Mwaka huu inshaallah mambo yakienda vizuri shamba February nataka nivute chuma budget yangu 20-25 Million yaan mambo ya magari sijui kabisa.
Ni gari gani nzuri itanifaa kwa huku kwetu ni maeneo ya milima na barabara za vumbi kwa asilimia kubwa so itakua ni ya kuendea mjini kwa safari za karibu.
Mimi sio bishoo yaan kikubwa gari iendane tu na hali na ambayo haitanisumbua 😂
Nayatamani yale Maford Ranger japo najua litakua mkasi sana !!Japo sijui undani wake ila linanivutia mno muundo wake, mnishauri hata kama naweza kupata linalofanania la bei ya chama 😂
Oya ile chuma nikiisukuma nimepigilia na kofia langu na nimechomekea , inanifurahisha sana najikuta kama John Dutton kwenye Yellowstone au Tommy Norris wa Landman
Nimeiga mfumo wa maisha design kama wale COWBOYS ndo maana nimejitenga mbali na mji kabisa huko ni kilimo na kufuga na kumiliki aridhi.