Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tetesi za chama wiki nzima ndio nini? Tena anasajiliwa yanga misimu iliyopita anachezea Simba.Tetesi za usajili zipo duniani kote.Hata vyombo vikubwa duniani kama bbc huandika tetesi za usajili na wakati mwingine uhalisia huwa kinyume na tetesi zao.
Kabla sijaendelea,unajua maana ya tetesi?
Ndio iko hivyoKivipi?
Haya! Ngoja basi nikipunguzie presha. Maana tunaweza tukakupoteza hivi hivi!Mwezi mzima huu vyombo vya habari hakuna hata kimoja kilichoandika habari ya usajili wa mchezaji Clatous Chota Chama kwa usahihi, sio vyombo vya habari vya michezo, sio mitandao ya kijamii na wala sio wachambuzi au wachang'ombe feki hapa nchini.
Hebu fikiria ndipo uone kuwa vyombo vya habari vya michezo nchini vimeishiwa kabisa udadisi, mchezaji Chama kwako wala sio mbali, kwao ni hapo Zambia, ukifika Tunduma Zambia unaiona ileee.
Huko miaka ya nyuma sisi tuliowahi kufanya kazi enzi hizo The Guardian ni kampuni kubwa, habari hii kama hii kwetu sisi walaji haikuwa shida, zamani chombo vya habari katika kutafuta ukweli kiliweza kutuma mwandishi nguli aende Zambia kufuatilia ukweli wa habari ya usajili wa Chama.
Kule mwandishi angeweza kwenda kuonana na Chama mwenyewe, angeweza kumsaka babake au hata ndugu zake ambao kifamilia suala hilo wanalijua, wao wangeweza kusema Chama atakuwa upande gani msimu ujao.
Lakini hakuna, kila siku wanabahatisha t, leo wanaandika hivi na kesho wanabadilisha vile, magazeti yamekuwa ya hovyo kabisa.Habari zimejaa uongo, ushabiki, unafiki na uchonganishi mtupu.
Ndio maana magazeti yanakufa nchini.
Comrade, huyo aliyeingilia kati kwenye lile suala la Dogo Fei alikuwa ni huyu binti kiziwi ninayemfahamu, au ni CHURA KIZIWI?Umepitwa sana mkuu. Siku hizi hata baba au mama mzazi wa mchezaji profeshno kama chama atakwambia mfate meneja wake. Unafikiri chama ni dizaini ya wachezaji wa kuokoteza kama feitoto ambapo mama ake anasema hiki, fei analia kivile, mjomba anagugumia huku, Yani mpaka Binti kiziwi aingilie kati ndio auzwe.
Hahah nimepata ndugu anaitwa Chura kiziwi eeenhe? 😅Comrade, huyo aliyeingilia kati kwenye lile suala la Dogo Fei alikuwa ni huyu binti kiziwi ninayemfahamu, au ni CHURA KIZIWI?
Nilitamani nimuulize hivyo, ila baadae nikagundua huyo ni mbumbumbu hajawahi kuwa na akili.Mbona hujahitimisha kuwa Chama kasajiliwa wapi? Kaongeza mkataba Simba au kasajiliwa Yanga? Sasa umeponda vyombo vya habari za michezo halafu swala la msingi umeliacha kulikoni?
Binti chura yule wa kwenye hadithi za bi Debora mwenda rtd wakati nilipokiwa kid 😅Comrade, huyo aliyeingilia kati kwenye lile suala la Dogo Fei alikuwa ni huyu binti kiziwi ninayemfahamu, au ni CHURA KIZIWI?