Mkuu sio jamii zote ndo hufanya hivyo.Mkuu misiba ya kwetu waafrika inajiendesha yenyewe.
We ni kutangaza tu kwamba umefiwa.
Tatizo pale wewe usipohudhuria misiba ya wengine katika jamii.
Wakati mkikamilisha mafunzo ya kiimani hasa wakatoliki huwa mnaambiwaga mkristo ana sherehe tatu. Kuzaliwa (kubatizwa), Kuoa na kufa. Sasa sielewi kwamba somo la baba paroko hukulielewa au umeamua kukaza ubongo tu?Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.
Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.
Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.
Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.
Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.
Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.
Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula
Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.
Wanaopika sio wafiwa wa karibu, ni majirani na ndugu wa mbali wa waliofiwa. Sasa mwambie mkeo siku nyingine akienda msibani kwa jirani akasaidie kupika, sio anakaa tu mkao wa kusubiri ahudumiwe ubwabwa wa msibaniSuala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.
Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.
Hahahah uzito wa Bufee kwenye shughuli hata Hashim Rungwe Spunda anauelewa!Bila bufee hatujui hata msibani
Hahahahah wahuni sio watu kmmmk 😅😅😂😂😂Hata msiba uwe mzito niaje ila msosi lazima upikwe!
Aisee nimecheka kinoma na huu uzi 😂😂😂😂😂😂Halafu kuna mijitu inashinda msibani kuanzia asubuhi hadi usiku yupo tu na anakula chakula bila kuchangia hata senti eti anamfariji mfiwa, wengine wanalalamika msibani unakuta nyumba imejaa watu wanalala sebuleni, vyumbani hadi nje.
Ni utaratibu wa kipuuzi sana, wanatakiwa wabaki watu wachache wa karibu wasiozidi kumi.
Hahahahah hio ilikuwa Yombo huko huko au ulikuwa ujahama Mikocheni 😂?Jirani yetu kijana wao alifia Ughaibuni, mipango ya kusafirisha mwili ilichukua kama wiki mbili. Katika zile wikimbili masharobaro wote mtaani waliakua wanapata chai na maandazi pale msibani, wakishafungua kinywa wanakwenda kwenye mishe zao, mchana wana wahi msosi na jioni.
Uzuri ni kwamba hata wewe ukifa tutakula Pilau nyama kwenye masinia na Soda juu hata kama hutaki! Na tutakufukia futi 6 kama kawaida. Huo ndio mwisho wetu sote hamna atakaekwepa wala kuweka ngumu.Anaetoa rambirambi ni nani na anaekuja kuzika ni nani ?
Tuachane na anaetoa rambirambi alafu siku ya kuzika haji,huyu katoa.Naweza kuja kutoa rambi rambi na siku ya kuzika au muda wa kuzika nisiwepo, na mwingine anaweza kutoa rambi rambi na siku ya kuzika au muda wa kuzika akahudhuria
Kwa akili yangu nisingekubaliana na maneno ya paroko kwa sababu kufa sio jambo la kufurahia kwa wafiwa.Wakati mkikamilisha mafunzo ya kiimani hasa wakatoliki huwa mnaambiwaga mkristo ana sherehe tatu. Kuzaliwa (kubatizwa), Kuoa na kufa. Sasa sielewi kwamba somo la baba paroko hukulielewa au umeamua kukaza ubongo tu?
Definition ya Sherehe; ni tafrija fupi inayohusisha kula na kunywa.
Kuna watu misibani zao ni kuangalia wasiokula.
Hapo tatizo ni huyo mchonganishi na wala sio wewe tatizo.
Hivyo aache uchonganishi tu
Sawa nitamuambia.Wanaopika sio wafiwa wa karibu, ni majirani na ndugu wa mbali wa waliofiwa. Sasa mwambie mkeo siku nyingine akienda msibani kwa jirani akasaidie kupika, sio anakaa tu mkao wa kusubiri ahudumiwe ubwabwa wa msibani
Kwahiyo kila comment lazima nisijibu pia ?
Mimi sijajibu.Jibu zinazohitaji jibu.