Suala la Wamachinga: Kuwatimua DC na DED inaweza kuonekana ni kuwatetea "wanyonge" lakini ni kuendeleza kero kwa wananchi

Yaani ni tatizo
Jana kwenye taarifa ya habari niliona morogoro sijui ndio kusherehekea kutimuliwa kwa ded na Dc
Jamaa wameamua kuingia hadi barabarani kabisa.
Kuna kiongozi alikuwa analalamika anawaambia wanavyofanya wamachinga sio vizuri , kiongozi mwingine akaibuka akasema wawaache wamsubiri RC arudi ndio adili nao
Wamachinga wa barabarani wamekuwa na viburi lakini pia wanajifanya pia wanaleta mambo ya huruma , utu na utafutaji ridhiki.
Hili suala la machinga lipatiwe sululisho la kudumu
Nashauri wamachinga watengewe maeneo rasmi wakatazwe kufanya biashara kiholela
 
Leseni yenyewe licha ya kuwa ina masharti yake lakini yanaweza kubadirishwa muda wowote au kuzuiwa, sembuse kitambulisho?!!eti hakuna kosa kwenye kutafuta riziki!!ni suala la muda tu, lakini lazima wapangwe tu kwa kufuata sheria za halimashauri.Mfano juzi kwenye ujenzi wa barabara ya DART, mbagala kuna baadhi walitaka kuleta vurugu kisa kuambiwa wapishe wajenzi waliokuwa wanataka kuchimba mitaro, wanasema waende wapi?wakawa wanazuia greda lisifanye kazi, Mtu ana kibanda chenye bidhaa za milioni tano, kipo pembezoni mwa barabara eti na yeye ni machinga!!!
Js imagine mwendokasi isijengwe kisa machinga!,.
 
This is a Huge Problem na hakuna mtu kwa sasa (hususan anayetegemea kupigiwa kura na hao majority) ambaye atachukua maamuzi magumu, easy way out ni kupiga dana dana na ku-buy time, kufumba na kufumbua miaka mitano imepita, mara kumi mzigo huo atapewa mwingine.

Root Cause inaanzia pale ambapo kama taifa hatuna policy za kuwaondoa watu mitaani bali tunazidi kuwaambia vijana wajitafutie kila mtu kivyake.

(Nchi ya Bora Liende)
Root cause ya hiki kinachoendelea kwa sasa kwa machinga ni MWENDAZAKE, hakuna kingine!!mbona kipindi cha jk halikuwepo tatizo hilo kwa kiasi kikubwa kwani sheria za miji ziko wazi na walikuwa wakikamatwa sana!!ndio maana haikuwa kwa kiwango hiki!!mfano maeneo ya mbagala siku moja lori liliacha njia kidogo likauwa wakina mama wawili waliokuwa wakiuza nyanya kwenye kituo cha daladala, yule dreva alisema mimi gari limegonga shimo likayumba, lakini bado niko barabarani?!trafiki walisema "tumesema sana juu ya hili lakini siasa ndio zinapelekea hali hii" lakini wakiamua ni siku tatu miji yote ina kuwa mieupeee!!
 
Labda ufanyike mkutano wa Wadau wote ili kupata suluhu ya kudumu
Watu wa TANROADS,TRA,Jiji/Halmashauri,Machinga wenyewe na wale wafanyabiashara rasmi wenye frame zao/wanaofata taratibu,Bwana Afya nk nk

ili kila mtu aseme njia nzuri ni ipi
Kwa sheria zilizopo
Iamuliwe way forward

Hayati aliwalea..leo huwaambii kitu
 
Root cause ya hiki kinachoendelea kwa sasa kwa machinga ni MWENDAZAKE, hakuna kingine!!mbona kipindi cha jk halikuwepo tatizo hilo kwa kiasi kikubwa kwani sheria za miji ziko wazi na walikuwa wakikamatwa sana!!ndio maana haikuwa kwa kiwango hiki!!mfano maeneo ya mbagala siku moja lori liliacha njia kidogo likauwa wakina mama wawili waliokuwa wakiuza nyanya kwenye kituo cha daladala, yule dreva alisema mimi gari limegonga shimo likayumba, lakini bado niko barabarani?!trafiki walisema "tumesema sana juu ya hili lakini siasa ndio zinapelekea hali hii" lakini wakiamua ni siku tatu miji yote ina kuwa mieupeee!!
Mwendazake alikuwa a catalyst..., lakini root cause ni majority ya wananchi wana-maisha ya kubangaiza na kila siku zinavyozidi ndio wanaongezeka exponentially bila kuondoa hilo tatizo (kuwa-absorb watu watoke mitaani) mwisho wake sio mzuri... (Tuache kujisifia kwamba watu wamejiajiri na wamekuwa wachuuzi, bali tuone ni jinsi gani ya kupunguza wachuuzi na kuongeza wazalishaji)
 
Yaani ulikuwa mzozo mkubwa!hadi ilikuja gari ya tanroad ndio wakaambiwa kwa nguvu , kwani walikuwa wana muonea mchina!!
Imagine watu na mindset hio
Hata kodi utawalipisha kweli

ila mi nafkr wapewe wanachokitafuta
Warasimishiwe vijieneo na kodi walipishwe mana mtu ana kizimba rasmi na anauza

ikiwa handled properly yaweza ongeza makusanyo ya kodi maradufu
 
Kuwaondoa machinga ni vita kali kubwa sana sidhani kamamama atapitisha salama....ugomvi mkubwa sana wako fujo nchi nzima wakiandamana watapigwa kuvunjwa miguu .....nashauri mama asiende kwa pupa
Hakuna kitu kama hicho ni kuwatia kichwa tu!!serikali inachotakiwa kukifanya ni kutoa tangazo kwa nchi nzima,kwa kutoa muda, na utaratibu mmoja, sio kila RC, ana kuja na utaratibu wake, mbona linakwisha, kwani haiwezekani waachiwe wafanye biashara maeneo wanayoyataka wao, mfano mzozo wa soko la morogoro,/Arusha ndani kuna vizimba vingi tu, lakini hawataki kwenda kule, na wale waliokubali kwenda huko, mwishowe nao wanatoka ndani kuwafuata wenzao nje, kwani ndio wanaouza!!
 
Wamachinga huwa wanapenda kukaa sehem zenye mkusanyiko wa watu wengi hasa wale ambao wapo katika movement kubwa ya kutoka sehem moja kwenda nyingine.

Kwa jiji la Dar es Salaam sasa hivi jinsi lilivyo inahitajika kubuni stendi kubwa nyingi sanaa na kuhakikisha daladala za kwenda sehem mbalimbali zinakutana katika hizo stendi.

Mfano stendi kama Makumbusho, Mwenge, Mbagala rangi 3, Ubungo, Tabata, Buguruni, Temeke, Tandika, Kigamboni, Gongo la mboto, Tegeta, Mbezi na maeneo mengi ambayo yanakuwa na movements ya watu wengi.

Stendi zijengwe kwa kuwezesha daladala ziwe zinalazimika kuwamwaga watu hapo na hapo wanatakiwa kuunganisha safari zao bila ya kutembea tena umbali mwingine kufuata daladala zingine.

Hii itasaidia sana kuwaondoa wale wamachinga wanao jipanga kando ya barabara kuvizia hizo movements za watu.

Kingine mfano wa stendi ya makumbusho pale hakuna wamachinga wengi wamejipanga kando kando ya barabara za kuingia kuelekea stendi sababu hawana huo ulazima. Wamachinga wengi wapo ndani mule stendi wamejibana.

Mtu hawezi kushuka ndani ya gari huku mwanzoni mwa zile barabara zinazotumiwa na daladala kuingia stendi ya makumbusho kisa tu anunue kitu ambacho akifika ndani mule stendi anaweza kukipata na akaunga Safari yake bila usumbufu.

Wamachinga wateja wao ni watu ambao wananunua vitu kwa kushtukiza yaani, ameona bidhaa rahisi kubebeka na akaona kule nyumbani sina hiko kitu basi ananunua na kuendelea na safari yake.

Tofuati na hayo ma Mall na Supermarket ambapo mteja huwa anajipanga kabisa kuwa naenda kufanya shopping sehemu fulani.

Kwahiyo kusema wamachinga wakusanyike sehemu sijui kama machinga Complex pale hakuna movement ya wa ya kueleweka ni kama kuwafanya wajiwekee kishopping Mall chao na kamwe hawawezi kupata wateja wao wa siku zote ambao ni watu wapita njia tu.
 
Mwendazake alikuwa a catalyst..., lakini root cause ni majority ya wananchi wana-maisha ya kubangaiza na kila siku zinavyozidi ndio wanaongezeka exponentially bila kuondoa hilo tatizo (kuwa-absorb watu watoke mitaani) mwisho wake sio mzuri... (Tuache kujisifia kwamba watu wamejiajiri na wamekuwa wachuuzi, bali tuone ni jinsi gani ya kupunguza wachuuzi na kuongeza wazalishaji)
Sasa mkuu kwa hizi nchi za kiafrika hilo ni gumu sana!kwani kilimo ndio kunaweza kuwa -absorb lakini kwa sera hizi hilo linawezekana?!!wao ni kuja na kauli mbiu tu!!na kwa sasa vijijini maisha ni kama jehanamu ndio maana wanakimbilia mijini!!mtu atalima pamba, mahindi mpunga, kwa tabu sana huku pembe jeo za kilimo zikiwa juu, ngoja bei ya mazao hao kwenye kuuza!!
 
Mambo yanabadilika mkuu
Kidogo katiba mpya tena ile ya warioba ikipatikana ndio tunaweza fikia huko!!kwani kwa sasa mgombea hasa kwenye urais hategemei kura za wananchi ili aweze kutangazwa mshindi!!ndio maana hata akiwa jeuri haina athari kwake.
 
Hii ni nchi yetu sote, matajiri na maskini wanayo haki ya kufanya biashara mijini, kinachotakiwa ni kuwapanga vizuri hawa wajasiriamali ili biashara zao zisiingiliane na biashara kubwa. Utaratibu wa kitambulisho cha mjasiriamali kinawapa fursa ya kuchangia ktk mapato ya nchi.
Umeongea vizuri sana, kila mtu anahaki ya kufanya biashara mjini, tatizo ni mipango mibovu ya watendaji wa serikali, wanataka short cut katika kutafuta solutions, na ndiyo haohao wanaotumia vibaya fadha za umma mwishowe wanatumia nguvu kuwahamisha machinga badala ya akili
 
Wamachinga huwa wanapenda kukaa sehem zenye mkusanyiko wa watu wengi hasa wale ambao wapo katika movement kubwa ya kutoka sehem moja kwenda nyingine.

Kwa jiji la Dar es Salaam sasa hivi jinsi lilivyo inahitajika kubuni stendi kubwa nyingi sanaa na kuhakikisha daladala za kwenda sehem mbalimbali zinakutana katika hizo stendi.

Mfano stendi kama Makumbusho, Mwenge, Mbagala rangi 3, Ubungo, Tabata, Buguruni, Temeke, Tandika, Kigamboni, Gongo la mboto, Tegeta, Mbezi na maeneo mengi ambayo yanakuwa na movements ya watu wengi.

Stendi zijengwe kwa kuwezesha daladala ziwe zinalazimika kuwamwaga watu hapo na hapo wanatakiwa kuunganisha safari zao bila ya kutembea tena umbali mwingine kufuata daladala zingine.

Hii itasaidia sana kuwaondoa wale wamachinga wanao jipanga kando ya barabara kuvizia hizo movements za watu.

Kingine mfano wa stendi ya makumbusho pale hakuna wamachinga wengi wamejipanga kando kando ya barabara za kuingia kuelekea stendi sababu hawana huo ulazima. Wamachinga wengi wapo ndani mule stendi wamejibana.

Mtu hawezi kushuka ndani ya gari huku mwanzoni mwa zile barabara zinazotumiwa na daladala kuingia stendi ya makumbusho kisa tu anunue kitu ambacho akifika ndani mule stendi anaweza kukipata na akaunga Safari yake bila usumbufu.

Wamachinga wateja wao ni watu ambao wananunua vitu kwa kushtukiza yaani, ameona bidhaa rahisi kubebeka na akaona kule nyumbani sina hiko kitu basi ananunua na kuendelea na safari yake.

Tofuati na hayo ma Mall na Supermarket ambapo mteja huwa anajipanga kabisa kuwa naenda kufanya shopping sehemu fulani.

Kwahiyo kusema wamachinga wakusanyike sehemu sijui kama machinga Complex pale hakuna movement ya wa ya kueleweka ni kama kuwafanya wajiwekee kishopping Mall chao na kamwe hawawezi kupata wateja wao wa siku zote ambao ni watu wapita njia tu.
Stendi yaweza kuwa option nzuri kuwa accomodate

Barabarani marufuku
 
Mama hajasema wamachinga wafanye biashara ovyo..alichochukia ni wagambo kuwapiga wale watu...mbona alisema wangeweza kuwahamisha lakini bila kutumia nguvu
Walitumia ngivu kwa sababu ya ukaidi Kama mtu ameona kutoka unawezaje kumtoa hapo kwa mfano Kama sio nguvu
 
Tatizo siyo kuwaondoa tu, wawekee mazingira mazuri ya biashara maeneo ndani ya miji, siyo wanawaswaga kwenda huko nje ya miji ambako hakuna biashara.
Mkuu hiyo ni better said than done.
Yaani ni tatizo
Jana kwenye taarifa ya habari niliona morogoro sijui ndio kusherehekea kutimuliwa kwa ded na Dc
Jamaa wameamua kuingia hadi barabarani kabisa.
Kuna kiongozi alikuwa analalamika anawaambia wanavyofanya wamachinga sio vizuri , kiongozi mwingine akaibuka akasema wawaache wamsubiri RC arudi ndio adili nao
Wamachinga wa barabarani wamekuwa na viburi lakini pia wanajifanya pia wanaleta mambo ya huruma , utu na utafutaji ridhiki.
Hili suala la machinga lipatiwe sululisho la kudumu
Nashauri wamachinga watengewe maeneo rasmi wakatazwe kufanya biashara kiholela
Awamu zote zinalikwepa hili tatizo kiaina.
 
Root cause ya hiki kinachoendelea kwa sasa kwa machinga ni MWENDAZAKE, hakuna kingine!!mbona kipindi cha jk halikuwepo tatizo hilo kwa kiasi kikubwa kwani sheria za miji ziko wazi na walikuwa wakikamatwa sana!!ndio maana haikuwa kwa kiwango hiki!!mfano maeneo ya mbagala siku moja lori liliacha njia kidogo likauwa wakina mama wawili waliokuwa wakiuza nyanya kwenye kituo cha daladala, yule dreva alisema mimi gari limegonga shimo likayumba, lakini bado niko barabarani?!trafiki walisema "tumesema sana juu ya hili lakini siasa ndio zinapelekea hali hii" lakini wakiamua ni siku tatu miji yote ina kuwa mieupeee!!
Ni vyema suala la Machinga lisifanywe la kisiasa, ama sivyo miji haitatawalika.
 
Kupunguza Wamachinga ni kuboresha sekta ya kilimo, ambapo asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima. Automatically watu watakimbilia shambani, vinginevyo kuwaondoa bila kutengeneza mazingira rafiki kwao ni kuwaonea. Msisahau ni ndugu na jamaa zetu, na hakuna anayependa kufanya kazi inayoonekana kudharauliwa. Na wako na familia za kulisha na kusomesha kama walivyo makundi mengine kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom