Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Mkuu misiba ya kwetu waafrika inajiendesha yenyewe.
We ni kutangaza tu kwamba umefiwa.
Tatizo pale wewe usipohudhuria misiba ya wengine katika jamii.
Mkuu sio jamii zote ndo hufanya hivyo.

Mimi ni muafrika pia na katika jamii ninayotoka mmkuu watu wengi wakifiwa basi gharama za chakula wanagaramia wafiwa,hawa waliokuja kuzika kazi yao ni kupika tu.

Ipa kama wazikaji wanakuja na vyakula vyao mbona haina tatizo kabisa,ishu ni wafiwa kutupiwa mzigo wa chakula mkuu.
 
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.

Wale wanaokuja kukupa pole na kuzika ndo wakupe chakula cha wewe kula kwa sababu umepatwa na msiba,umeshughulishwa na kuondoka kipenzi chako halafu inakuwaje uwaze kuwapikia wanaokuja kuzika, hiyo sio sherehe.

Mtu anatoka nyumba ya pili tu hapo halafu anataka kuja kula kwako uliyefiwa haoni haya kabisa.

Nilishatangaza nyumbani kuwa nikifiwa na mtu aliyeko ndani ya mamlaka yangu chakula ni kwa ajili ya familia tu kama kawaida na wale wageni wa mbali ambao hata bila msiba wangepikiwa na sio vinginevyo.

Ndugu wengi wakimaliza maziko wanabaki na madeni yasiyo ya lazima kwa sababu ya kutimiza utaratibu waliokuta katika jamii licha ya kuwa unawaumiza utaratibu huo lakini wamo tu.

Mfiwa kupika chakula ni sawa na mwenye sherehe kupika chakula

Kama kweli wameguswa na msiba wako wao ndio wakuletee chakula wewe uliyefiwa.
Wakati mkikamilisha mafunzo ya kiimani hasa wakatoliki huwa mnaambiwaga mkristo ana sherehe tatu. Kuzaliwa (kubatizwa), Kuoa na kufa. Sasa sielewi kwamba somo la baba paroko hukulielewa au umeamua kukaza ubongo tu?

Definition ya Sherehe; ni tafrija fupi inayohusisha kula na kunywa.
 
Suala hili lipigwe vita vikali sana kwa sababu ni sherehe tu ndio inayo namna ya kupika ili waliokuja kwenye hiyo shughuli wapate kula.

Haiwezekani umefiwa na kipenzi chako halafu hapo hapo unawapikia wanaokuja kumzika wale washibe waende zao.
Wanaopika sio wafiwa wa karibu, ni majirani na ndugu wa mbali wa waliofiwa. Sasa mwambie mkeo siku nyingine akienda msibani kwa jirani akasaidie kupika, sio anakaa tu mkao wa kusubiri ahudumiwe ubwabwa wa msibani
 
Halafu kuna mijitu inashinda msibani kuanzia asubuhi hadi usiku yupo tu na anakula chakula bila kuchangia hata senti eti anamfariji mfiwa, wengine wanalalamika msibani unakuta nyumba imejaa watu wanalala sebuleni, vyumbani hadi nje.
Ni utaratibu wa kipuuzi sana, wanatakiwa wabaki watu wachache wa karibu wasiozidi kumi.
Aisee nimecheka kinoma na huu uzi 😂😂😂😂😂😂
 
Jirani yetu kijana wao alifia Ughaibuni, mipango ya kusafirisha mwili ilichukua kama wiki mbili. Katika zile wikimbili masharobaro wote mtaani waliakua wanapata chai na maandazi pale msibani, wakishafungua kinywa wanakwenda kwenye mishe zao, mchana wana wahi msosi na jioni.
Hahahahah hio ilikuwa Yombo huko huko au ulikuwa ujahama Mikocheni 😂?
 
uzu
Anaetoa rambirambi ni nani na anaekuja kuzika ni nani ?
Uzuri ni kwamba hata wewe ukifa tutakula Pilau nyama kwenye masinia na Soda juu hata kama hutaki! Na tutakufukia futi 6 kama kawaida. Huo ndio mwisho wetu sote hamna atakaekwepa wala kuweka ngumu.
 
uzu
Uzuri ni kwamba hata wewe ukifa tutakula Pilau nyama kwenye masinia na Soda juu hata kama hutaki! Na tutakufukia futi 6 kama kawaida. Huo ndio mwisho wetu sote hamna atakaekwepa wala kuweka ngumu.
Sawa mkuuu😃
 
Naweza kuja kutoa rambi rambi na siku ya kuzika au muda wa kuzika nisiwepo, na mwingine anaweza kutoa rambi rambi na siku ya kuzika au muda wa kuzika akahudhuria
Tuachane na anaetoa rambirambi alafu siku ya kuzika haji,huyu katoa.

Tuje na huyu anaetoa rambirambi alafu rambi rambi yake kumbe ndo inapika chakula,kwa hiyo huyu hajatoa rambirambi kwa wafiwa bali kajitolea mwenyewe tu mchango wa kula na kuleta jam tu msibani.

Rambirambi yake ilikuwa asile pale ili iwafaidishe wafiwa,lakini mnachanga alafu mnanunua chskula mnapika,mtasemaje kuwa mumemchangia mfiwa wakati nyie wenyewe ndo mumekula chenu.

Huu sio uungwana,uungwana mchange alafu munawapa wafiwa na kama chakula nyie ndo muwapikie wafiwa wale sio mle nyie mazee.
 
Wakati mkikamilisha mafunzo ya kiimani hasa wakatoliki huwa mnaambiwaga mkristo ana sherehe tatu. Kuzaliwa (kubatizwa), Kuoa na kufa. Sasa sielewi kwamba somo la baba paroko hukulielewa au umeamua kukaza ubongo tu?

Definition ya Sherehe; ni tafrija fupi inayohusisha kula na kunywa.
Kwa akili yangu nisingekubaliana na maneno ya paroko kwa sababu kufa sio jambo la kufurahia kwa wafiwa.

Mtu anakufa unalia kwa huzuni na majonzi tele alafu how uniambie ni sherehe 😃😃
 
Kweli halafu anaenda kukuchongea kwa wafiwa eti hujala unahisi wamechanganya kitu kwenye chakula
Hapo tatizo ni huyo mchonganishi na wala sio wewe tatizo.

Hivyo aache uchonganishi tu
 
Mkuu umeanzisha uzi lakini sio kila comment lazima ujibu. Acha mjadala ujiendeshe
Hapo tatizo ni huyo mchonganishi na wala sio wewe tatizo.

Hivyo aache uchonganishi tu
 
Wanaopika sio wafiwa wa karibu, ni majirani na ndugu wa mbali wa waliofiwa. Sasa mwambie mkeo siku nyingine akienda msibani kwa jirani akasaidie kupika, sio anakaa tu mkao wa kusubiri ahudumiwe ubwabwa wa msibani
Sawa nitamuambia.

Nilichopinga mimi suala la wafiwa kugaramia chakula kwa ajili ya wazikaji,nadhani hukuelewa uzi.

Kwa ulivyosema wewe ndivyo inavyotakiwa iwe yani wanaokuja msibani ndo wachangie kama kupika papikwe wasaidiwe wafiwa.
 
Jibu zinazohitaji jibu.
Mimi sijajibu.

Wapi umeuliza mkuu ?
Mimi nimechangia katika maneno yako(comment yako)

Lakini kama uliuliza swali basi naam lile ni jibu,ila kama hukuuliza basi yale ni maoni tu,na maoni ni haki yangu kutoa.

Ila kama nimekukera basi tusameheane mkuu
 
Back
Top Bottom