Naona hautaki kulundikwa kwenye desturi zetu, mindset ya kimarekani imekuingia unaanza kuzikataa mila na desturi zako, hata kama huzitaki, wazazi wako wanazifuata, hiyo ndio sababu iliyonifanya nikachagua kutumia neno "zetu" nikimaanisha waswahili, sio wakina wewe "swahili-zungu".
Hapa pia kuna angle ya pili niiite social status.
Mzee Mwinyi alikuwa mtu mzito hapa Tanzania -Rais Mstaafu, hivyo kwangu sioni ubaya yeye kujadiliwa, hata nawe huwa unakuwa kwenye upande wa kuunga mkono mtu mwenye nafasi kwenye jamii kuzungumziwa, nikikumbuka umekuwa ukilaumu taarifa za viongozi wagonjwa kwenda nje kutibiwa kufanywa siri na serikali.
Sasa sijui kwanini hapa kwa marehemu Mzee Mwinyi umeamua kugeuka kuwa mtu wa kutaka "ushahidi wa vikao vya kifamilia", kwanini wakati ule wa ugonjwa wa viongozi huwa huulizii ushahidi wa ugonjwa wa kiongozi toka kwa familia yake kwanza, badala yake huishia tu kuitaka serikali isitufiche habari zao?
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app