Suala la timu ya USM Alger kuja na Maji na vyakula linafikirisha sana

Suala la timu ya USM Alger kuja na Maji na vyakula linafikirisha sana

Juzi tumeona kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha timu ya USM Alger ikiwasili JK Nyerere International Airport ikiwa na shehena ya Maji ya kunywa na pia inasemekana walibeba na vyakula vyao.

Huenda wakawa na nia njema ya kuhakikisha usalama wao na kuepuka hujuma za kimichezo lakini pia kwa upande mwingine wanaweza kutumia fursa hiyo kuingiza vimiminika kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa wachezaji wao ambapo unaweza kukuta mchezaji mwanzo mwisho yupo na energy ile ile au mara dufu.

Inavyoonekana vinywaji hivyo wameingia navyo siku hiyohiyo ambapo ukifuatilia sidhani kama mamlaka husika kama TFDA, TBS nk zilikuwa na muda wa kufanya ukaguzi wa kina.

Nadhani mambo kama haya vyombo vyetu vya Usalama including SSIT kwenda mbali zaidi.
Sidhani kama hayo mambo ya dopping yafanyika na kuwa na effect kwa muda mfupi kiasi hicho.
Anabolic steroids ni process na inachukua muda kupata matokeo sio overnight procedure
 
Sasa kama hivyo vyakula na maji yao wanaingia nayo bila kukukaguliwa na kupimwa wanaweza wakaingia na dawa za kulevya tukadhani ni vyakula tu vya kuliwa kumbe kuna vingine vya siri zao
Aliyekwambia hawakukaguliwa ni nani?
 
Naona hao USM Alger wamecomplicate tu hiyo issue, dunia imebadilika, hakuna sababu ya kuja na vyakula wala maji, vyakula na maji vilivyopo hapa Tz ni sawa tu na huko kwao na huenda vya hapa kwetu vikawa na ubora kwa kuwa vitakuwa more fresh.

Wajikite kucheza mpira na sio hivyo vitu vidogo.

Sidhani kama ishu ni ubora, wameangalia usalama zaidi, kukwepa figisu na hujuma kwenye soka
 
Back
Top Bottom