Suala la wafiwa kuandaa chakula kwa ajili ya wanaokuja kuzika ni utaratibu wa kupigwa vita

Wewe endelea kujibana na hizo mali zako, siku ukifa tuko pale kupiga pilau na soda... dadadeeki!
Ahahhahaha daah haya bwana
Ila watu wa roho mbaya kwel.,chakula msibani it's is not a big deal...hizi ni chembechembe za roho mbaya...jaman...ebu mtoa mada fikiria vingine ila sio chakula msibani,...
Mkuu aliepatwa na tatizo ama msiba anatakiwa asaidiwe au yeye ndo asaidie watu ?

Je kwa nini kula msibani isiwe ni malipo ya kwenda kumzika ndugu yao ?
 
Ila niseme ukwel ,misaba ya saiv inaenda kisasa..zaid kuliko zaman ,nakumbuka kwenye kikundi cha mama yangu palitokea Mwana kikundi wao kufiwa na baba yake...,kilichofanyika kikundi chake kiligharamikia shuhuli za msiba kwa asilimia kubwa..ila asilimia..chache ndio anaachiwa mfiwa...,
 
Nadhani ukija kuwa mkubwa na kujua majukumu ya wakubwa.... utagundua chakula wanachokula waombolezaji hakitolewi na mfiwa bali waombolezaji, ndugu, jamaa majirani na marafiki hujichangisha na wao ndio huhakikisha kinaandaliwa, kupikwa na kupakuliwa....
 
Nadhani haya majibu uliyotoa yalikuwa ni kwa ajili ya mtoa mada... Ata mimi nmechangia kama wewe! sasa sielewi huo ukubwa wa kuchangia na majukumu unaozungumzia ni upi...
Exactly... ulikuwa ujumbe wa mleta mada. Samahani kama nimekukwaza kwa kukunukuu kwa bahati mbaya
 
Uchoyo tabia mbaya, faraja inaendana na kula na majirani, ndugu na marafiki.

Mleta mada hujafiwa, ukifiwa hutatamani waondoke. Wakiondoka upweke unasumbua.

Chakula ni m*vi, ni kinyesi, siyo kitu ya kukosesha mtu usingizi.
Mwakaleli, wakija msibani, wanabeba, mahindi, maharage, viazi, mafuta n.k. mjini wanakuja na hela.

Basi hutaki kuwalisha, ukachimbe kaburi wewe, ukazike wewe, ukimaliza waje kukupa pole.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Daaah, mkuu hakika wewe ni jembe. Umefafanua kwa umakini na hekima ya hali ya juu sana mzee baba. Asante sana mkuu. Hakika unautendea haki utu uzima wako.
 
Alaa kumbe kile chakula ni malipo ya wao kukuchimbia kaburi na kukubebea marwhemu wako sio ?
 
Daaah aisee hatari sana
 
Mkuu, mimi binafsi ninadhani ulipaswa kuhimiza zaidi watu kuchangia fedha na chakula katika changamoto hii ya dharura ya msiba na sio kuweka msimamo mkali wa kugoma kuwapa chakula waombolezaji au kuwapa chakula kwa kuwabagua kuwa huyu ni wa mbali na yula ni wa karibu.

Ninadhani una jambo zuri sana la kuzungumza ila umeliongelea kwa namna ambayo sio sahihi.
 
Hata sikuelewi unasema nini ndugu.
Umesema hujisikii vizuri kuona wafiwa wakigharamia chakula kwa waombolezaji, kwa hiyo nilikuwa naongea jinsi waombolezaji wanaweza kutoa michango ya fedha au vitu kama namna ya kufariji wafiwa
 
Amen mkuu.
Nafsi zote zinapita njia hiyo, kuagana vema ni ubinadamu.
Hakika njia yetu ni moja mkuu na chakula kwa mgeni ni sehemu ya utamaduni wetu sisi waafrika. Mgeni akija nyumbani kama sio kumpa chakula basi atakunywa soda au maji. Hivyo ndivyo tulivyokuzwa na hiyo ndio desturi yetu sisi waafrika.

Mimi ninaona huyu ndugu yetu safuher alipaswa kusisitiza watu kutoa michango katika misiba kadri ya vipato vyao na sio kubagua utoaji wa huduma ya chakula.

Michango ya msiba ndio ilipaswa kuwa dhima kuu ya mada hii.
 
Mchango tunachanga wenyewe. Mfiwa ww ni kuloloma tu, kikiiva unaletewa. Kupika tunapika wenyewe tatizo liko wapi?
Au huko pemba mfiwa ndio anawajibika kila idara?
 
Mchango umechangwa laki tatu

Gharama za chakula kwa wafiwa laki nne.

Ni sawa ndugu wa marehemu umewatia hasara ya laki moja nzima,bado ni gharama tu.

Ikiwa majirani watawachangia wafiwa haina shida.
Hiyo familia inaonekana ni ya Hali ya chini Sana au haina ndugu ambao wako tayari kubebana. Hiwezi ukawa mtu wa karibu na marehemu either rafiki au ndugu na kipato unacho ukaruhusu aibu ya aina hii. Mfiwa anatakiwa afarijiwe na sehemu ya kumfariji ni kuubeba msiba wake kwa mikono miwili.
 
Hujasoma mada yangu ukaielewa,umesoma coment ambazo nazo nyingi hazijaelewa nani kakusudiwa.

Rejeea uzi pengine ukaelewa makusudio.
 
Umesema hujisikii vizuri kuona wafiwa wakigharamia chakula kwa waombolezaji, kwa hiyo nilikuwa naongea jinsi waombolezaji wanaweza kutoa michango ya fedha au vitu kama namna ya kufariji wafiwa
Ni kweli hilo lipo,ila isiwe kuwa nakupa alfu kumi mfiwa alafu wewe unanipikia chakula cha alfu hamsini,hapo hujanifariji kwa alfu kumi yako,umeniongezea mzigo tu.

Zipo jamii hufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…