Suala la Wamachinga: Kuwatimua DC na DED inaweza kuonekana ni kuwatetea "wanyonge" lakini ni kuendeleza kero kwa wananchi

Suala la Wamachinga: Kuwatimua DC na DED inaweza kuonekana ni kuwatetea "wanyonge" lakini ni kuendeleza kero kwa wananchi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Tumeona karibuni Mama Samia kamtumbua DC na DED huko Morogoro.

Suala ni namna ya kuwaondoa Machinga barabarani.

Kwanza, kuwaondoa Machinga na kuwaweka sehemu "iliyotengwa", kwa kweli ni kutoelewa how a machinga operates.

A machinga is a small trader of no fixed abode.

Machinga angeweza angeweka na kutandika nyanya katikati ya barabara, kwenye wateja wengi!

Lakini machinga wametuhurumia, wanafunga side walks na mitaro ya maji ya mvua.

Na disposal ya waste zao ni humo humo , including human waste.

Hii ni social problem, ya miaka mingi. Kumuondoa huyu machinga hapo alipo ni shughuli pevu.

SHERIA ZA MIJI SI ZIPO?

Machinga ni kero kubwa kwa Law abiding citizens na sidhani kama serikali imewahi kutoa muongozo kisheria namna ya kudeal na machinga.

Hivyo kuwatimua DC na DED inaweza kuonekana kama kitendo cha kuwatetea "wanyonge" lakini upande mwingine ni kuendeleza kero kwa wananchi wengine.
 
Lakini machinga wametuhurumia, wanafunga side walks na mitaro ya maji ya mvua.
Machinga wasilaumiwe kwa hili, serikali imeanza kuwaona machinga na aina ya ufanyaji wao wa biashara miaka mingi, kwanini haikuwa inatengeneza miundombinu yake kwa ku accommodate shughuli zao kama inavyofanya kwenye kuweka hifadhi ya barabara na side walks hivi sasa? in other words serikali inapojenga barabara zake ione umuhimu wa kukumbuka uwepo wa side walks na maeneo ya machinga wakati huohuo
 
Machinga wasilaumiwe kwa hili, serikali imeanza kuwaona machinga na aina ya ufanyaji wao wa biashara miaka mingi, kwanini haikuwa inatengeneza miundombinu yake kwa ku accommodate shughuli zao kama inavyofanya kwenye kuweka hifadhi ya barabara na side walks hivi sasa? in other words serikali inapojenga barabara zake ione umuhimu wa kukumbuka uwepo wa side walks na maeneo ya machinga wakati huohuo
Thinking hii nayo ni ya kimachinga.

Mtu halipi kodi wala tozo za Halmashauri ili kujenga hiyo miundombinu.

Tutajenga nchi ya kimachinga.
 
Suala la wamachinga halina shortcut, Serikali iweke mpango mzuri wa kudeal na hilo suala

Wamachinga ni raia wenzetu wanaotafuta kula yao ya kila siku, kuwaondoa bila mpango maana yake unataka wafe kwa njaa, sasa hakuna binadamu anayeweza kukubali wewe usimame katikati ya njaa yake, mtazinguana.

Serikali yenyewe ndo ilifanya hili suala kuwa la kisiasa, sasa chickens are coming home to roost, ni wajibu wa serikali kulisolve hilo, Wamachinga hawana kosa, hakuna kosa kwenye kutafuta rizki halali ili usife njaa!.

Mambo ya mipango miji mtajua wenyewe, maadamu keshalipa 20000 ya kitambulisho chake na mlimhakikishia kuwa atafanya baiashara popote bila kusumbuliwa basi timizeni ahadi yenu!
 
This is a Huge Problem na hakuna mtu kwa sasa (hususan anayetegemea kupigiwa kura na hao majority) ambaye atachukua maamuzi magumu, easy way out ni kupiga dana dana na ku-buy time, kufumba na kufumbua miaka mitano imepita, mara kumi mzigo huo atapewa mwingine.

Root Cause inaanzia pale ambapo kama taifa hatuna policy za kuwaondoa watu mitaani bali tunazidi kuwaambia vijana wajitafutie kila mtu kivyake.

(Nchi ya Bora Liende)
 
Hicho ni kielelezo cha misingi mibovu ya uchumi. Tanzania soko la ajira ni jembamba sana ndiyo maana mpaka vijana waliomaliza vyuo vikuu wanakimbilia kufanya biashara za kutembeza bidhaa za madukani.

Zamani machinga alikuwa ni darasa la 7 kwenda nyuma na hususan watu wa Mtwara. Ila sasa hivi kila kabila na kila kiwango cha elimu kina machinga.

Watengeneza sera wetu wamepotea sana katika hili. Namkumbuka Lowassa mwaka 2014 au 2015 alisema ajira kwa vijana ni bomu linalosubiriwa kupasuka.

Awamu ya 5 chini ya Mwendazake au Hamnazo kwanza yenyewe haikuajiri mpaka itokee dharura, hivyo kwa miaka 5 yawezekana kati ya graduates 100,000 waliofuzu pengine imeajiri 5,000 tu, chini ya 5%.

Pili Awamu ya 5 ilipiga vita sekta binafsi kwa kufilisi mabenki, kuwanyang'anya fedha matajiri, kuwa harass matajiri Kama Yusuf Manji, kuwabambikiza madai ya UWONGO makampuni ili Serikali ipate fedha kama Halotel, Vodacom etc.

Halafu mazingira ya uwekezaji hayakuwa rafiki. Toka alipokuja DANGOTE wakati wa JK hakuna muwekezaji mwingine serious aliyeongezeka nchini kwa miaka 5 ambaye angeleta mtaji na ajira. Sasa watu wanaendelea kuzaliana, wahitimu wanaongezeka kufuzu, Ila AJIRA zinapungua.

Wachumi wanasema "there is inverse relationships between population growth and economic expansion".

Mwishowe mtoa mada nilitaka nikuambie kuwa hali unayoiona mitaa ya DSM ndiyo hali halisi ya uchumi wa Tanzania mnaoambiwa umehamia uchumi wa kati. Ni aibu hata pale City Centre karibu na Sanamu ya Askari upande wa IPS kuna Mama Ntilie wanapika kwa mkaa na kuni.
 
That's very correct...

Naona na yeye anafuata njia ileile ya Mwendazake.

Kutumia kigezo cha "kutetea wanyonge" ili kupata populism ya kisiasa. This is wrong na sasa anaanza ku - loose focus (umakini Wa kiuongozi) taaratibu.

Tatizo siyo DC wala DED. Tatizo ni udhaifu mkubwa wa kisera ambalo inazaa tatizo la kiuongozi.

Tatizo liko katika SERA na SHERIA za kibiashara. Hakuna kama ulivyosema mwongozo unaoweza kusimamiwa na kila DC au DED. Kwa kuwa iko hivi, kinachofanyika kila RC, DC na CCD/MCD/TCD/DED katika mamlaka ya serikali za mitaa anabuni na kuja na njia zake za kuwa treat wafanyabiashara ndogo ndogo hao kwa namna anavyoona inafaa.

Sasa kosa lao ni nini maana Rais hajawapa mwongozo wa namna ya kuwatendea hao?
 
Thinking hii nayo ni ya kimachinga.
Mtu halipi kodi wala tozo za Halmashauri ili kujenga hiyo miundombinu.
Tutajenga nchi ya kimachinga.
Hata wewe ulianza kutumia miundombinu ya serikali kabla hujaanza kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom