa hiyo hatakua mpweke.
Na kama kuna ulazima wa kupeleka udongo Mkuranga utapelekwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…