Subaru forester SJ5 / FB20 ni mgonjwa wa kansa anayetembea barabarani

Ninayo na nimeshatembelea zaidi ya km elfu 40 na oil naweka 5W30 sijakumbana na tatizo lolote.

Hao mafundi ni feki, wanatumia vitu feki.
Wabongo wakinunua gari hawajishughulishi kusoma manual za gari hizo.

Matatizo ya gari yanaletwa na vitu vingi sana, ila wengi kwenye subaru watakwambia oil tu wanasahau uzembe wao na mafundi kanjanja wanaowapa hizo gari kutengeneza.
 
Puma niliwafuata kununua 0W20 hawana. Option zikabaki mbili tu, Atlantic au Liquimolly. Nasikia Castrol wanazo ila naiogopa sana Castrol.
 
Unatumia Aina gani ya oil mkuu maana wengine wametumia 5W - 30 bado engine zimekufa
Mkuu, usiweke oil ambayo haijawa recommended kwenye manual ya gari yako.

Sasa kama jamaa hapo anatumia 5W - 30 kwenye FB20 baada ya siku kadhaa atakuja na uzi subaru ni mbovu na zina matatizo.

Na hizo oil kuna SP, SN, SM, SL zote unakuwa umeandikiwa kwenye manual sasa wengi wetu haya mambo hatuelewi, tunaenda tu kwa kukariri.

Tujishughulishe jamani kufatilia mambo tutalaumu milele na milele hizo gari.
 
Castrol Original kuipata shughuli kweli. Nadhani ndio oil inayoongoza kwa kuchakachuliwa. Toka wavunje ushirikiano na Puma, sijui ata mnanunua wapi OG.
Ukihitaji nambie nikutumie unapokea hapo daslm kutoka kwenye Truck iliyobeba kutoka SA kit yote ya Service ya gari ila gari ziwe hizi za Mabeberu ndio kaburu anazo..
 
Puma niliwafuata kununua 0W20 hawana. Option zikabaki mbili tu, Atlantic au Liquimolly. Nasikia Castrol wanazo ila naiogopa sana Castrol.
0W20 PUMA hawana.

Kwenye kifuniko cha oil cha Subaru SJ5 wameandika 0W20 ila kwa mazingira ya hali ya joto nchi yetu si salama kwa hii oil.

Kwenye manual wameandika tumia 0W20 ila ukikosa unaweza ukatumia 5W30 ama 5W40 ila next service uweke 0W20.

Kama mtengenezaji ameshauri.unaweza kutumia 5W30 kwanini mimi niwe na wasiwasi wa kuitumia muda wote.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…