Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Mfano uliotoa hauufanani kabisa na suala la Mzee Mwinyi.
Kwa nini haufanani?

Kwanza kabisa, sijajibu suala la Mzee Mwinyi, nimejibu suala la mwanamme hazikwi alikooa.

Pili,

Kwa muktadha wa kukataa mwanamme kuzikwa sehemu aliyooa, wewe ni nani uamue mtu mwingine azikwe wapi? Unajipa vipi mamlaka ya kumuamlia mtu mwingine sehemu ya kuzikwa?
 
Kuhusudu sana mila na desturi ni ujinga.

Mwinyi angehusudu sana mila na desturi, angebaki kijijini kwao, asingeenda hata Zanzibar, na tusingempata huyu Ali Hassan Mwinyi wa leo.

Wapo wenzake wengi sana walioheshimu mila na desturi hata shule za elimu dunia wamekataa kwenda. Wameishia kufulia.

Wakati wakoloni wanaanzisha mifumo ya elimu, walipita kuchukua watoto wa machifu wakasome. Chifu Mazengo wa Ugogo alikataa watoto wake kuchukuliwa wakasome. Jirani yake Chief Mazengo alikuwa baba yao kina John Malecela na Job Lusinde, yeye alikuwa na muamko kidogo wa kutaka elimu, akakubali watoto wake kina John Malecela na Job Lusinde waende kusoma.

Matokeo yake, mtu aliyeheshimu mila na desturi Chief Mazengo, kawakosesha fursa ya kuwa viongozi watoto wake, kwa sababu hawakupata elimu, mtu ambaye alisema hizi mila na desturi zipo lakini inabidi tujiongeze, Mzee Malecela, watoto wake kina John Malecela na Job Lusinde wameenda kuongoza nchi.

So kuangalia mila na desturi bila ku focus kwenye kuangalia mbele na ku shape mila na desturi mpya zinazofaa zaidi kwa dunia ya kesho ni ulofa, ni ujinga tu kama alioufanya Chief Mazengo wa kukataa shule.

Kuhusu kujadiliwa.

Kwani wapi nimekataa Mzee Mwinyi kijadiliwa?

Unajua kuna tofauti kati ya kukataa Mwinyi kujadiliwa na kukataa Mwinyi kujadiliwa kwa hadithi za uzushi zisizo na chembe ya ushahidi?
Kuhusudu mila na desturi sio ujinga, na wala sio kweli wanaofuata mila na desturi huishia kufulia, naona wewe ndie unaishi kwa kukariri.

Kuhusu Mzee Mwinyi kujadliwa ni kujadiliwa tu, iwe kwa story zenye ushahidi au zisizo na ushahidi, hiyo yote ndio mijadala yenyewe, usitufunge midomo.

Kama hupendi story za uzushi kwanini wewe huitaka serikali ikwambie wapi walipolazwa viongozi wetu, ikiwa wewe hujui lini waliondoka nchini na ugonjwa upi unaowasumbua?

Kwanini usiitake serikali kwanza ikupe ushahidi wa ugonjwa wao, ili uanze kutaka kujua wapi walipoenda kulazwa viongozi wetu?

Hujioni nawe kutaka kujua wapi walipolazwa viongozi wetu, bila kujua kwanza ugonjwa wao nawe ni miongoni mwetu wanaopenda uzushi wa vijiweni?

Kaa chini tafakari.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kuhusudu mila na desturi sio ujinga, na wala sio kweli wanaofuata mila na desturi huishia kufulia, naona wewe ndie unaishi kwa kukariri.

Kuhusu Mzee Mwinyi kujadliwa ni kujadiliwa tu, iwe kwa story zenye ushahidi au zisizo na ushahidi, hiyo yote ni mijadala.

Kama hupendi story za uzushi kwanini huitaka serikali ikwambie wapi walipolazwa viongozi wetu, ikiwa hujui lini waliondoka nchini na ugonjwa upi unaowasumbua?

Kwanini usiitake serikali kwanza ikupe ushahidi wa ugonjwa wao, ili uanze kutaka kujua wapi walipoenda kulazwa viongozi wetu? Hujioni nawe kutaka kujua wapi walipolazwa viongozi wetu, bila kujua kwanza ugonjwa wao nawe ni miongoni mwetu wanaopenda uzushi?

Kaa chini tafakari.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mila na desturi hazisimami, zinaendelea kila siku. Na unajuaje kama Mwinyi, kiongozi aliyeweka rekodi ya kuzaliwa bara na kuwa rais visiwani, katuanzishia mila na desturi mpya ya kuzaliwa bara na kuzikwa Zanzibar ili kuudumisha zaidi Muungano?

Kuna tofauti kati ya kujadiliwa na uzushi, hizo habari za wosia wa Mwinyi ni uzushi tu, hakuna mtu mwenye ushahidi wa wosia huo.

Unaniuliza "kama hupendi story za uzushi kwa nini..." ina maana wewe unapenda stories za uzushi na unatetea kupenda kwako stories za uzushi?
 
Huwezi kulitenga suala hili na siasa hasa siasa za Zanzibar
Kuzikwa popote siyo tatizo, hata Raza aliyeuchukia Muungano alizikwa Kisutu.

Unguja wangependa azikwe huko kwasababu ni mwana Mapinduzi na itaondoa hoja za Wapemba
Mwinyi alikubalika Zanzibar kwasababu ilikuwa timu ya Kombo Thabiti , watu wa Mapinduzi

Kwasiasa za ubaguzi, wapo wanaoamini Mwinyi na waliotoka Bara kama VP Seif Idd si Wazanzibar.

Rais Hussein Mwinyi anakutana na wakati mgumu sana akisemwa si ''Mzanzibar halisi'' , anapigwa vita hata ''Shangazi' amewahi kulisema.

Kwa kutambua hilo kwa maoni yangu Familia iliamua azikwe Zanzibar ili kujenga msingi wa vizazi vijavyo kwamba ni Wazanzibar! Siasa ipo ndani ya hili

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Mila na desturi hazisimami, zinaendelea kila siku. Na unajuaje kama Mwinyi, kiongozi aliyeweka rekodi ya kuzaliwa bara na kuwa rais visiwani, katuanzishia mila na desturi mpya ya kuzaliwa bara na kuzikwa Zanzibar ili kuudumisha zaidi Muungano?

Kuna tofauti kati ya kujadiliwa na uzushi, hizo habari za wosia wa Mwinyi ni uzushi tu, hakuna mtu mwenye ushahidi wa wosia huo.

Unaniuliza "kama hupendi story za uzushi kwa nini..." ina maana wewe unapenda stories za uzushi na unatetea kupenda kwako stories za uzushi?
Suala la kuzaliwa hapa na kuzikwa pale sio la kimuungano, wala sio la kisiasa, hata Magufuli aliwahi kupinga kuzikwa Dodoma akifariki, ni suala la mila na desturi zetu unazoziita ni ujinga hutaki kuzifuata.

So, kwangu naona kuleta habari ya kuzaliwa hapa na kwenda kuzikwa kule ili kukuza muungano ndio ujinga wenyewe, kwani huko Zanzibar hakuna waliozaliwa na kuishi huko? kama wapo kwanini wakifariki wasizikwe kwao walipozaliwa?!

Unaonekana hujui hata tetesi wewe unaita uzushi ni chanzo kimojawapo cha habari, hapo ndipo huwasukuma waandishi wanaojielewa kuanza kuchimba kuutafuta ukweli, kuzikataa tetesi/uzushi kama unavyoita, ni kujinyima haki yako ya kupata habari.

Ndio mimi stories za uzushi nazipenda kwasababu zina expand my brain muscles, zinaifanya akili yangu itanuke, napata wasaa wa ku- connect dots, sipendi kuwa na lazy mind ya kusubiri ushahidi wa kila jambo kama vile niko mahakamani.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.

Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.

Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?

Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.

Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.

Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.
Mwinyi kajenga msikiti kisalawe na alikuwa akiwa dar ijumaa anasali kisarawe.aidha usia wake aliandika azikwe kisarawe na hadi barabara zilichongwa wakawaza madhara ya hilo
 
Babu Duni wa ACT moja ya mikutano yake alimwiita mzee Mwinyi "MZARAMO" na si Mzanzibari, alitakiwa kuzikwa makaburi ya Kinondoni!!!!
 
Suala la kuzaliwa hapa na kuzikwa pale sio la kimuungano, wala sio la kisiasa, hata Magufuli aliwahi kupinga kuzikwa Dodoma akifariki, ni suala la mila na desturi zetu unazoziita ni ujinga hutaki kuzifuata.

So kwangu naona kuleta habari ya kuzaliwa hapa na kwenda kuzikwa kule ili kukuza muungano ndio ujinga wenyewe, kwani huko Zanzibar hakuna waliozaliwa na kuishi huko? kama wapo kwanini wasizikwe kwao walipozaliwa?!

Unaonekana hujui hata tetesi wewe unaita uzushi ni chanzo kimojawapo cha habari, hapo ndipo huwasukuma waandishi wanaojielewa kuanza kuchimba kuutafuta ukweli, kuzikataa tetesi/uzushi kama unavyoita ni kujinyima haki yako ya kupata habari.

Ndio mimi stories za uzushi nazipenda kwasababu zina expand my brain muscles, zinaifanya akili yangu itanuke, napata wasaa wa ku- connect dots, sipendi kuwa na lazy mund ya jusubiri ushahidi wa kila jambo kama vile niko mahakamani.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
1. Huna ushahidi wowote kuhusu wosia wa Mwinyi. Habari zozote kuhusu wosia huu ni uzushi tu.
2. Suala la mazishi ya Mwinyi ni maamuzi ya familia, wewe ni mtu wa familia?
3. Uki support stories za uzushi zisizo na ushahidi, ume support chaos, mimi naweza kuanzisha uzushi kwamba wewe ni mpinzani wa kisiasa wa familia ya Mwinyi unaleta uzushi ili ukufaidishe kisiasa tu. Tukaanza kubishana uzushi juu ya uzushi mpaka maongezi yakwa hayana maana.
 
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.

Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.

Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?

Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.

Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.

Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.

Ngoswe kaokotwa wapi?
 
1. Huna ushahidi wowote kuhusu wosia wa Mwinyi.
2. Suala la mazishi ya Mwinyi ni maamuzi ya familia, wewe ni mtu wa familia?
3. Uki support stories za uzushi zisizo na ushahidi, ume support chaos, mimi naweza kuanzisha uzushi kwamba wewe ni mpinzani wa kisiasa wa familia ya Mwinyi unaleta uzushi ili ukufaidishe kisiasa tu. Tukaanza kubishana uzushi juu ya uzushi mpaka maongezi yakwa hayana maana.
Nimeshakuonesha umuhimu wa unachokiita uzushi kwenye jamii, yapo mambo mengi huanza kama uzushi lakini baadae huthibitika kuwa uzushi ule ulikuwa ni kweli, amsha akili.

Hata kama suala la mazishi ya Mzee Mwinyi ni maamuzi ya kifamilia, lakini Mzee Mwinyi kuwahi kuwa kiongozi wa kitaifa kunatufanya na wengine tujadili sababu za maziko yake kuwa Zanzibar, kama hakupenda kujadiliwa angeacha kuwa kiongozi wa kitaifa hakuna ambaye angehaika nae leo.

Mimi nina support stories unazoita za uzushi ili kuwasukuma waandishi wetu wa habari wakachimbe kuutafuta ukweli, suala la "chaos za kisiasa" ni maoni yako binafsi, siwezi kuyapinga.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nimeshakuonesha umuhimu wa unachokiita uzushi kwenye jamii, yapo mambo mengi huanza kama uzushi baadae huthibitika kuwa uzushi ule ulikuwa ni kweli, amsha akili.

Hata kama suala la mazishi ya Mzee Mwinyi ni maamuzi ya kifamilia, lakini Mzee Mwinyi kuwahi kuwa kiongozi wa kitaifa kunatufanya na wengine tujadili sababu za maziko yake kuwa Zanzibar, kama hakupenda kujadiliwa angeacha kuwa kiongozi wa kitaifa hakuna ambaye angehaika nae leo.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Huo uzushi wako hauna hata muelekeo wa kuwa kweli. Kwa sababu hakuna logical inconsistency yoyote Mwinyi kuamua kuzikwa Zanzibar.

Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, sehemu ambayo Mwinyi kasoma, kaishi, kalowea, mpaka kawa rais, mbona unafanya kama vile Mwinyi kaenda kuzikwa Misri?
 
".... Hauna hata muelekeo wa kuwa kweli" naona unajigeuza mtabiri sasa, kwani hii nayo ni fani yako? kama sio basi tuache muda uamue.

Mzee Mwinyi hata kama angezikwa Misri nisingeshangaa chochote kama asingekuwa "political figure", na ndio maana hata wewe umesema kule juu ukifa utazikwa Marekani, sikushangaa chochote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
"....Hauna hata muelekeo wa kuwa kweli" naona unajigeuza mtabiri sasa, kwani hii nato ni fani yako?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hiyo kauli sikuiandika kwa urahisi, nilivyoiandika, nikajirudi na kutaka kuipatia justification.Nimekupa sababu ya kuandika hivyo.

Hujaiweka sababu hiyo hapa tuichambue.

Ama kwa sababu uelewa wako ni mdogo sana hukuweza kuielewa, ama kwa sababu umeielewa huna nia ya kuichambua kwa sababu itakupa mzigo wa kuthibitisha mambo ambayo huwezi kuthibitisha.

Sasa, wewe uko kundi gani?

Mjinga sana hujaelewa au muongmuongo tu umeelewa lakini unataka kukwepa mazungumzo ya mantiki?
 
Kwani wewe hiyo statement "hauna muelekeo wa kuwa kweli" umeiona kwa kutumia kipimo gani? kilichothibitishwa wapi?

Kama ni fikra zako, basi tuliza hicho kichwa, fikra zako sio kipimo cha kuthibitisha mambo hapa ulimwenguni, wewe ni mwanadamu tu, kama nilivyo mimi, na wengine ...

Hatuko complete kila wakati kifikra, mara nyingine hukosea pia, hata kama mwanzo hujiona tuko sahihi.

Back
Top Bottom