Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Mwezi mzima huu vyombo vya habari hakuna hata kimoja kilichoandika habari ya usajili wa mchezaji Clatous Chota Chama kwa usahihi, sio vyombo vya habari vya michezo, sio mitandao ya kijamii na wala sio wachambuzi au wachang'ombe feki hapa nchini.
Hebu fikiria ndipo uone kuwa vyombo vya habari vya michezo nchini vimeishiwa kabisa udadisi, mchezaji Chama kwako wala sio mbali, kwao ni hapo Zambia, ukifika Tunduma Zambia unaiona ileee.
Huko miaka ya nyuma sisi tuliowahi kufanya kazi enzi hizo The Guardian ni kampuni kubwa, habari hii kama hii kwetu sisi walaji haikuwa shida, zamani chombo vya habari katika kutafuta ukweli kiliweza kutuma mwandishi nguli aende Zambia kufuatilia ukweli wa habari ya usajili wa Chama.
Kule mwandishi angeweza kwenda kuonana na Chama mwenyewe, angeweza kumsaka babake au hata ndugu zake ambao kifamilia suala hilo wanalijua, wao wangeweza kusema Chama atakuwa upande gani msimu ujao.
Lakini hakuna, kila siku wanabahatisha t, leo wanaandika hivi na kesho wanabadilisha vile, magazeti yamekuwa ya hovyo kabisa.Habari zimejaa uongo, ushabiki, unafiki na uchonganishi mtupu.
Ndio maana magazeti yanakufa nchini.